Hao wapinzani wana nini zaidi ya kuwa na ilani mbovu inayobebwa na mgombea mgonjwa? Asanteni Watanzania kwa kuamua kumchagua Magufuli
Mkuu umezisoma ilani za vyama vyote? Au ni mahaba ya kisiasa tu yanakuendesha? Hebu tupe tofauti ya ilani za vyama hivi (CCM V/s Chadema/ Ukawa) ndipo tujue kama ni ilani mbovu ama la! Vinginevyo tutajua umeongea tu na hujui chochote kuhusu ilani za uchagzi za vyama hivi. Au unashabikia chama aidha kwa sababu ya maslahi ya siku moja (njaa ya siku moja) au unashabikia tu bila kuelewa chochote then unabaki kusota na kulalamika kwa miaka mitano.