TIZAMA: Namna ya kuwapigia kura RAMADHANI BROTHERS ukiwa Tanzania kwenye mashindano ya America Got Talent

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Habarini ndugu zangu naomba tuwapigie ndugu zetu RAMADHANI BROTHERS wanaoiwakilisha TANZANIA 🇹🇿 kwenye mashindano ya America Got Talent. Tufanye hili jambo haraka iwezekanavyo ili waweze kushinda, ikumbukwe vijana hawa wameingia kwenye Fainali ya mashindano haya.

Upigaji kura inafungwa saa 7:00A.M kwa huku itakuwa saa 11 jioni, siku ya leo Jumatano, hivyo tuna masaa machache ya kupiga kura, piga kura kwa haraka na washirikishe watanzania wengine wapige kura

Namna ya kuwapigia kura

1. Pakua app ya TURBO VPN kwenye Playstore au App store

Screenshot_20230927-115725_1.jpg


2. Fungua App Kisha Bonyeza SERVERS LIST na chagua UNITED STATES kisha bonyeza LOS ANGELES na automatically utakuwa umewasha VPN.
Screenshot_20230927-121453_1.jpg


3. Ikisha-connect nenda kwenye account ya instagram ya RAMADHANI BROTHERS bonyeza link kwenye profile yao yenye neno "agt" au unaweza kubonyeza hapa link hii Vote and Save - America’s Got Talent
Screenshot_20230927-121826.jpg

Lakini akikisha ukibonyeza ifunguke kwenye browser moja kwa moja, au ukiifungua kwenye short browser nenda kwenye vidogo vitatu na bonyeza OPEN IN CHROME ua fungua kwenye default browser yoyote inayotumia hili iweze kufungua website vizuri.
Screenshot_20230927-130936.jpg



4. Baada ya hapo nenda kwenye LOGIN kisha jaza taarifa zako kwa kuchagua haina ya njia ya Email kama
Screenshot_20230927-122124.jpg


5. Jaza Jinsia na taarifa nyingine za muhimu watakazokuomba ambazo chache tu... Wakikuuliza ZIP CODE au POSTAL CODE weka 10000. kisha utakuwa umejiandiksha.
Screenshot_20230927-123912.jpg



6. Baada ya kutengeneza profile itakuruhusu kwenda kupiga kura
Screenshot_20230927-123836.jpg


7. Piga kura kwa kuzungusha hilo duara mpaka kwenye 10, hapo utakuwa umepiga kura 10, kisha bonyeza neno SUBMIT VOTES. na umefanikiwa uwapigia Ramadhani Brothers.
Screenshot_20230927-124250.jpg


Hakikisha unapiga kura na pia unawafundisha na marafiki namna ya kupiga kura hili hawa watanzania washinde. Mashindano yanafungwa saa moja asubuhi muda wa Marekani
 

Attachments

  • Screenshot_20230927-124250.jpg
    Screenshot_20230927-124250.jpg
    66.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom