TLP wazichapa kavukavu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TLP wazichapa kavukavu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Jun 28, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]TLP wazichapa kavukavu
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 27 June 2011 20:58 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Mwenyekiti wa TLP,Augustine Mrema

  Ellen ManyanguVIOJA na vurugu jana vilitawala katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), na kusababisha Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kuingilia kati na kuwakamata baadhi ya wanachama wa TLP.
  Vurugu hizo zilitokea jana kwenye mkutano na waandishi wa habari uliokuwa umeitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Hamad Tao.Taharuki ilianza pale Tao ambaye alikuwa na lengo la kumbomoa Mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrema kujikuta anatoa maelezo ambayo hayafanani na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa kwa waandishi wakati mkutano huo upokuwa ukiendelea.
  Vurugu lilianzia pale mmoja wa waandishi alipohoji Tao kutoa maelezo yanayopingana na taarifa yake ya maandishi ambayo yeye mwenyewe ameisaini na kila mwandishi kugawiwa nakala.Tao alipoponyeshwa taarifa hiyo alitaharuki na kuanza kujaribu kuikanusha, lakini wanachama wengine wa TLP aliokuwa ameandamana nao walianza kupingana naye hali ambayo ilisababisha mkutano kuvurugika na kuondoa maelewano.

  Tatizo hilo lilitokana na Tao kuandamana na wanachama wengine ambao wakati anaanza kutoa maelezo, waligawa karatasi hizo, lakini cha kushangaza ni pale maelezo yalipotofautiana huku taarifa hiyo ikiwa na saini ambayo Tao alishindwa kuikataa kuwa ni yake.
  Hali ilikuwaje?
  Hali yenyewe ilikuwa hivi, Tao aliwasili katika mkutano huo saa 5.00 na moja kwa moja alianza mazungumzo yake na waandishi wa habari kuhusu hali ya kisiasa ndani ya chama hicho.Pamoja na mambo mengine alimtaka kuwa Mrema si mwanachama wa TLP bali ni wa CCM na wala chama hicho hakijawahi kumpa nyumba kama yeye anavyodai.

  Wakati akiendelea kutoa maelezo ya kumbomoa Mrema, kama dakika 20 baadaye kundi la wanachama wengine wa chama hicho ambao awali walikaa katika viti kama waandishi wa habari wakimsikiliza lilianza kugawa taarifa ya maandishi.
  Watu hao walianza kuwagawia waandishi taarifa iliyosainiwa na Tao na wala yeye mwenyewe hakushtuka wala kupinga watu hao kugawa taarifa hiyo ya maandishi.Waandishi walipigwa na butwaa kuona taarifa hiyo inamsifu Mrema wakati Tao anamponda, ikabidi waanze kuangaliana na mmoja wao akaamua kupasua jipu na kumuuliza:“Naibu Katibu, unakanusha juu ya taarifa za Mrema kupewa nyumba na wanachama na unaeleza kuwa Mrema ni kada wa CCM. Mbona katika taarifa uliyotupa inakanusha yote na kuelezea kuwa Mrema alipewa nyumba na wanachama wote waliridhia?” alihoji mmoja wa wanahabari.
  Swali hilo lilimfanya Naibu Katibu huyo ashikwe na butwaa na kushangaa juu ya maelezo hayo ya mwandishi wa habari ambao walimtaka kufafanua juu ya utata huo.Tao alijitetea, “Mimi sijui taarifa hizo na wala sikanushi maneno yangu kwani hata taarifa zangu za maandishi zinajieleza. Hawa wanaogawa taarifa hizi wametumwa na Mrema ili nisiseme ukweli wa mambo mabaya anayoyafanya ndani ya chama kwani amegeuza chama kuwa chake na si cha wananchi.”
  Alipotakiwa kujieleza zaidi juu ya saini iliyopo kwenye taarifa hiyo alikanusha na kusema yeye hajui chochote na kuwa huo ni mchezo mchafu ulifanywa na Mrema ili kujisafisha.“Sahihi hiyo mimi siijui na maelezo yaliyomo humo ndani ya taarifa hiyo siyatambui,” alisema Tao.
  Taarifa hiyo ambayo ilikuwa na sahihi ya Tao ilikuwa ikizungumzia nyumba anayoishi Mrema ambayo inadaiwa alinunuliwa na chama hicho na kwamba ni mali halali ya Mrema.Hali hiyo ilisababisha malumbano makubwa na mkutano huo kuvunjika huku waandishi wakabakia njia panda juu ya kipi ni ukweli hasa ikizingatia kuwa waliogawa taarifa hiyo waliandamana wote na kuingia kwenye chumba cha mkutano.
  Baada ya kuona ubishi inazidi na maelewano hakuna huku munkari unazidi kupanda kila mmoja akitetea upande wake, maofisa wa Idara ya Habari (Maelezo), waliamua kumchukua Tao na wenzake na kwenda kuwaweka katika chumba kimoja.
  Ujio wa FFU
  Muda mfupi baadaye FFU, walifika na kuwachukua wafuasi wanne wa TLP waliokuwa wanapingana, akiwemo Tao.Walichukuliwa na kupakizwa katika gari ya polisi na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
  Waliochukuliwa askari hao ni pamoja na Naibu Katibu, Richard Lyimo, Katibu wa Wanawake Taifa, Nacy Mlikalia na mlinzi Anderson Temu.Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Maelezo, Raphael Hokororo alisema wamelazimika kuwaita FFU kutokana na mzozano makali ambayo waliona mwisho wake ungeweza kuwa ni mapambano, kujeruhi na uharibifu wa mali.
  “Tumelazimika kuita watu wa usalama kutokana na vurugu hizi kwani watu hawa wameingia hapa na kumwambia mlinzi kuwa ni wa moja katika mkutano, lakini kumbe ni kinyume chake. Matokeo yake wamesababisha mtafaruku huu,” alisema Hokororo.
  Alisema wamelazimika kufanya hivyo ili kuweza kulinda mali za waandishi na watu wote wanaokuja katika mkutano kwani ofisi hizo ni za Serikali na kwamba zinapaswa kuheshimiwa.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Mrema ni mwenyekiti wa idara, kamati na halmashauri zote ndani ya chama.
  Kesho mtasikia akiita mwenyekiti wa wanawake wa TLP
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kheee hii picha ni ya nani?aiseee huyu astaafishwe ubunge bana khaaa
   
