Title deed

Title deed

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
571
Reaction score
156
Habari zenu wana JF?
Naomba utaratibu wa kupata title deed ktk kiwanja changu ambacho hakiko ktk eneo lililopimwa na halmashauri, pia majirani watake nao kupimiwa au wasitake (ili tupunguze gharama kwa kila kiwanja) MIMI sijali nahitaji nipate title deed ya kiwanja changu. Hata kama inachukua mwaka mzima kuanzia kupima hadi kupata hiyo title deed MIMI NAHITAJI NIIPATE KABLA YA JULY, 2013. Nadhani mmenisoma ninaposema "hata kama utaratibu unachukua zaidi ya mwaka, mimi nahitaji ndani ya mwezi mmoja"

Mwenye kujua njia ya kupita ani-PM.
Asante!
 
Kuna thread ilijibiwa may be utafute huku unasubiria wadau wajibu
 
Kupima mwaweza kujiorganise na mkatafuta any registered surveyor/mpima akawapimia maeneo yenu kwa gharama mtakayokubaliana naye,ila kumilikishwa kwa maana ya kupata hati utatakiwa kwenda halmashauri husika idara ya ardhi ambamo kiwanja chako kipo,utapeleka barua ya maombi ya kupimiwa,survey map kutoka kwa surveyor na TP drawing /ramani ya mipangomiji kilipo kiwanja chako,utalipa gharama za kumilikishwa kama uandaaji wa hati,usajili wake,kodi ya ardhi na stamp duty then utaandaliwa hati yako ,utakwenda kuisaini mbele ya hakimu,wakili nk baada ya hapo hati yako itapelekwa kwa kamishna wa ardhi kwa kusainiwa na kusajiliwa na msajili wa hati ili iweze kuoperate kama kuikopea bank ,kuweka dhamana nk
 
Back
Top Bottom