TLP sasa yataka madiwani wake watemwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TLP sasa yataka madiwani wake watemwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jul 13, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  KAMATI Kuu ya chama cha TLP imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kupangua uteuzi wa madiwani wa viti maalumu na wa mkoani Arusha ambao waliteuliwa kwa nyaraka za kugushi na kutaka wahusika wapelekwe mahakamani.

  Katika barua iliyoandikwa juzi na kusainiwa na mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrema iliyoelekezwa kwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ilisema kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilithibitisha kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliteua viongozi hao ambao hawakuteuliwa. Kikao cha kamati kuu kilithibitisha kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliteua majina ya madiwani na viti maalumu wa TLP ambao hawakuteuliwa na kamati kuu ya chama hicho kama katiba inavyotaka ilieleza barua hiyo. Hata hivyo, kamati hiyo iliitaka tume hiyo kuwafikisha maofisa wa chama hicho waliohusika na tukio hilo ambao ni Hamad Tao na Major Jesse Makundi mahakamani kwa kosa la kutoa taarifa za uongo na nyaraka za kugushi kwa Ofisi ya Serikali.

  Pia ilitaja majina ya madiwani wa viti maalumu walioteuliwa kwa udanganyifu ambao ni Mwahija Chogga Manispaa ya Arusha, Naishie Mollel wa Halmashauri ya Arusha na Fortunata Mpalamba wa Halmshauri ya Chunya.

  Kamati ilieleza kuwa madiwani hao hawajawahi kuteuliwa na kamati hiyo iliyokutana Moshi Septemba 29 mwaka jana na wala ile iliyokutana Julai 9, mwaka huu kama katiba ya chama hicho Ibara 2003/b(4) inavyosema. Aidha barua hiyo pamoja na kuitaka tume ya uchaguzi kutegua nyadhifa za viongozi hao walioteuliwa kwa nyaraka za kugushi pia aliitaka tume hiyo iwateue viongozi walioteuliwa na kamati ambao ni Mwamvua Mahanza kwa Halmashauri ya Arusha, Happy Mollel kwa Halmashauri ya Wilaya na Sharifa Lema kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

  Pamoja na kuelekezwa kwa tume ya uchaguzi pia barua hiyo ilipelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa nchini, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya na kushauri tume itengue uteuzi huo ili iweze kusaidia kumaliza mgogoro. Julai 9, mwaka huu, kamati kuu ya TLP ilimsimamisha aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho Hamad Tao akiwa ni mmoja wa maofisa waliohusika kugushi nyaraka hizo baada ya ofisa mwenzake Jesse Makundi kujiuzulu kutokana na kashifa hiyo.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 4,929
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  usafi uanzie ndani ya chama ndipo ufate kwingine....good move TLP
   
Loading...