Today last year I lost my Mother

Today last year I lost my Mother

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,702
Amkeni mkajenge familia, na nkuijenga nchi, wenye changamoto za kiafya, kiuchumi MUNGU wa Mbinguni awasimamie.

Mwaka jana ndio mwaka ulionipa uchungu saaaana maishani mwangu maana nlipoteza mama na baba.

Najua kuna yatima wengi ila nazungumzia upande wangu.

Tarehe 4/2/2021 ndio siku mama yangu alipo aga dunia pale Mloganzila Hospital.

Tulimuuguza saana baba kwa miaka mingi ila yeye akatukimbia ndani ya wiki tu akatuachia baba tumuuguze sisi.

Halafu tarehe 4/9/2021 baba akakufuata akitokea pale Bochi hospital Kwa Msuguri.

Why tarehe4?????

Why mwaka2021???

Mungu nakuachia wewe

Lala mama yangu mpenzi ila nina tumaini hili kwa kuwa nina uhakika mahali ulipo.

I'm heart broken.


1 The 4:13-18 SUV

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

Siku njema wadau. Mungu wa Mbinguni awabariki na kuwasimamia katika kila jema mnalolifanya
 
Jipe moyo mkuu, hauko peke yako.Kikubwa kuwaombea na kushukuru kwa waliyotenda hapa duniani ,maisha yaendelee.pole
 
Amkeni mkaijenge familia, na nchi, wenye changamoto za kiafya, kiuchumi MUNGU wa Mbinguni awasimamie.

Mwaka jana ndio mwaka ulionipa uchungu saaaana maishani mwangu maana nlipoteza mama na mama na baba.

Naj
Today last year
 
Siku njema kwako pia ndugu mleta mada.
Pole sana pole mno!
Tupo hapa duniani kama wageni na wapitaji, marejeo ni kwa Mungu na wenyeji wetu kadhalika ni kwa Mungu pia.

Mwenyezi Mungu awajalie nuru ya milele.
 
Pole ndugu
Ninajua uchungu unaopitia maana hata mimi December nilimzika mama yangu baada ya kumuuguza kwa miaka 7.
Asee ninajaribu kujichangamsha lakini wapiii
Bora hata baba mzazi angekuwa na ubinadamu....lakini wapiii Ana roho zaidi ya mnyama.
Kila iitwapo Leo ninammiss mama yangu mpendwa aliyejua kunipenda kupita maelezoo...such a humble soul
Mungu nijalie siku ile ya ufufuo nikutane na mama yangu...
 
Pole sana mkuu na wengine nyote mliopoteza wazazi, japo sijui maumivu yenu ila nimeshawwhi kuishi bila mzazi mmoja kwa miaka mingi tu, hivyo naelewa ni kwa kiasi gap la mzazi likiwa wazi hakuna anaeweza kuliziba

Mungu awatie nguvu
 
Pole sana na kwangu pia, I had lost both 2 parents,Mara nyingi tunapopoteza wazazi ndipo tunapokuja kujua umuhimu wao na fadhili zao na ushauri ulio mwema kutoka kwao.
Pole mkuu but its hard to let it go
 
Back
Top Bottom