Wakati umefika kwa TLS kujiongeza kwa kujenga ofisi zao za makao makuu Dodioma. Serikali ipo Dodoma, bei ya ardhi Dodoma ni chini, Dodoma ni katikati ya nchi. Hivyo sababu za TLS HQ kuhamia Dodoma zipo. Shida labda utashi wa kufanya maamuzi hayo. Dunia itawashangaa kama wataendelea kubanana Dar wakati wadau wakubwa kama serikali na utawala wa mahakama vinahamia Dodoma. Uongozi mpya wa TLS walao mkitekeleza hili mtakuwa mmeacha legacy ya maana ktk awamu yenu.