Dadio
JF-Expert Member
- Mar 14, 2012
- 359
- 42
Naombeni kujua tofauti dhidi ya Ipad NA Tablet
==========
By Millah
Kaka kwanza pole kwa majibu ya ajabu, labda somo la kwanza kuwa makini katika kuuliza maswali ukumbi huu, watu ni wakali mno na wana majibu sahihi kabisa lakini pengine sio yenye kuridhisha sana.
Labda umekusudia kuuliza tofauti kati ya iPad na Tablet nyingine.
iPad kama walivyosema wazungumzaji waliopita ni Tablet ya Apple, na katika ulimwengu wa leo ni vigumu kutofautisha tablet kama hujaweka kigezo maalum cha kuangalia tofauti, kwa hiyo ili kuifupisha mada nitazungumzia tofauti moja tu na kigezo ni OS (operating System) au niseme software kuu inayoiendesha kompyuta.
iPad inatumia iOS: sifa kubwa za OS hii ni kuwa inaongoza kwa Apps na ni rahisi kuitumia na kwa vile soko lake la apps lina usimamizi basi apps zake nyingi ni za quality kubwa. Hata kampuni kubwa kwanza hulengesha kutoa app kwenye iPad kabla ya kwenda kwengine.
Tablet za Android: Hizi ziko nyingi kama utitiri, za bei rahisi, feki, za quality ya juu, convertible, yaani utachoka mwenyewe: Sifa kubwa ya Android ni OS ambayo inapendwa na watundu wa kompyuta kwa vile ina customisation zaidi kuliko OS nyingine yoyote katika simu na tablet. Yaani katika siku 365 za mwaka wewe unaweza kuifanya simu yako iwe na muenekano tofauti kila siku bila kurudia muenekano walau kwa miezi 3 mizima. (ingawa hii inategemea tablet yenyewe, na customisation zaidi iko kwenye simu)
Tablet Za Windows 8: Hili ni kundi jipya, sifa kubwa ya tableti zake ni kuwa zinatumia OS ile ile ya laptop kwa hiyo unaweza kutumia kufanya kazi zako kama tablet na kama laptop, nyingi huwa ni kubwa na nzito kidogo ukifananisha na zile za Android 7" au iPad Mini ambayo ni 7.9". Ukubwa wake nyingu huanzia 10.1 iches, na OS hii ina makundi mawili makubwa nayo ni Windows 8 RT na Windows 8 pro, RT haina uwezo wa ku-run baadhi ya software za zamani. Hivyo kama unalengesha kununua basi uwe makini unanunua Windows 8 gani.
kwa vile ni soko jipya lina ukame wa apps katika Windows 8 ingawa linakuwa kwa haraka kiasi, kwa mtazamo wangu ni mapema mno kutegemea Windows 8 kama typical tablet (kwa mtazamo wa uwezo wa ipad na Android Tablet)
Pia kuna OS nyingine mikangafu ambayo bado haijapata uhai wa kutosha kama vile Blackberry OS ya Blackberry Playbook na hayati Web OS iliyotumika kwenye tablet ya HP, pia ziko ambazo ndio zimezaliwa kama vile Ubuntu OS.
Nadhani utakuwa umepata picha kidogo kama itakuwa nimepatia kulibuni swali lako.
Kama umekusudia kununua tablet na wewe ni mpya katika mambo haya basi ushauri wangu nunua iPad, laa kama umeshatumia simu za Android na iPhone basi chukua exprience ya simu uamue ipi ni bora kwako.