Toa maoni yako

JK anahusika na kashfa za ufisadi na mikataba mibovu ?

 • Anahusika

  Votes: 18 69.2%
 • Hahusiki moja kwa moja ila anatumiwa

  Votes: 5 19.2%
 • Hahusiki

  Votes: 3 11.5%
 • sijui

  Votes: 1 3.8%

 • Total voters
  26
 • Poll closed .

Mtu Mzima

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
395
250
Jk amekuwa akielezewa kama mtu asiyehusika na ufisadi na mikataba ya madini.Hata vyombo vya habari vilinukuliwa vikisema kuwa waziri wa nishati na madini alisaini mkataba mpya pasi na rais kufahamu.
Nini maoni yako?

Anahusika
Hahusiki moja kwa moja ila anatumiwa
Hahusiki
Sijui
 

Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,338
1,250
houseboy ataweza fanya kazi ya bosi wake bila bosi kujua???samaki mmoja akioza woote watanuka shombo tuu woote wanahusika wasituzuge at all
 

Curriculum Specialist

JF-Expert Member
Oct 8, 2007
2,731
0
Kwani angekuwa hahusiki si angesha mfukuza Karamagi siku nyingi, hiyo ni natural kwamba kama huna haki huwezi kumhukumu mkosaji, kwani hiyo hukumu itakuwa yako pia, kwani huna tofauti ya uliyemuhukumu.
 

Tluway

Member
Oct 4, 2007
15
0
Jk amekuwa akielezewa kama mtu asiyehusika na ufisadi na mikataba ya madini.Hata vyombo vya habari vilinukuliwa vikisema kuwa waziri wa nishati na madini alisaini mkataba mpya pasi na rais kufahamu.
Nini maoni yako?

Anahusika
Hahusiki moja kwa moja ila anatumiwa
Hahusiki
Sijui

Hivi ni vichekesho tu,waziri anaposafiri nje ya nchi kwa kazi nyeti kama hiyo inawezekanaje Rais asifahamu? hata huo mkataba mpya ungefanyiwa kazi wapi? anahusika maana mpaka leo angelimwajibisha....janja ..yao ...
 

mboje

Member
Oct 11, 2007
10
0
Hilo ni chnga la macho waheshimiwa. Kaka JK kwa namna moja ama nyingine ni hao hao. Kauli zake pia zinamfanya watu waamini kuwa wanakula wote, waache hiyo zugaring yao.... yumo ndani ya kapu moja ila anachungulia kwa mbali hatumuoni...
 

Mr EWA

JF-Expert Member
Mar 15, 2007
332
225
Tatizo ni kuona hata viongozi wa ngazi za juu nao wanalalamika juu ya ufisadi na rushwa hapa nani hasa anatakiwa kuwaadabisha wanaokiuka maelekezo. "hata kiongozi mwenye mamlaka yote ya kuwashughulikia wahalifu wote naye analalamika si basi akaimu nafasi yake ili huyo anayekaimu awashughulikie hawo wanaolalamikiwa na baadaye yeye arudi kwenye nafasi yake kwani pengine anawaonea haya."
 

OpenMinded

Member
Nov 15, 2007
16
0
Tatizo ni kwamba hawa watu wanadhani watanzania ni wajinga sana kiasi cha kushindwa kuona hali halisi. Ni suala liko wazi kabisa kwamba JK anahusika na hii mikataba otherwise angekuwa amechukua hatua zinazostahili
 

OpenMinded

Member
Nov 15, 2007
16
0
tatizo huwezi kuandika suala kama hili kwenye chombo cha habari maana utaulizwa ushahidi na ni wazi huwezi kuwa na uthibitisho zaidi ya ushahidi wa kimazingira kwa hiyo akili kumkichwa kaka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom