TMA yatoa taarifa ya kimbunga Batsirai

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
TMA yatoa taarifa ya kimbunga Batsirai

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa Kimbunga Batsirai katika maeneo ya kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi.

TMA imesema Kimbunga hicho tangu kilipojitokeza katika bahari ya Hindi Januari 27, 2022 na kwa sasa kimesogea katika maeneo ya kisiwa cha Madagascar.

Kwa taarifa iliyotolewa leo na Mamlaka hiyo imesema uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonyesha kutokuwepo kwa uwezekano wa Kimbunga hicho cha Batsirai kufika katika Pwani ya Tanzania.

Imeeleza kuwa uwepo wa kimbunga hicho baharini unatarajiwa kuathiri mifumo ya hali ya hewa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha ongezeko la mvua, vipindi vya upepo mkali unaofika na kuzidi kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa baharini yanayozidi mita 2 hasa kwa maeneo ya ukanda wa pwani.
 
Nakiona hapo 57kt sio mchezo
Screenshot_20220205-104305_Chrome.jpg
 
TMA banaaaa sijui kwanini huwa nawafananisha na TFF

TMA siku zote huwa wanatabiri matukio yaliyokwisha tokea
Hujui maana ya probability !!?
taarifa yao haiwezi kuwa certain kwa asilimia 100
huwa wanazungumza kabla ya matukio
 
Mbona kimbunga kimepita usiku,au hamjasikia ule upepo wa usiku wa kuamkia leo nyie?
 
Hujui maana ya probability !!?
taarifa yao haiwezi kuwa certain kwa asilimia 100
huwa wanazungumza kabla ya matukio
Sawa Mzee wa Probability ila 'TMA' za wenzetu probability to happen is 0.9 sie ya kwetu probability not to happen as predicted is 0.9
 
Back
Top Bottom