GE2025 TLS yacharuka juu ya vitendo vya udhalilishaji wa mawakili (Tukio la Kupigwa kwa Wakili Mahinyila)

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
745
Reaction score
1,470
Wanajamvi kwema?

Nadhani wote tunakumbuka tarehe 15/09/2025, taifa lilishuhudia kadhia ya aibu katika Mahakama Kuu DSM. Wanachama wa CHADEMA walipigwa na kudhalilishwa na jeshi la polisi ila mbali na hayo pia Wakili Deogratius Mahinyila (ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Vijana), akiwa kazini kama Afisa wa Mahakama, alivamiwa na askari polisi, akakabwa, akapigwa vibao, ngumi, mateke na virungu mbele ya umma na kamera za vyombo vya habari. Cha kusikitisha zaidi, baada ya kipigo hicho, Mahinyila aliyetupwa rumande akituhumiwa kwa kosa la kufanya fujo Mahakamani.

View: https://youtu.be/3IONoqSHnMk?si=oNZ9NjwtP5Tb25tG

Tukio hili limeibua hasira na taharuki kubwa miongoni mwa wanasheria. Tanganyika Law Society (TLS) imetafsiri tukio hili si kama shambulio dhidi ya wakili mmoja, bali kama tishio kwa heshima ya taaluma nzima ya uwakili, hadhi ya Mahakama, na msingi wa Utawala wa Sheria nchini.

Kupitia vikao vyake vya dharura, TLS imetangaza hatua kadhaa za haraka ikiwemo​

  1. kusitisha ushiriki wa mawakili katika kesi za msaada wa kisheria (hasa za jinai) pamoja na Samia Legal Aid,​
  2. kuandika barua rasmi kwa Jaji Mkuu na Waziri wa Katiba na Sheria kutaka tamko la wazi,​
  3. kufungua mashauri dhidi ya askari waliohusika,​
  4. kuandaa maandamano ya kitaifa ya amani kwa mawakili wote.​
  5. Pia TLS imetangaza kuwa itakutana na viongozi wa juu wa Mahakama, Polisi na Serikali ili kudai suluhisho la kudumu.​
Lakini hoja kubwa hapa haipo kwa Mahinyila peke yake. Tukio hili linaashiria hatari kwa kila raia. Ikiwa wakili ambae ni Afisa wa Mahakama na anayelindwa kisheria anashambuliwa ndani ya viunga vya Mahakama, mwananchi wa kawaida atawezaje kusimama mbele ya mfumo wa sheria bila hofu ya kudhalilishwa?

Hili ni zaidi ya tukio la udhalilishaji wa mtu binafsi; ni jaribio la kubomoa nguzo za haki na amani. Kukaa kimya ni kuruhusu mabavu yaingie Mahakamani na kuyavua nguvu mamlaka ya sheria. TLS imesimama imara, na ni wajibu wa kila mdau wa haki nchini kushirikiana kuhakikisha kuwa utu na heshima ya kila mwananchi inalindwa.

IMG_6820.jpeg
IMG_6821.jpeg

IMG_6822.jpeg

IMG_6823.jpeg

IMG_6824.jpeg

IMG_6825.jpeg

IMG_6826.jpeg

IMG_6827.jpeg
 
Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) limeamua kuandaa maandamano ya amani nchi nzima, kama ishara ya kulaani na kukemea kitendo alichofanyiwa wakili Deogratius Mahinyila na askari wa Jeshi la Polisi tarehe 15 Septemba 2025, katika viwanja vya Mahakama Kuu, Masijala ndogo ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa Septemba 18, 2025 na kusainiwa na Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi, maandamano hayo yatashirikisha mawakili wote nchini na yataambatana na tamko maalum litakalosomwa na viongozi wa mikoa wa kila ofisi ya TLS.

“TLS kupitia Baraza la Uongozi, ipange na kutangaza siku rasmi ya maandamano ya amani ya mawakili wote nchi nzima kama ishara ya kulaani kitendo alichofanyiwa Wakili Deo Mahinyila pamoja na mawakili wengine waliowahi kupitia udhalilishwaji, manyanyaso au uonevu wakati wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi yetu,” taarifa ya TLS imesema.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa maandamano hayo yatalenga kulinda haki, utu na heshima ya kila wakili, ikiweka wazi kuwa shambulio kwa wakili mmoja ni shambulio kwa taaluma nzima ya sheria na ustawi wa haki nchini.

