Tofauti ya Battery health 86% 100%

Tofauti ya Battery health 86% 100%

Joined
Dec 4, 2013
Posts
49
Reaction score
33
Leo ningependa niandike kuhusu battery health kuanzia 100% to 86% siku hizi imeibuka tabia ya watumiaji wa iphone ukimuzia simu cha kwanza ana kimbilia kutazama battery health kwa lugha isiyo rasmi tunaita (Afya ya Battery) akikuta ipo kuanzia 86% basi hanunui hiyo simu atasema kuwa battery ni mbovu. Ana taka ianzie 100% mpk 97% angalau.

Sasa iko hivi, simu nyingi sana ambazo zinauzwa sasa hivi kama 6,6plus,7plus,8plus mpaka X kukuta battery health ni 100% ama 97% juwa kwamba hiyo simu imesha badilishwa battery ili iweze kukuvutia ww mteja ununue.

Kama simu ni mpya umetoa kwenye box hapa namanisha sio zile refublish ambazo zimebadilishwa housing, ukakuta battery health ipo 86% nakushauri ununue sababu hiyo simu battery yake itakuwa original na haija badilishwa. Nasisitiza tena kama sio refublish.

Lakini ikatokea umeuziwa simu ambayo ni refublish na ukakuta battery health ni 86% omba muzaji akubadilishie battery haraka kwani hiyo simu battery yake itakuwa imeshabadilishwa na kutumika sana hivyo haitakuwa na uwezo wa kutunza charge. Mana siku hizi wauza simu wengi wanauza simu ambazo zimebadilishwa housing na unakuta battery health ipo 100% wakati simu ni refublish hii si kweli.

Hivyo usisite kununua simu ambayo si refublish sababu battery health ipo 86% nakushauri nunua tu. Ila kama ni refublish No hiyo hapana.
Niwatakie mapumziko mema.

Follow instagram page @elmuraphonerepair
#elmuraphonerepair

Tupigie +255 715798947 kwa huduma zaidi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Asante mimi mmojawapo ambae nilikua najichanga nije ninunue iphone na kigezo kimojawapo ni battery iwe juu ya 90%, ila kwa sasa hata nikiona 85% nitanunua ikiwa nitaridhika na vigezo vingine.
 
Refurbished

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
cheche IT works, Nimekuelewa sana mkuu mimi

Kingine haujaelezea zile iPhone ambazo kwenye battery health zimeandikwa service
 
Kwaio simu ni mpya, na sio refurbished na umeitoa kwenye box lake na makaratasi yake hio 86% inatoka wapi wakati haijawahi kutumika? Kitu cha kuzingatia hakuna iphone 6-8 mpya...
 
Nimecheka kwa sauti upoje lakini
😍Nafurahi ukicheka, lakini uache kunidanganya,huwa nakuona nyuzi mbali mbali unashusha Nondo ila nikichat na wewe unajidai hujui kitu yani country side Girl
 
Nafurahi ukicheka, lakini uache kunidanganya,huwa nakuona nyuzi mbali mbali unashusha Nondo ila nikichat na wewe unajidai hujui kitu yani country side Girl
Hahaha huyo unayemuonaga ni mdogo wangu ameingia kwa I'd yangu
 
Hahaha huyo unayemuonaga ni mdogo wangu ameingia kwa I'd yangu
😂 kumbe nawe kama mimi huwa unamuachia simu mdogo wako, mimi pia mdogo angu huwa anatumia hii ID na ndiyo huyo anayekupenda kila siku anakulilia,nishamshauri aache coz una babes wengi ila hataki kuskia
 
Back
Top Bottom