Hizi taarifa za mkopo wa Korea Kusini mbona zina utata mwingi?

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
16,464
35,703
Nimenukuu kutoka mtandao wa X kwa ndugu Martin Maranja Masese, na nimeamua kuiweka hapa ili na nyinyi Wakuu muweze kutoa maoni yenu. Maana habari za vyombo vikubwa vya habari kama Sauti ya America na Reuters vilio ripoti kama ilivyo nukuliwa hapo chini, akaja na Waziri wa uwekezaji na yeye akatoa tamko lake, Balozi wa Korea Kusini naye akazungumza kama ilivyonukuliwa.

Na Jokate Mwegelo Katibu wa UWT naye akaja na matamshi yake. Najiuliza kwanini Viongozi wa Serikali kila mmoja amekuwa akitoa kauli inayokinzana na mwenzake? Kwanini Msemaji Mkuu wa Serikali ameshindwa kuja na kauli ya moja kwa moja kuweka taarifa sawa zinazohusiana na huu mkopo?

VOA/REUTERS; Tanzania imepewa mkopo na Korea Kusini na kutoa bahari na madini yanayotumika katika teknolojia ya nishati safi (nikeli, Lithiamu, grafiti)

KITILA MKUMBO; Tumesaini mkataba kwa lengo la kushirikiana kuboresha teknolojia ya uvuvi, kujenga bandari za uvuvi na viwanda kuchakata Samaki.

TOGOLANI MAVURA; Tanzania haijasaini mkataba wowote na Korea unaohusu bahari wala madini katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea.

JOKATE MWEGELO; Tanzania imepata mkopo wa Sh6.8 trilioni. Mkopo wa masharti nafuu, utakaolipwa katika miaka 40 kuanzia mwaka wa 26 kwa riba ya 0.01%.

WATANZANIA; Hakuna tatizo, tunaomba kupewa mkataba wa mkopo, tusome wote. Inawezekana siyo bahari na madini tu mmeuza, labda na makazi yetu.

Brigedia Mtikila, MMM.

Pia soma
 
Hata DP world walibisha sana lakini sasa bandari imechukuliwa na mapato ni siri kati ya Samia na DP world.

Hata mkopo wa Korea itakuwa hivyovyo we subiri tu, muda ni mwl mzuri.
 
Katika taarifa zote chukua ya Waziri Prof. Kitila Mkumbo maana ndio taarifa Rasmi. Ila ukitaka kujichanganya, chukua za wengine.
 
Nilimsikia msemaji wa serikali kupitia EFM anasema riba yake ni 0.01% tena kwa miaka 40.
Nilijiuliza maswali mengi sana ya kihasibu.

Mfano rahisi, au basi!
 
Mkuu ili swali uwa najiuliza sana kwamba TISS na JWT hawa sio watanzania kama sisi na je ata kama wao wanalipwa mishahara minono ya kuwaziba midomo hawana ndugu wanao walilia kuhusu ili?
. Wahuni walio tengeneza DP WORLD, ni hao hao ndo wanazidi kutafuna hovyo hovyo nchi ya TANGANYIKA.

. Mda mwingine najiuliza, hivi J.WT wana kazi gani hapa TANZANIA ☹️
 
TISS na JWTZ mko wapi? Kazi yenu ni nini hasa iwapo mambo yako hivi huku mkiangalia tu?

Yaani nchi ya Tanganyika inauzwa kwa nchi za kigeni na Rais wa nchi nyingine ya kigeni (Zanzibar) kiasi hiki huku nyie mkiwa kama "macho na masikio ya siri" ya wana wa nchi hii mkiwa mnaangalia tu bila kuchukua hatua kuzuia? Really?

Je, ni kwa sababu mmeungana na wana rushwa na mafisadi ya CCM kuihujumu nchi kwa kuwa mnatulizwa kwa mishahara mikubwakubwa na marupurupu mengi na kuwaacha ndugu zenu wa Vijijini na mijini wanaogelea kwenye umasikini uliosababishwa na viongozi hawa wa CCM wanaoiba na kuficha mabilioni ya mapesa nje nchi?

TISS na JWTZ chukueni hatua. Wananchi tuko nyuma yenu!!!
 
Mkuu ili swali uwa najiuliza sana kwamba TISS na JWT hawa sio watanzania kama sisi na je ata kama wao wanalipwa mishahara minono ya kuwaziba midomo hawana ndugu wanao walilia kuhusu ili?
. Inachukiza sana mkuu, yule bibi ilitakiwa ni wakumpa kauli moja tu..

. Huyu bibi ilitakiwa apingiwe majukumu mengine... Lakini siyo kukaa kwenye nyumba nyeupe.
 
Back
Top Bottom