Timu ya kampeni ya Bernard Membe hii hapa

Timu ya kampeni ya Bernard Membe hii hapa

Mkuu mbona wale wa jana ulikuwa unawapamba na kuwajenga lakini hawa wa leo ni kama unawatukana na kuwachafua siasa kazi kweli tutaona mengi sana mwaka huu wanaotumiwa watajulikana na hata wanaotumwa nao watajulikana.

CCM yetu hii mkuu, ngoja tuone tutatoboaje?
 
.4. Jack GothamHuyu ndio mkusanyaji wa fedha katika hii kambi, amekuwa kama mwekahazina pamoja na kuhamasisha ukusanyaji wa fedha...Ndio engene ya fedha na hazina ya hii timu ingawa amekuwa na mgogoro kidogo na hiyo timu hasa kwa nyakati hizi ambapo wanasema haeleweki ni kama kaamia kambi nyingine..
Mkuu Ocampo, japo baadhi ya watu kwenye hizi team zako, unawabambikia tuu, mfano jina langu kwenye ile team ya yule jamaa yangu, hivyo hata hapa kutakuwa na majina ya uongo!, ila asante kwa very good analysis japo ume mu under estimate yule kijana aliyepachikwa pale Maelezo!.

Ila huyu jamaa, No. 4, ndiye aliyekuwa the "master mind" wa kampeni ya JK, nakumbuka tukiwa pale UDSM, ndipo JK alipotangazia nia!, kwa kukitumia kikundi cha kina Omar Ilyas na Jaque wa ZZK, jamaa huyu ali facilitate JK akaja kutangazia nia pale Nkurumah, pia najua alizawadiwa nini baada ya kazi ile nzuri!. Sijui na alipo Ilyas ndizo shukrani zenyewe au laa!.

Ili kuijua team "La Mdimu" ni nani na nani, njoo Dodoma siku MFA inawasilisha budget yake, utawaona wote, na ni kweli huwa namuona huyu jamaa, hii inamaanisha mgombea yoyote anayesupportiwa na huyu jamaa ndiye rais wetu wa 2015!.
Hili la kuonekana kama haeleweki, pia linawezekana ili kulinda track record yake, hawezi kuendelea kupoteza nguvu na resources zake kwa mtu asiyeuzika kabisa!, panga pangua, piga ua galagaza, yule "jamaa yangu" ndio mpango mzima!, nadhani huyu jamaa amelitambua hilo and I hope soon atafanya uamuzi wa busara!.

Thanks.
Pasco
 
mwee mbona mwaka huu mtamu sana...inabidi nitafute ipad kabisa maana ngoma badi mbichi kabisaaa...
 
Nimemchek Membe hotuba yake kama kapanic vile....amekurupuka so far Mwigulu ana credit tukiacha ushabik
 
Nimemchek Membe hotuba yake kama kapanic vile....amekurupuka so far Mwigulu ana credit tukiacha ushabik
ya mwigilu ilikuwa nzuri,ila alikuwa akakosea Sana baadaa ya kui critisize serikali amabyo yeye yumo na ni waziri .
pale alikuwa anaibomoa ccm bila kujua au alifanya vile maksudu,
na kwa kutamka weakness ya serikali anayo serve as deputy minister for finance,which mean maovu yote yanayofanywa na ccm na serikali yake anayajua lakin hata siku moja hajajitokeza kukemea.
so he is dirty Kama wakina lowasa na wenzake.makongoro is still the man to beat so far
 
Nimemchek Membe hotuba yake kama kapanic vile....amekurupuka so far Mwigulu ana credit tukiacha ushabik

Sio ka panic Membe hafai na ni pumba tupu kichwani mule hakuna kitu pale
 
hiyo team ya kichovu kama ingekuwa ya mpira basi naifananisha na lipuli au villa squad
 
Kumbe membe ni msanii mzuri wa ngoma za kienyeji...
 
Duhhhh mwaka huu jamani hatari tupu ngoja nimsikilize mtoto wa makamba sijui anamwaga sera zipi mwehh!!
 
Mtalia sana,Dr.Slaa ni kiboko ya wote.Subirini October
 
Binafsi naona membe Amekuwa na hotuba inayojieleza na jinsi atakavyoendeleza mipango ya sasa!wengine zimekuwa hotuba ni Kama ndo wanakuwa marais kwa Mara ya kwanza!kumbuka lazima kuna plan zilizopo ambazo utazikuta hakuna serikali waweza kuwa kila kitu kitakuwa kipya!kazungumzia namna atakavyo kabiliana na rushwa!
 
Jana baada ya kuleta analysis ya timu kubwa, ya ushindi na kali katika mbio za urais 2015 ndani ya CCM, leo naomba nilete mgombea mwingine tena, for more comparative analysis.

