Tofauti na tafsiri ya kula na kulishwa nyama ndotoni

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Vema tukarejea kwenye mada zetu hizi... Huko siasani ni tabu tupu... Kunaweza kukufanya mtu sometimes uwe na frustration zako... Nitajitahidi nisiende tena kule.... Japo naona kama naidhulumu nafsi.....

Dhana ya kula chakula ndotoni si jambo baya si jambo la ajabu japo kuna wakati huambatana na matatizo ya kisaikolojia kwa sehemu! Lakini lazima tutambue kuwa lazima tuote kuota ni lazima na kuna ndoto baadhi hazina maana yoyote zaidi ya kumbukumbu ya yaliyopita.....

Kuota mara kwa mara unakula ni ishara ya kutamani kufanikisha jambo fulani katika maisha, hamu ya kuwa na mahusiano , mali ama mafanikio yoyote yale.. Chakula ni uhai bila chakula uhai uko shakani hivyo kuota unakula ni dalili za kutaka kupata uhai kwenye jambo fulani

Lakini vilevile kuota unakula hutokana na kutamani chakula fulani lakini ikatokea hukukipata lakini ufahamu wako ukahifadhi ile hamu na usiku unapolala roho yako huondoka na kwenda kutafuta chakula husika na kuiridhisha nafsi tamanifu....
Sasa turudi kwenye mada... Kuota unakula nyama na kulishwa nyama... Kuna tofauti kubwa hapa

Kuota unakula nyama ni tafsiri ni dalili ya kutaka mafanikio ama kufanikisha jambo lako kwa njia ya kudhuru ama kuumiza wengine.. Yani ufanikiwe wewe lakini ukiacha wengine na madhara... Nyama inatokana na kuondosha uhai wa kiumbe hai kingine... Hii hutokana na mawazo tuwazayo bila kujua madhara yake kiroho... Kwa mfano penzi linazingua unatamani kurekebisha mambo lakini masharti ya mtaalam unatakiwa upate kuku wa kafara....

Ni kitu kama hiki... Unatamani cheo kazini, mvuto ama umaarufu nk unaambiwa dawa yake lazima itengenezwe na damu na mzoga wa mbuzi... Ni vitu kama hivi... Hivyo kupitia ndotoni hujidhihiri kwa njia ya kula nyama. Kwamba unashibisha nafsi huku kiumbe kikipoteza uhai

Sasa linapokuja suala la kulishwa nyama ndotoni... Hiki ni kitu tofauti kabisa.. Hizi ni ndoto zenye kuakisi uhalisia.. Ni ndoto za kichawi na unacholishwa ni nyama halisi kwa njia za kishirikina na nyama hizo si nzuri si nyama za wanyama tulao bali ni nyama za mizoga ya kenge nyani mbweha fisi konokono hata panya nk...

Sio nyama nzuri kwakuwa zina madawa ya kudhuru kiroho na hushibisha na hata kuvimbiza.. Hujaza tumbo kabisa na kukufanya ushindwe kula chochote.... Na tafsiri yake ni moja tu kukufunga usifanikiwe tena kwenye lolote.. Kwamba ukishakula na kushiba huwezi kula tena....

Namna bora ya kutatua tatizo hili ni kitunguu saumu na ndimu tuu... Kabla ya kulala hakikisha unalamba ndimu au kutafuna kipande cha kitunguu saumu ama vyote kwa pamoja... Kwa njia hii utakuwa umeidhibiti hiyo hali

Jr
 
ndugu mshana jr ikiwa ukiota kifo tafasiri yake ni kukiepuka vipi kuhusu kuota ndoa ina maana umeiepuka? Asante!
Unajua watu hufa kabla ya kufa kabisa.

Mtu anakuonea kijicho anakuendea kwa mganga ili akuondoe duniani.. Anapewa beseni la maji mara anaona sura yako majini. Anapewa kisu achome yale maji akisita umepona na huko uliko utashtuka toka kwenye ndoto mbaya ya kifo. Asiposita umeondoka.

Lakini vilevile usiku roho huenda kuvinjari ulimwengu huko hukutana na hathatari mbalimbali na ndio mwanzo wa ndoto za kifo
 
ndugu mshana jr ikiwa ukiota kifo tafasiri yake ni kukiepuka vipi kuhusu kuota ndoa ina maana umeiepuka? Asante!

Samahani sana mkuu Mshana yupo busy kwasasa ngoja nimsaidie kujibu.

Suala la kuepuka kufa hilo haliwezekani hata kidogo, ukiandikia kufa Tanzania unakufa hata kama utakua Ulaya.

Naomba twende sawa hapa. "Kuna kuepuka ajali na kunusurika kufa". Huwa kwenye taarifa za habari wanatoa sana neno hili " KUNUSURIKA KUFA".

Naomba muweke mawazo yenu kwamba hakuna ambae anaweza kukunusuru usife. Mwenye uwezo huo ni Mungu pekee. Kifo kikiandikwa kimeandikwa. Ila ajali ina kinga.
 
Unajua watu hufa kabla ya kufa kabisa... Mtu anakuonea kijicho anakuendea kwa mganga ili akuondoe duniani.. Anapewa beseni la maji mara anaona sura yako majini. Anapewa kisu achome yale maji akisita umepona na huko uliko utashtuka toka kwenye ndoto mbaya ya kifo... Asiposita umeondoka
Lakini vilevile usiku roho huenda kuvinjari ulimwengu huko hukutana na hathatari mbalimbali na ndio mwanzo wa ndoto za kifo
Unaonekana una ujuvi mkubwa sana kwenye haya mamno, nitakutafuta tufanye collabo!
 
Samahani sana mkuu Mshana yupo busy kwasasa ngoja nimsaidie kujibu.
Suala la kuepuka kufa hilo haliwezekani hata kidogo, ukiandikia kufa Tanzania unakufa hata kama utakua Ulaya.
Naomba twende sawa hapa. "Kuna kuepuka ajali na kunusurika kufa". Huwa kwenye taarifa za habari wanatoa sana neno hili " KUNUSURIKA KUFA". Naomba muweke mawazo yenu kwamba hakuna ambae anaweza kukunusuru usife. Mwenye uwezo huo ni Mungu pekee. Kifo kikiandikwa kimeandikwa. Ila ajali ina kinga.
Karot
 
Utajali kujibu kwenye context ya ndoa? maana hapo ndo lilikuwa swali la msingi, maelezo ya awali yalikuwa kwenye kuunda hoja tu!
 
Unajua watu hufa kabla ya kufa kabisa... Mtu anakuonea kijicho anakuendea kwa mganga ili akuondoe duniani.. Anapewa beseni la maji mara anaona sura yako majini. Anapewa kisu achome yale maji akisita umepona na huko uliko utashtuka toka kwenye ndoto mbaya ya kifo... Asiposita umeondoka
Lakini vilevile usiku roho huenda kuvinjari ulimwengu huko hukutana na hathatari mbalimbali na ndio mwanzo wa ndoto za kifo
Aiseee

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
 
Utajali kujibu kwenye context ya ndoa? maana hapo ndo lilikuwa swali la msingi, maelezo ya awali yalikuwa kwenye kuunda hoja tu!
Ahsante sana mkuu nimekusoma kidogo, ila kabla sijajaribu kukujibu swali lako nakuomba kama nimekosea unisamehe sana.

Suala la kuota ndoa sihafahamu ulikusudia vipi, " kuota kwamba umeifunga au imevunjika? Naomba unisaidie hapo ili twende sawa.
 
Back
Top Bottom