Timu ya Wakaguzi kutoka CAF imehitimisha ukaguzi wao salama

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Timu ya Wakaguzi ya utayari wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji AFCON 2027, kutoka Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) imehitimisha ukaguzi wao salama Agosti 2, 2023 Zanzibar kwa kikao cha majumuisho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Ndugu Saidi Yakubu.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Wallace Karia amezishukuru Serikali za nchi hizo kwa ushirikiano waliotoa kufanikisha ukaguzi huo ikiwemo nia ya kuomba kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

“Ukaguzi umemalizika vizuri, kwa kweli wameona tupo ‘serious’ na kuna mambo ambayo wametuelekeza tuyafanye, kwa upande wetu kama Tanzania bara na Zanzibar yapo mengi yamefanyika kwa sababu wakandarasi wapo site na vitu vinaonekana, wameelekeza hili jambo hili tulifanye kwa pamoja na wametoa siku 10 ili kukamilisha nyaraka zote zinazohitajika kulingana na maelekezo yao” amesema Rais Karia.

Aidha, Rais Karia ametoa rai kwa mataifa yote matatu kutekeleza kwa pamoja maelekezo yaliyotolewa ili kufikia lengo la Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo ambayo hayajawahi kufanyika katika ukanda huo na nchi hizo zinatakiwa kukamilisha miundombinu ya michezo itakayotumika kwenye mashindano hayo kabla ya Desemba 2025.

IMG-20230802-WA0106.jpg
 
Naam nadhani wamejifunza na watayafanyia kaz mapungufu walio elekezwa na team hio.
 
Magufuli alituahidi kutujengea uwanja Mwaka 2017.

MBAKA anafariki 2021 alishindwa kumwaga hata CHEPE ya mchanga.

NCHI INAVIONGOZI WA AJABU MNO.
 
Hivi yule mfalme wa Morocco, si aliahidi kujenga uwanja mkubwa wa michezo Dodoma? Au ameishia kujenga msikiti tu?
 
Tungepunguza ubadhilifu serikalini kwa miaka hii iliyopita, leo hii tungeweza kuandaa mashindano haya wenyewe badala ya kuwategemea nchi kama Uganda ambao leo hii wanazunguka huku na huko nje ya Uganda kucheza mechi zao za nyumbani.

Pia kuna uzi niliuliza, inakuwaje Zanzibar amejumuishwa katika mchakato huu wakati wana uwakilishi wao unaojitegemea huko CAF? Nauliza hili swali ili nielimishwe.
 
Back
Top Bottom