TMA - Taarifa kwa Umma: Hali ya bahari kufuatia tetemeko la ardhi la Agosti 12, 2020

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
TAARIFA KWA UMMA HALI YA BAHARI KUFUATIA TETEMEKO LA ARDHI CHINI YA BAHARI YA HINDI

Dar es Salaam, 12 Agosti 2020:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa kuhusu hali ya bahari kufuatia tetemeko la ardhi chini ya bahari ya Hindi. Leo tarehe 12/08/2020 majira ya saa mbili (2) usiku, tumepokea taarifa zilizothibitishwa na “Geological Survey of Tanzania” (GST) kuhusu tetemeko la Ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 5.9 katika eneo la kusini mashariki mwa Mkoa wa Pwani katika bahari ya Hindi.

Kutokana na Tetemeko hilo kutokea katika eneo la chini ya bahari, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imefanya uchambuzi wa taarifa za tetemeko hilo katika kituo chake cha Tahadhari ya Tsunami ili kuona iwapo kuna uwezekano wowote wa tetemeko hilo kusababisha mawimbi ya Tsunami baharini. Matokeo ya uchambuzi huo yanaonesha kuwa hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko hilo. Tetemeko hilo halikuwa nguvu kubwa na hakuna maporomoko ya ardhi yaliyojitokeza baharini ambayo yangeweza kuzalisha tsunami.

TMA inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa baharini na kutoa taarifa endapo kutajitokeza mwendelezo wa matetemeko katika eneo la Bahari.

ATHARI: Hakuna adhari zilizojitokeza au zinazotarajiwa katika mifumo ya hali ya hewa ya bahari kutokana na tetemeko hilo.

USHAURI: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawashauri watumiaji wa eneo la bahari ikiwa ni pamoja wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyokaribu na bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli kwa kuzingatia taarifa ya hali ya hewa Baharini kama ilivyotolewa awali na Mamlaka.

Imetolewa na;
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania


Pia, soma: News Alert: - Tetemeko la Ardhi latokea baadhi ya Mikoa ya Tanzania
 

Attachments

  • TAARIFA KWA UMMA_TETEMEKO BAHARINI (1).pdf
    80.8 KB · Views: 8
Sidhani kama TMA wanamakosa au lawama yoyote. Matetemeko huwa hayatabiriki before vinginevyo nchi kama Japan na nyinginezo wangekua wanajitayarisha kukabiliana na hilo janga

Taarifa na maelekezo waliyoyatoa ni sahihi kabisa na yametolewa kwa wakati. Nadhani tuwasapoti badala ya kuwashutumu
 
Afadahli mimi nilijiamulia kushi huku Kibaha,huko beach ntakuwa naenda siku za sikukuu tu kuogelea...
 
Utabiri wa tetemeko haupo. Hii ni ibada ikioanzishwa na pinga pinga fv ambayo itashuka daraja soon
 
Utabiri wa tetemeko haupo. Hii ni ibada ikioanzishwa na pinga pinga fv ambayo itashuka daraja soon
Sasa ilikua kitu gani ile inatetemesha nyumba na hatujawahi hata kuona tangu tuishi pale. Huwezi kujua kila kitu mkuu acha ubishi
 
Sio earthquake tu Hawa TMA Mambo mengi yakitokea na wao ndo hutoa tahadhari mfano mvua kubwa ikitokea ndo wanaongea, naona hawajui kazi yao vizuri
Nadhani wanajitahidi sana kwa sasa, last time walifanya forecast za mvua msimu mzima na walipatia almost 95%, kumbuka ni FORECAST/PREDICTION. Kingine wao wanatabiri kwa kutumia mitambo, so huenda mitambo ipo outdated.
 
beth,

Hawa TMA ni kama CCM Mataga wanasubiri majanga yatokee ndo wanaleta kiki
Wabongo kwa kupenda kulaumu, wamarekani wenyewe na teknolojia zao zote hawawezi kutabiri kwa hakika sehemu na wakati gani tetemeko linaweza kutokea.
Wasome hama US Geological Survey (USGS):
Can you predict earthquakes?
No. Neither the USGS nor any other scientists have ever predicted a major earthquake. We do not know how, and we do not expect to know how any time in the foreseeable future. USGS scientists can only calculate the probability that a significant earthquake will occur in a specific area within a certain number of years.
An earthquake prediction must define 3 elements: 1) the date and time, 2) the location, and 3) the magnitude.
Yes, some people say they can predict earthquakes, but here are the reasons why their statements are false:
  1. They are not based on scientific evidence, and earthquakes are part of a scientific process. For example, earthquakes have nothing to do with clouds, bodily aches and pains, or slugs.
  2. They do not define all three of the elements required for a prediction.
  3. Their predictions are so general that there will always be an earthquake that fits; such as, (a) There will be a M4 earthquake somewhere in the U.S. in the next 30 days. (b) There will be a M2 earthquake on the west coast of the U.S. today.
Source: Can you predict earthquakes?

Lakini kuna wanyama kama chura aina flani wanaweza kutabiri sikuau masaa kadhaa kabla ya tetemeko kutokea. Mpaka sasa wataalamu hawajajua kwa hakika hao wanyama hutumia mbinu gani kutambua ujio wa tetemeko.
 
Back
Top Bottom