Timu ya ushindi UKAWA yavurugana, wadai kuna wasaliti miongoni mwao

Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea uchaguzu mkuu, hali imezidi kuwa mbaya kwa kambi ya UKAWA kutokana na migogoro isiyoisha inayoibuka kila siku. Katika siku mbili hizi kumeibuka shutuma miongoni mwa viongozi wa UKAWA wakiwashutumu wenzao kuwa ni wasaliti. Baadhi ya watu wanaoshutumiwa kuwa ni wasaliti ni Waziri mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye anayedaiwa kutumwa na vyombo vya mfumo kwenda kuimaliza UKAWA kwa kuvujisha siri za ndani kabisa za UKAWA (Hii inathibitika siku alipotangaza kujitoa ndani ya CCMpale aliposema nahama CCM ili kuiimarisha CCM njeya CCM). Pia mtu mwingine anayeshutumiwa kuhujumu UKAWA ni Mzee Matson Chizii ambaye alikuwa ni mtumishi wa CCM kwa muda mrefu sana, ambaye pia ni mtu aliyebobea katika masuala ya usalama ndani ya CCM, na pia amebobea katika mikakati na mbinu za kushinda uchaguzi. Mzee Chizii anahisiwa kutumia mikakati ya UKAWA kwa kutengeneza mikakati mbadala itakayoisaidia CCM kushinda

Somewhere there is a real Julian Assange. Fake Assange, fake message.
 
Back
Top Bottom