Huyu comrade kama tunavyojua ni shushushu wa muda mrefu, ingawa ushushushu wake amekaa nao nje ya nchi kwa muda wa miaka mingi sana, hivyo katika siasa za Tanzania unaweza kusema bila kusita kuwa ni mgeni sana sana.. Huyu bwana hakuwa na ndoto hata siku moja ya kuwa rais wa JMT ingawa anajiona anafaa kwa sababu kuu mbili.....

a). Kubebwa na familia ya ikulu hasa First lady
b). Baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje amechukua things for granted; kwa maana ya kwamba kwa kuwa JK alikuwa waziri wa mambo ya nje basi na mimi lazima nitakuwa rais kwa sababu ni waziri wa mambo ya nje (Akisahau kwamba sio kila siku ni jumapili).

Baada ya hiyo bashraf ndogo ya huyo jamaa sasa naomba nilete timu ya huyu jamaa........

1. First Lady (Mama Salma)

Huyu ndio kampeni meneja wa hii kambi... kazi yake kubwa ni mbili katika hii kambi, mosi ni kumshawishi mkulu ambaye ni rais na at the same time ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kuweza kumbeba bwana Membe na jina lake lirudi katika tatu bora ingawa historia uonyesha kuwa hakuna mtu hata moja aliyebebwa na rais aliyoko madarakani na akapata kushinda (Rejea chaguzi kipindi cha Mwinyi na Mkapa).

Kazi kubwa ya pili ya mheshimiwa First Lady ni kukusanya fedha kupitia WAMA, na kwa hakika mpaka sasa wamefanikiwa sana katika hili, kuna ela nyingi sana zimekusanywa kupitia hiyo organizasheni yenye kazi kubwa ya kusaidia wanawake katika maendeleo..... Taarifa zilizopo ni kuwa alipokuja Buffet feki wa Nyalandu aliweza kumwaga fedha nyingi sana kwa ajili ya kampeni ya bwana Membe kupitia account ya organization hiyo iliyopo benki ya FNB tawi la ohio opposite na Movenpick.......

2. Ridhiwani

Huyu bila shaka wengi vijana tunamfahamu sio kwa hekima na uzuri ila tumeweza kumfahamu kama mtoto wa rais aliyeiba fedha nyingi sana katika nchi hii, huyu ndiye mmiliki wa Lakeoil, huyu ndiye mmiliki wa rhino cement, huyu ndiye mtoto wa rais aliyepata kashfa ya kuuza vitu kama unga, sembe (Ingawa amekanusha hilo katika sehemu mbali mbali).

Huyu kijana amekuwa ndiye rais wa pili wa maamuzi katika nchi hii mpaka saizi kafikia hatua na yeye kujiona kama atuletee rais wa 2015, wakati ndani ya siasa hana hata miaka kumi. Huyu kijana wachambuzi wanasema ni mpiganaji wa vita asiyejua uwanja wa vita uko wapi; uwanja wake wa vita na mapambano ni facebook, kwa maana nyingine facebook ndio mwanza yake, ndio arusha yake, ndio lindi yake ya kutafutia kura.. kwa kweli anasifika sana kwa siasa za facebook....umuhimu wake katika kambi ni kumshawishi mzee na kumwambia kuwa Membe ni mtu mwema sana na akipata mwingine anaweza kuniumiza kwa hizi fedha nilizokuapua baba...

Ameweza kusaidia kujipanga hasa kwa kuwateuwa wakuu wa wilaya kiaina kwa dhumuni la kujiimarisha kama wakina mzindakaya, ulega, Mtaka (aliyewai kupatwa na kashfa ya kufumaniwa na mtangazaji moja wa Itv wa morogoro hope munamfahamu) na wakuu wa wilaya wengine..

3. Lazaro Nyalandu

Huyu mtu amekuwa akijinadi kuwa ni afisa usalama ila trust me hakuna hata jina lake hapa maeneo ya makumbusho, na hata hajawai kuitwa interview hapa makumbusho katika historia ya nchi hii......Ni mtanzania mwenye uzalendo nusu nusu kwa sababu ana uraia wa nchi mbili ya Tanzania na Marekani hivyo ni mtu ambaye hawezi fanya kitu cha kunufaisha tanzania kwa asilimia100% never on earth...Umuhimu wake ni kuwa amekuwa bigwa wa kukusanya fedha za kampeni hasa kwa marafiki zake wa marekani ambao anawaleta kwa mgongo wa kutembelea maliasili, mpaka sasa ameweza kuleta fedha nyingi sana katika hii kambi na mara ya mwisho alipomleta Buffet feki aliweza kuleta fedha nyingi sana sana.... Huyu bwana ameusishwa na biashara haramu ya uuzaji wa unga katika sehemu mbali mbali ingawa amekuwa hakikanusha ila kukanusha tu haitoshi ni sawa sawa na mimi ukinuiliza nishazini na mke wa mtu definitely nitasema NO.... Vikao vya mgombea hufanyika katika nyumba ya huyu jamaa.

4. Jack Gotham
Huyu ndio mkusanyaji wa fedha katika hii kambi, amekuwa kama mwekahazina pamoja na kuhamasisha ukusanyaji wa fedha...Ndio engene ya fedha na hazina ya hii timu ingawa amekuwa na mgogoro kidogo na hiyo timu hasa kwa nyakati hizi ambapo wanasema haeleweki ni kama kaamia kambi nyingine..

5. Pau Makonda

Huyu kazi yake kubwa ni kuingia front katika kutoa matamko ambayo uandaliwa na kambi hiyo, na amekuwa akifanya hayo bila uwoga, wasifu wake mkubwa ni kijana wa kutoa tamko bila ya kuchanganya na akili zake mwenyewe; wakati Mheshimiwa rais aliwai kusema akili za kuambiwa changanya na za kwako. Amekuwa ni kijana wa kuganga njaa nyakati zote tokea alipokuwa Chuo cha Ushirika.

Utiifu wake katika hii kambi ni kwa reasons mbili, mosi aliweza kusaidiwa na Riz kuepuka disco katika chuo hicho tajwa hapo juu, hii ni baada ya kushindwa kuclear supplementary 4 alizopata kwa semister moja which is technical disco, pili amekuwa akifadhiliwa na sita kwa kipindi kirefu (Sita kwa sasa amesurrender urais baada ya kuona maji marefu) na ukikumbuka alikuwa moja wa waazilishi wa chama cha CCJ...

6. Kurugenzi ya Maelezo

Hii idara ndio kiungo muhimu wa kambi hii na wananchi, ingawa wamejaribu kwa muda mrefu bila ya mafanikio, idara hii ikiongozwa na Asser Mwabene almaarufu humu ndani kama mbopo ndio machampion wa hii kambi, la kusikitisha hawana hela, hawana watu, hawana influence na zaidi hawana convincing power kabisa kwa kifupi ni idara mfu katika kambi hii. Umuhimu wake ni kusaidia kuweka picha za Membe katika blog kama michuzi ambayo haina impact yoyote ile katika kuongeza kura au wajumbe.

7. Kundi la wasanii

Kati ya kundi linalochekesha ni hili la Membe, kundi hili wanahangaika na wasanii kila kukicha mara mwanza, mara dodoma, mara arusha wakati kati ya hao wasanii hakuna hata mjumbe moja wa mkutano mkuu wa ccm hii tunaita poor strategic planning.....

Kundi hili hata siku moja sio reliable kabisa katika jambo kitaalamu hawa tunawaita traditional semi intellectual (rejea maandiko ya Antonio Gramci-Hegemony) ni kundi linaloangalia hasa maslahi katika kipindi hicho hicho, ni kundi wasioitaji future while they prefer present.....Sisemi kuwa ni kundi la kubeza ila ni muhimu wakijua hapa wanapoteza muda na wakati....

NB: Pamoja na hayo yote kambi hili linaona kuingia ikulu ni sawa na ngamia kupenya katika tundu la sindano ingawa kuna mazingira ambayo ngamia anaweza kupenya kwenye tundu la sindano, (hasa katika maonyesho ya mazingaombwe).....

Inasemekana majeshi yanahamishiwa kwa Kayanza Pinda ili baadaye Membe apewe nafasi ya Upm......... Hili kundi kwa ujumla lina tatizo moja kuwa wote wanaopendekezwa hawauziki hata kwa dawa mbele ya wanachi .....walianza na Migiro wakaona kumuuza itakuwa ni sawa na kubeba pipa la misumari hasa chadema wakimrudisha Dr. Slaa, Wakaja na Membe pia wakagundua huyu ndio bora hata Migiro na sasa wamehamia kwa Pm ambaye katika sababu ya kugombea kwake juzi alisema sababu kubwa ni kuwa kashauriwa na mke wake (Chukua muda kidogo na ufikiri hapo nilipo bold).


Asante sana......see you again Jumatatu
Vijana wa Lowasa wote mko kama wavuta bangi kabisa.
 
Ndugu yetu Bernard Membe ameanza safari ya matumaini

Source:Mzee Mchopa -M/kiti wa CCM mkoa Lindi 7/06/2015
 
Back
Top Bottom