TISS iachane na kufuatilia wanasiasa, ijikite hata kwenye mikataba mbalimbali Rais Samia anayoingia maana tunapigwa mchana kweupe

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,033
Hawa jamaa

Sasa waachane na vile visa mara Zitto katumiwa meseji za kutishwa mara Lissu katishiwa kwa kupigiwa simu, mara mtu akiwa chadema wanamdukua yaani wao kudeal na wapinzani tu hapana waachane na siasa hizi maana sijaona mpinzani anaefanya siasa za kuhatarisha usalama wa nchi kwa kua hatuna mwanasiasa mwenye makundi ya waasi na wenye silaha,

Ukiangalia mikataba ya Rais Samia Uganda na Kenya unajua kabisa tumepigwa mchana kweupe kwa mfano Ruto na Raila wote sera yao kwa sasa ni kuachana na kuagiza mahindi au mazao nje ya nchi na hapa inalengwa Tanzania.

Wao unawapa soko la bidhaa zao na kuwapa vibali vya kufanya kazi huku ukichekacheka come on! DUNIA YA UBEPARI UKICHEKA UMELIWA.

TISS sasa ijikite kwenye kufanya intelijensia za kiuchumi ikiwamo kutafiti juu ya mikataba wanayoingia viongozi, kwa mfano utaona tu visa toka vya Dowans, Symbion, unaona hapa TISS hawakushauri vizuri ndio maana tunapigwa.

Mikataba tu ya January Makamba raia wa kawaida niliepo kijijini unaona hapa tunapigwa mchana kweupe lakini wao wapo tu hadi itokee tena tuvunje mikataba na tulipe mabilioni ya fidia hapana.

Position ilipo Tanzania haitakiwi kua hivi ilivo ni wakati vyombo vya usalama kuzuia matumizi mabovu ya rasilimali za nchi na hata miradi mbali mbali inayofanywa huko kwenye halmashauri waifuatilie.

MIKATABA YA UGANDA NA KENYA NA MIKATABA YA JANUARY NA MIKATABA YA KULE MALIASILI SINA IMANI NAYO TUNAPIGWA MCHANA KWEUPE.
 
Nadhani umeongea ujinga ,kwamba Kenya waache kuoambania watu wao wawe wanawajali nyie sio?


Mahindi sio chakula cha binadamu bali ni chakula cha mifugo,pointi ya msingi iwe kugeuza ufugaji uwe wa kisasa Ili mahindi yapate soko.

Kulaumu wengine kwa sababu zisizo na mashiko ni kukosa akili.

Kwa hiyo Kenya wakiwekeza uzalishaji ukawa mkubwa kwao waagize Tzn Ili iwaje? Hili linahusikaje na biashara ya Tzn na Kenya? Wapi mlikubaliana kwamba Tzn itauza mahindi Kenya afu wao wataleta maziwa?
 
Back
Top Bottom