Aidha, TLS imetangaza hatua nyingine za haraka, ikiwemo kusitisha ushiriki wa mawakili kwenye kesi za msaada wa kisheria za jinai (Criminal Sessions Cases) pamoja na shughuli zinazohusisha Mahakama na Serikali, hadi pale hatua za kisheria zitakapochukuliwa dhidi ya askari wote waliohusika kumshambulia Mahinyila.

“Mawakili wasipokee kesi zozote za msaada wa kisheria kutoka Mahakamani (Criminal Sessions Cases) hadi pale hatua za kisheria zitakapochukuliwa dhidi ya wote waliohusika na shambulio la aibu na tupate taarifa juu ya hatua hizo zilizochukuliwa. Na taarifa ya kutokupokea kesi itolewe mara moja kwa Mahakama na Jamhuri”, imeeleza TLS.

Baraza hilo pia limepanga kufungua mashauri dhidi ya askari waliohusika kumshambulia wakili huyo, huku TLS ikiahidi kumsaidia Mahinyila kufungua mashauri hayo.

Zaidi, TLS imeitaka Serikali, Mahakama na Jeshi la Polisi kutoa tamko na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya waliomshambulia Mahinyila.
 
Ila huyu Mwabukusi siku hizi simuelewi... naanza kuona na yeye ni ms3ng3 tu.. anajitia yupo against na government lakini huyu ni pandikizi , ms3ng3 tu..
 
Maandamano.yahusishe wananchi wote wanaokerwa na matendo ya polisi
 
Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) limeamua kuandaa maandamano ya amani nchi nzima, kama ishara ya kulaani na kukemea kitendo alichofanyiwa wakili Deogratius Mahinyila na askari wa Jeshi la Polisi tarehe 15 Septemba 2025, katika viwanja vya Mahakama Kuu, Masijala ndogo ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa Septemba 18, 2025 na kusainiwa na Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi, maandamano hayo yatashirikisha mawakili wote nchini na yataambatana na tamko maalum litakalosomwa na viongozi wa mikoa wa kila ofisi ya TLS.

“TLS kupitia Baraza la Uongozi, ipange na kutangaza siku rasmi ya maandamano ya amani ya mawakili wote nchi nzima kama ishara ya kulaani kitendo alichofanyiwa Wakili Deo Mahinyila pamoja na mawakili wengine waliowahi kupitia udhalilishwaji, manyanyaso au uonevu wakati wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi yetu,” taarifa ya TLS imesema.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa maandamano hayo yatalenga kulinda haki, utu na heshima ya kila wakili, ikiweka wazi kuwa shambulio kwa wakili mmoja ni shambulio kwa taaluma nzima ya sheria na ustawi wa haki nchini.

Aidha, TLS imetangaza hatua nyingine za haraka, ikiwemo kusitisha ushiriki wa mawakili kwenye kesi za msaada wa kisheria za jinai (Criminal Sessions Cases) pamoja na shughuli zinazohusisha Mahakama na Serikali, hadi pale hatua za kisheria zitakapochukuliwa dhidi ya askari wote waliohusika kumshambulia Mahinyila.

“Mawakili wasipokee kesi zozote za msaada wa kisheria kutoka Mahakamani (Criminal Sessions Cases) hadi pale hatua za kisheria zitakapochukuliwa dhidi ya wote waliohusika na shambulio la aibu na tupate taarifa juu ya hatua hizo zilizochukuliwa. Na taarifa ya kutokupokea kesi itolewe mara moja kwa Mahakama na Jamhuri”, imeeleza TLS.

Baraza hilo pia limepanga kufungua mashauri dhidi ya askari waliohusika kumshambulia wakili huyo, huku TLS ikiahidi kumsaidia Mahinyila kufungua mashauri hayo.

Zaidi, TLS imeitaka Serikali, Mahakama na Jeshi la Polisi kutoa tamko na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya waliomshambulia Mahinyila.
Tunaanza kuzungumza lugha moja
 
Mwabukusi bhana… A lot of tough talking, couple with zero action! Hapo nyuma alituaminisha kwamba kutekwa na kupotezwa kwa Nyagali Mdude kungekuwa kiama cha wasiojulikana. Matokeo yake? You be the judge!
 
Kila anayeweza afanye kitu, Polisi ndio mtu wa mwisho anayepaswa kumuonea raia mwema.

Kwa bahati mbaya kwa Tanzania ni kinyume chake.
 
Wanajamvi kwema?

Nadhani wote tunakumbuka tarehe 15/09/2025, taifa lilishuhudia kadhia ya aibu katika Mahakama Kuu DSM. Wanachama wa CHADEMA walipigwa na kudhalilishwa na jeshi la polisi ila mbali na hayo pia Wakili Deogratius Mahinyila (ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Vijana), akiwa kazini kama Afisa wa Mahakama, alivamiwa na askari polisi, akakabwa, akapigwa vibao, ngumi, mateke na virungu mbele ya umma na kamera za vyombo vya habari. Cha kusikitisha zaidi, baada ya kipigo hicho, Mahinyila aliyetupwa rumande akituhumiwa kwa kosa la kufanya fujo Mahakamani.

View: https://youtu.be/3IONoqSHnMk?si=oNZ9NjwtP5Tb25tG

Tukio hili limeibua hasira na taharuki kubwa miongoni mwa wanasheria. Tanganyika Law Society (TLS) imetafsiri tukio hili si kama shambulio dhidi ya wakili mmoja, bali kama tishio kwa heshima ya taaluma nzima ya uwakili, hadhi ya Mahakama, na msingi wa Utawala wa Sheria nchini.

Kupitia vikao vyake vya dharura, TLS imetangaza hatua kadhaa za haraka ikiwemo​

  1. kusitisha ushiriki wa mawakili katika kesi za msaada wa kisheria (hasa za jinai) pamoja na Samia Legal Aid,​
  2. kuandika barua rasmi kwa Jaji Mkuu na Waziri wa Katiba na Sheria kutaka tamko la wazi,​
  3. kufungua mashauri dhidi ya askari waliohusika,​
  4. kuandaa maandamano ya kitaifa ya amani kwa mawakili wote.​
  5. Pia TLS imetangaza kuwa itakutana na viongozi wa juu wa Mahakama, Polisi na Serikali ili kudai suluhisho la kudumu.​
Lakini hoja kubwa hapa haipo kwa Mahinyila peke yake. Tukio hili linaashiria hatari kwa kila raia. Ikiwa wakili ambae ni Afisa wa Mahakama na anayelindwa kisheria anashambuliwa ndani ya viunga vya Mahakama, mwananchi wa kawaida atawezaje kusimama mbele ya mfumo wa sheria bila hofu ya kudhalilishwa?

Hili ni zaidi ya tukio la udhalilishaji wa mtu binafsi; ni jaribio la kubomoa nguzo za haki na amani. Kukaa kimya ni kuruhusu mabavu yaingie Mahakamani na kuyavua nguvu mamlaka ya sheria. TLS imesimama imara, na ni wajibu wa kila mdau wa haki nchini kushirikiana kuhakikisha kuwa utu na heshima ya kila mwananchi inalindwa.

View attachment 3476002
View attachment 3476003
View attachment 3476004
View attachment 3476006
View attachment 3476007
View attachment 3476008
View attachment 3476009
View attachment 3476010

Mnamwendekeza huyu bibi sultani na utawala wa.kioga oga wa kugawa pesa kuwa chengua mipolisi
 
Haya mambo ya kungoja mpaka mtu wako aguswe ndio upige kelele mara nyingi ndio yanatufikisha sehemu mbaya mpaka pale tutakapoanza kuangalia HAKI kama HAKI na kila mmoja wetu ni Binadamu let alone Mtanzania tutaendelea kugawanywa na watawala katika Itikadi, Imani na Wao na Sisi....

Tutaweza ku-Survive wote kwa Umoja wetu au Ku-Perish mmoja mmoja....
 
Back
Top Bottom