mimi sio fundi wa simu ila nina uelewa kiasi wa mambo kama hayo.
Scatter file ni TXT file ambayo inabeba taarifa au Location ya files zote zilizopo kwenye Folder la ROM.
kwa mfano : una folder la ROM ya TECNO f1, hilo folder la ROM lina mafaili na mafolder mengi sana na mengine yapo ndani ya folder , ndani ya folder lingine. Sasa scatter file ndio inayoiambia program ya kuflash simu kwamba file fulani lipo wapi, na file lipi linaanza kuflashiwa na lipi ni la mwisho.
.BIN file ni sehemu ya yale ma file mengi ya kwenye ROM. .Bin huwa ni extension ya flash files au firmware za microchip. Format nyingine ni kama vile - .HEX file extension.