 4. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mbona kila chama cha upinzani alipopita mrema kumetokea migogoro? Poor management? Acha kutawala mithili ya mganga wa kienyeji mh.mrema,yaani kila kitu wewe tu? Au unatumika kuua upinzani?
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hili ndio tatizo kubwa la Mrema
  Kila cheo na madaraka vyake ndani ya chama
  Huko Vunjo mrema ni mbunge,DED, DC,DPC-district police Commisioner, Askofu wa jimbo,Hakimu wa Wilaya yaani noumer sana
   
 6. p

  police Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu tao ni mamluki wa cdm katumwa nao, juzi mrema kawaponda cdm bungeni naona wanarudisha mashambulizi. huu ni mkono wa cdm.
   
 7. p

  police Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu tao ni mamluki wa cdm katumwa nao, juzi mrema kawaponda cdm bungeni naona wanarudisha mashambulizi. huu ni mkono wa cdm. kuna vyama 18 kwanini tao asiende huko atapata uenyekiti..
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  kigogo sijakuona siku nyingi,sio kawaida yako
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  hapana mkuu.....ni tatizo la wachaga......
   
 10. J Rated

  J Rated JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Itakuwa ulipigwa chini na wachaga,sio siri..
   
 11. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Dikteta Mrema anavyoonyesha rangi zake zote alizonazo,huyu jamaa anatisha vibaya sana!!!
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha poor management,huyu jamaa ni puppet wa CCM,anachokifanya anakijua yeye mwenyewe!!
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu acha ukabila,hauwezi kukusaidia lolote!!
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hahahaha Mrema mroho wa madaraka
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  acha ujinga
  Mbona Mbowe Mwenyekiti aliruhusu Slaa kugombea 2010?
  Mbatia mwenyekiti aliruhusu Rungwe 2010

  mrema ni wa ovyo sana linapokuja swala la madaraka
   
 16. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Hivi kabla ya kuapishwa kuwa Mbunge hawa jamaaa zetu huwa wanapima afya zao kwanza kama kazi zingine?

  [​IMG]
   
 17. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Jamani Mrema kachoka mwacheni atapetape. Ni shushushu aliyeiva na kazi kubwa kwake kuua upinzani for the betterment of the ruling party!
   
Loading...