Timu za mkoani huwa zinakera sana ila basi tu!

oladipo

JF-Expert Member
Mar 8, 2022
1,432
2,291
Sijui kwanini timu za mkoani zinapenda sana kutoka sare!

Yaani neno ushindi kwao ni msamiati ambao haujazoeleka

Hebu angalia mfano mechi ya jana ya yanga dhidi ya geita! Yanga form ilikuwa ipo chini mno yaani geita wangekuwa wana uchu wa ushindi wangeshinda mechi ya jana.

Angalia mfano wa pili wa mechi ya leo ya simba na mashujaa. Simba walikuwa wanaruka ruka uwanjani lakini mwisho wa siku wanapata matokeo kwa mazingira ambayo kama ingekuwa timu inayojua kutumia nafasi basi leo ingeibuka na ushindi

Timu za mkoani haziamini kama simba na yanga zinafungika wakicheza nazo utaona kabisa wanatafuta angalau droo au wafungwe goli chache spirit yao ya upambanaji inakuwa ipo chini mno.

Kwa kifupi wajitafakari kwa kuwa tunaongalia hizi mechi tumelipia ili tuone burudani ila mwisho wa siku tunakereka na mechi zinazochezwa upande mmoja.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Timu Ziongeze Uwekezaji Ili Zilete Ushindani

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaongeza Uwekezaji kwenye mazingira Ovyo ya timu za mikoani zisizojielewa!?

Hakuna mtu atawekeza ktk ujinga kwa style ya uchezaji wa timu za mikoani, kama mtoa Mada alivyoeleza...

Kama zinashindwa kushindana na Simba mbovu, au Yanga inayocheza chini ya kiwango....si timu zisizojielewa hizi???

Ujinga Mwingi sana....
 
Inakera sana ...imagine mtu amefunga safari mpaka chamazi halafu anakutana upuuzi km ule wa timu zisizojielewa km hizi za mikoani.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Inakera sana ...imagine mtu amefunga safari mpaka chamazi halafu anakutana upuuzi km ule wa timu zisizojielewa km hizi za mikoani.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Kati ya mechi ya Geita na ya Mashujaa ipi imekukwaza zaidi?

Kuna wakati nilikuwa naamini Yanga wananunua matokeo kwa timu hizi ndogo ndogo ila baada ya kuchunguza nikajua hata kama hilo lingekuwa linafanyika linachangia nafasi ndogo sana katika kufungwa kwao. Kikubwa ni hicho ulichosema timu nyingi za mikoani hazijitambui na wachezaji wazawa ndiyo kabisa hovyo hovyo. Hii ndiyo ilinipelekea siku moja kuja na uzi wa jinsi ya kuifunga Yanga ya Gamondi. Nilisukumwa na hiki kitu ulichokiona wewe siku hizi mbili.

Hata wangetokea wawekezaji wa kuwekeza katika timu za mikoani, mizizi ya Simba na Yanga bado itazivuruga tu kama ambavyo inaikwamisha Azam.
 
Simba na yanga ni kama dini

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Marefa hawako na usawa kimaamuzi.

Timu zikicheza na Simba/Yanga zinajua sue watoto wa jambo,tuombe Angalau droo tujiondokee.

Ni vigumu Simba/Yanga magoli ambayo refa hana uhakika kama limevuka au la

Ngumu Simba/Yanga kupewa kadi nyekundu. KWA tukio hilo hilo refa kazama mfukoni. Aucho,Kanoute wangekuwa na njano/nyekundu nyingi ikiwa wangecheza vile halafu wangekuwa mikoani

Mechi dakk ya 90. Bila bila,timu ya mkoani ipewe penalty ya ushindi? Labda iwe wazi sanaaaaa
 
Mfano jana mashujaa wanacheza kuna muda inonga alipoteza mpira

Yule jamaa alikua ana uwezo wa kutoa pasi kushoto kwake kulikua kuna support akabutua

Mimi nakataa sio uwekezaji kuna ubovu mwingi sana kwa wachezaji wetu wa ndani
Na hili linatokana na wengi hawakupitia academy watu wanajichezea chezea tu
 
Unafikri wnapenda yawakute ya Ihefu? Yaani uifunge Simba halafu uje ukutane nayo round ya pili si utapigwa 7?
 
