TMA: Mvua iliyonyesha leo imezidi viwango vya ile ya elnino!

Mimi sikui ametumia nn ila mm kwangu hata tegeta niliweka ndoo nje kwa siku mbili imejaa kabisa kwa matone ya mvua tu sasa sijui unatafsirije hiyo
 
Huyo elnino hakuiona huyo....elnino ilinyesha mfululizo karibia siku 10 leo mvua ya siku mbili uifananishie elnino!anatania huyo kumfurahisha aliemchagua au anatafuta kupanda cheo.
Angetuambia alipataje hayo majibu Mm nakaa tgt niliweka ndoo ya lt 20 nje mahali pa wazi na ilijaa kwa matone ya mvua .Nilishangaa ila sikuwa na tafsiri halisi pengine kuna kanuweli
 
Meneja wa operesheni wa TMA Hellen Msemwa amesema mvua iliyonyesha leo imeweka rekodi mpya na kwamba kwa vipimo imeizidi ile ya elmino. Source channel ten habari!
Mvua ya leo ilikuwa kubwa lakini haikuwa na upepo.
Nakumbuka ile ya El nino iikuwa na upepo mkali na Jiji zima miti mingi iiangushwa!
 
Ndo mjue kwanini Magu anakomaa kuhamishia Ikulu Dodoma!!! Anahofu na mvua za kimbunga kama hii ya leo!!! Anapenda kula bata, raha na starehe zingine za kiume!!!! Sasa kwanini a risk maisha Kwa kubaki magogoni!!! Climate change effect!!
Ipo siku mvua na wimbi litapiga na kuifunika Magogoni, utumishi, Ardhi , BOT Na Wizara ya Fedha!!! Hapo ndo tutarudi to Squire 0!!!!
Mzee tuwahishe Dodoma!!!
 
Meneja wa operesheni wa TMA Hellen Msemwa amesema mvua iliyonyesha leo imeweka rekodi mpya na kwamba kwa vipimo imeizidi ile ya elmino. Source channel ten habari!

Kama ni kweli huyo Mtendaji wa TMA ' amefyatuka ' hivyo basi nadhani leo amejiaibisha mno kwani hakuna asiyejua kwamba ile mvua ya ' El nino ' hadi hivi leo bado haijapata ' mbadala ' wake kwani wana Dar es Salaam ' tulitafutana ' kwa takribani karibia wiki mbili. Nitoe tu Wito kwamba ukishajijua Wewe ni Mtendaji / Mtu mkubwa halafu unaenda kuzungumza na Umma kupitia Chombo cha Habari basi hakikisha katika ' Ubongo ' wako kunakuwa na kumbukumbu zote za kutosha kuliko ' Kukurupuka ' na kutuonyesha jinsi ulivyo wa ' hovyo hovyo '.
 
Siku mkiacha kuichagua ccm,huyo ndo mchawi wenu.
Ungejua mkuu hata usingesema. Wakazi wa dom town parcent kubwa sisi ni wahamiaji. Wapendwa wa chama wako huko wilayani na vijijini lakini huko walau wanapata mvua shida ni hapa mjini eeuwhh
 
Huyu ni mtaalamu,ndio Meneja Operation...Hapiki data na wala data zake huwezi kudanganya sababu dunia nzima inatambua.Tuwe na utamaduni wa kusikiliza na kuwapa heshima wataalamu wetu,tusiwachanganye na siasa.

Hiyo mvua ya leo ni kiboko...

Umekaa Arusha, hii mvua ni ya kawaida kabisa. Hakukua na mvua ya maana, miundo mbinu ni mibovu ndio maana maji yamejaa kila kona.
 
Meneja wa operesheni wa TMA Hellen Msemwa amesema mvua iliyonyesha leo imeweka rekodi mpya na kwamba kwa vipimo imeizidi ile ya elmino. Source channel ten habari!
Hakuna watu waongo kama watabiri wa hali ya hewa wa bongo.....siku zote wapo kimya....sasa ngoja mvua inyeshe,,hapo ndy wataibuka kusiko julikana na kutoa matamko,,,NA BADO..HII MVUA NI KUBWA MNO
 
Hakuna watu waongo kama watabiri wa hali ya hewa wa bongo.....siku zote wapo kimya....sasa ngoja mvua inyeshe,,hapo ndy wataibuka kusiko julikana na kutoa matamko,,,NA BADO..HII MVUA NI KUBWA MNO
Hawa watu huwa hawapo serious na kazi zao,

Sasa tutatahadharishwa sana wakati madhara tayari yametokea,

Utabiri unatakiwa kufanyika kabla majanga hayajatokea,

Sasa huku kwetu yakishatokea ndo wanatabiri
 
Umekaa Arusha, hii mvua ni ya kawaida kabisa. Hakukua na mvua ya maana, miundo mbinu ni mibovu ndio maana maji yamejaa kila kona.
Ndio ukiboko wenyewe mkuu,yaani ukiboko wake umeleta madhara tuliyoyaona kwenye mitandao na taarifa za habari za Tv mitandaoni...Kwamba majanga hayo ni sababu ya miundombinu?Basi hili ni suala jingine,dhana yangu ni kuwa madhara yameonekana
 
Back
Top Bottom