hakuna nchi inayoweza kuendesha kwa nguvu ikawashinda wananchi. polisi ni wachache kuliko wananchi. nawashauri waatumie taaluma kwenye kuzuia fujo, la sivyo wanaweza kuongeza fujo. vilevile, nafikiri tuzuie matamshi ya kuhamasisha fujo au yale yatakayoibua fujo. ninyi viongozi wa nchi ongozeni nchi kwa busara mkijizuia na maneno ya kuudhi na kusababisha chuko mioyoni mwa raia, maneno ya kebehi yanayoonyesha kama nchi hii inaongozwa kwa nguvu na si democrasia.
ninyi raia pia, pimeni wenyewe kipi chenye faida kukifanya kwa sasa. jiulize ukifanya maandamano tarehe moja, ni kwa maslahi gani, kuna faida gani utapata, au kama utavuruga maendeleo ya nchi kwanini usinyaamaze? binafsi ata kama magufuli atakuwa aliongea lugha fulani ya kuudhi, tunatakiwa kumchukulia alivyo, tumsome na tuchukuliane naye, kiiujumla hana nia mbaya kwa chochote anachofanya. tuseme ukweli tu hata uccm ccm ule wa zamani siku hizi umepungua, siku hizi rais anawaza maendeleo, unamwona ana nia ya ndani kabisa, hivyo hata kama atakuwa ameteleza ulimi, jueni kwamba maadamu alikuwa na nia njema moyoni basi tunachukuliana naye kama alivyo. la sivyo tunarudisha maendeleo nyuma na haina faida kwetu. rudini majumbani kweli mkafanye kazi. hao wanasiasa mnaowaamini ni wasaliti na wanawazunguka kila siku lakini hamuelewi tu.