Umendika ukweli kabisa. Hizi timu kuzifunga Simba na Yanga ni kama hutokea bahati mbaya
Kuanzia msimu ujao ntaangalia big match tu! Zinazohusu title contenders hawa wasindikizaji sitowapa nafasi! Yaani ligi ina timu 16 ila timu shindani ni tatu tu! Zilizobaki zinagombania kutoshuka daraja.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mfano jana mashujaa wanacheza kuna muda inonga alipoteza mpira

Yule jamaa alikua ana uwezo wa kutoa pasi kushoto kwake kulikua kuna support akabutua

Mimi nakataa sio uwekezaji kuna ubovu mwingi sana kwa wachezaji wetu wa ndani
Na hili linatokana na wengi hawakupitia academy watu wanajichezea chezea tu
Umeongea ukweli... hebu angalia timu kama jkt imechukua cream ya wachezaji wazawa waliotamba ligi kuu ila ona madudu wanayofanya uwanjani yaani wanacheza ilimradi mechi iishe wakafanye mambo yao mengine no discipline at all!!

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Sijui kwanini timu za mkoani zinapenda sana kutoka sare!

Yaani neno ushindi kwao ni msamiati ambao haujazoeleka

Hebu angalia mfano mechi ya jana ya yanga dhidi ya geita! Yanga form ilikuwa ipo chini mno yaani geita wangekuwa wana uchu wa ushindi wangeshinda mechi ya jana.

Angalia mfano wa pili wa mechi ya leo ya simba na mashujaa. Simba walikuwa wanaruka ruka uwanjani lakini mwisho wa siku wanapata matokeo kwa mazingira ambayo kama ingekuwa timu inayojua kutumia nafasi basi leo ingeibuka na ushindi

Timu za mkoani haziamini kama simba na yanga zinafungika wakicheza nazo utaona kabisa wanatafuta angalau droo au wafungwe goli chache spirit yao ya upambanaji inakuwa ipo chini mno.

Kwa kifupi wajitafakari kwa kuwa tunaongalia hizi mechi tumelipia ili tuone burudani ila mwisho wa siku tunakereka na mechi zinazochezwa upande mmoja.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Twiga ni mrefu,mnene na mzito kuliko simba.
Lkn simba anamrarua twiga vipande vipande.
Hiyo ni psychology tu mkuu,hali ya kuamini uwezo na hali ya kuhofia uwezo binafisi.
 
Marefa pia wanachangia kuzikandamiza timu za mkoani.

Goli la Max Nzengeli lingefungwa na Ihefu refa asingelikubali.

Goli halari la Obrey ,Chirwa alilowafunga Yanga, lingefungwa na Yanga Refa angelikubali.

Marefa ama wanahongwa au wanaziogopa timu za Simba na Yanga.
Inawezekana wanawaogopa mashabiki wao au wao pia wanazipenda hizo timu.

Ukiangalia hata maswala ya faulo, timu ya Yanga inafanya faulo nyingi sana lakini zinapiuziwa na Waamuzi. hasa mabeki wake.

Mfano Goli alilofunga KI AZIZ dhidi ya Ihefu Beki wa Ihefu alifanyiwa rafu mbaya hadi akaanguka na Azizi Ki kabla ya kufunga goli.

Penati nyingi wanapewa Simba na Yanga. Sikumbuki ni lini Penati ilitolewa dhidi ya Simba au Yanga.
 
Mimi nadhani suala la marefa kuchangia timu za mikoani kutoshinda mechi lina asilimia ndogo. Ila kama alivyoeleza mtoa mada suala lenye mchango mkubwa kwa timu za mikoani kushindwa kufurukuta mbele ya Simba na Yanga ni kucheza kwa kuamini kuwa hawana uwezo wa kuzifunga Yanga na Simba yaani kutojiamini. Maana unaona timu zinazojiamini zinapata matokeo mfano kwenye ligi ya mwaka 2023/24 Ihefu na Prisons wameonesha kuwa hawa wakubwa wanafungika. Timu nyingine ni Coastal Union, pamoja na kufungwa lakini wanaupiga mpira mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom