barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Serikali inakusudia kupeleka bungeni muswada wa sheria utakaofuta sheria inayoanzisha chama cha wanasheria nchini (TLS) na kutenganisha shughuli za uwakili na chama hicho. Sheria hiyo itaunda chombo kingine mbadala wa TLS kitakachoitwa "Bodi ya Wanataaluma wa sheria", ambayo itaundwa na Waziri mwenye dhamana ya sheria na ndiyo itakayoshughulikia usajili, weledi, na maadili ya mawakili wote nchini.
Kufuatia mabadiliko hayo ya sheria ikiwa TLS itahitaji kusajiliwa upya basi itasajiliwa kama NGO. Msemaji wa wizara ya Sheria ameliambia gazeti la HabariLeo kwamba maandalizi ya muswada huo yapo hatua za mwisho na utapelekwa bungeni ili kupitishwa na kuwa sheria Kamili. Ikiwa muswada huo utapita, TLS itakufa rasmi na mawakili wote watakua wakisajiliwa na Bodi ya wanataaluma wa sheria itakayoundwa na Waziri mwenye dhamana.
Hii itafanya Mawakili wote kusajiliwa na "chombo" ambacho kitakuwa chini ya Waziri na pia kuenguliwa ktk uwakili na chombo hichohicho.
Sasa wale mawakili "wakorofi" na wale ambao "mkuu" alisema wanatetea hata "maovu" wanaweza kuwa ktk hali mbaya sbb "regulator" wa "ubora" wa mawakili atakuwa ni serikali kupitia wizara ya Katiba na Sheria.
Bodi ikiamua kukupoka leseni ya uwakili,basi hakuna wa kuizuia.
Hii ndio hali halisi...Walianza na Wayahudi,tukasema sisi si Wayahudi,wakaja kwa Wanasiasa,tukasema sisi si wanasiasa,wakahamia kwa wanaharakati,tukasema sisi si wanaharakati,wakahamia kwa viongozi wa dini,tukasma sisi si wana dini...Wamefika kwetu,na hakuna wa kututetea...sababu wote waliopaswa kututetea,walishamalizwa.