TMA - Taarifa kwa Umma: Hali ya bahari kufuatia tetemeko la ardhi la Agosti 12, 2020

Mngeriwaindi ili taarifa itufikie kabla ya tetemeko, ingependeza zaidi.
Tetemeko jana saa mbili usiku tena mapema tu, taarifa leo saa tatu tena baada ya kunywa chai kwa mayai na kongoro.
 
Hawa TMA wana uwezo wa kupima hilo Tetemeko lilikuwa na ukubwa gani au mpaka wasaidiwe na mabeberu? Hiyo taarifa kutoka kwa mabeberu ina kibali cha TCRA / Msemaji Mkuu? Tunakumbushana Sheria ni msumeno
 
Tz tunawajua hata kma lingekuwepo mpaka watu wafe ndyo waridhike sometime ni kama kafara yani. Yani unawezaje pangia tsunami kutokea au isitokee.

Chi zenye technologia kubwa zimekumbwa na matsunami kibao na wao hawakuweza kuyatabir sembuse tz et itoe uhakika kuwa hakuna Tishio la Tsunami???

Tetemeko la Arth na Tsunami hayatabiriki labda wameenda kwa waganga wa kienyeji. Tusidanganyane.
 
JPM kuapishwa kuongoza awamu ya sita!!! Una maanisha nini?
Kwani kipi usichojua hapo? Unadhani watanzania watachagua wapiga mipasho? JPM awamu ya sita haina ubishi, hapa watu tunawaza kumuongezea awamu ya saba.
 
TAARIFA KWA UMMA HALI YA BAHARI KUFUATIA TETEMEKO LA ARDHI CHINI YA BAHARI YA HINDI

Dar es Salaam, 12 Agosti 2020:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa kuhusu hali ya bahari kufuatia tetemeko la ardhi chini ya bahari ya Hindi. Leo tarehe 12/08/2020 majira ya saa mbili (2) usiku, tumepokea taarifa zilizothibitishwa na “Geological Survey of Tanzania” (GST) kuhusu tetemeko la Ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 5.9 katika eneo la kusini mashariki mwa Mkoa wa Pwani katika bahari ya Hindi.

Kutokana na Tetemeko hilo kutokea katika eneo la chini ya bahari, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imefanya uchambuzi wa taarifa za tetemeko hilo katika kituo chake cha Tahadhari ya Tsunami ili kuona iwapo kuna uwezekano wowote wa tetemeko hilo kusababisha mawimbi ya Tsunami baharini. Matokeo ya uchambuzi huo yanaonesha kuwa hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko hilo. Tetemeko hilo halikuwa nguvu kubwa na hakuna maporomoko ya ardhi yaliyojitokeza baharini ambayo yangeweza kuzalisha tsunami.

TMA inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa baharini na kutoa taarifa endapo kutajitokeza mwendelezo wa matetemeko katika eneo la Bahari.

ATHARI: Hakuna adhari zilizojitokeza au zinazotarajiwa katika mifumo ya hali ya hewa ya bahari kutokana na tetemeko hilo.

USHAURI: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawashauri watumiaji wa eneo la bahari ikiwa ni pamoja wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyokaribu na bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli kwa kuzingatia taarifa ya hali ya hewa Baharini kama ilivyotolewa awali na Mamlaka.

Imetolewa na;
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania


Pia, soma: News Alert: - Tetemeko la Ardhi latokea baadhi ya Mikoa ya Tanzania
 

Attachments

  • TAARIFA YA TETEMEKO-12-8-2020_Page_1.jpg
    TAARIFA YA TETEMEKO-12-8-2020_Page_1.jpg
    152.8 KB · Views: 1
  • tetemeko.jpg
    tetemeko.jpg
    47 KB · Views: 1
Kwani kipi usichojua hapo? Unadhani watanzania watachagua wapiga mipasho? JPM awamu ya sita haina ubishi, hapa watu tunawaza kumuongezea awamu ya saba.


Kwahiyo wewe awamu unaelewaje kwani au ulidhani nakupinga hatashinda?

Tunaposema serikali ya awamu fulani unaelewaje?
 
Hali ya hewa na tetemeko
Pimeni majumba marefu kama hayaja athirika.
Shock ilikua kubwa
Na leo jioni liketokea tena magnitude 5 rc
Nyumba ndefu zikipata shock hivi kuna shida
 
Back
Top Bottom