VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Nimeambiwa kuwa ile ya kampeni ya CCM iliyoundwa kwa kumsaidia Dr. Magufuli na Mama Samia imesambaratika jana usiku baada ya kikao cha kimkakati. Nimearifiwa na mmoja wa wajumbe wa timu hiyo kuwa kusambaratika kwa timu hiyo kunatokana na sababu mbalimbali. Wapo wajumbe waliosusa baada ya kuona wananchi hawaelewi somo la CCM na kuielewa Ilani. Wananchi wamekuwa hawaelewi wanachoambiwa na sasa wajumbe wanaishiwa cha kusema.
Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa wanatuhumiana, na hata na Dr. Magufuli mwenyewe, kuwa ni popo wa kisiasa. Wanaunga mkono harakati za wapinzani kwa kificho na kumharibia Dr. Magufuli majukwaani kwa kutamka maneno ya kukwaza na kukera yanayochochea hasira za wananchi dhidi ya wagombea wa CCM wa ngazi za Urais, Ubunge na Udiwani.
Wapo wajumbe waliosusa kutokana na kutotimiziwa matakwa yao hasa ya malipo kwa kila siku wanayoifanyia kazi. Wajumbe hao wamesema kuwa hawana muda wa kusubiri kulipwa baadaye kwakuwa uchaguzi ni bahati nasibu na lolote laweza kutokea. Wanasisitiza kulipwa marupurupu yao sasa kwa mujibu wa makubaliano ya kichama na kutoahidiwa kulipwa baada ya uchaguzi.
Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa hawapewi uzito na umaarufu kama ilivyotarajiwa. Wanamlaumu Dr. Magufuli na viongozi waandamizi chamani, kwa mfano, kumuamini sana Abdallah Bulembo ambaye hana hadhi kichama, kisera na kihela kupewa nafasi ya kutawala majukwaa kama afanyavyo sasa. Wanalalama kuwa watu maarufu wamewekwa kando na sasa wanaanza kuota utando.
Sasa timu imesambaratika. Dr. Magufuli yuko njiapanda kikampeni. Itambidi kupambana kiume ili kuendelea kujieleza mbele ya wananchi. Apambane kivyake sasa na watakaobaki naye!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam