Time travel na ufunuo wa ufufuko

Mimi tangu mwanzo nilikwambia kabisa kwamba Mola ana umbile na umbile lake halifanani na kiumbe chochote,
Kwa hayo uliyosema kama nilivyo ya -highlight hapo, unakusudia kusema nini? "...Mola ana umbile na umbile lake halifanani na kiumbe chochote...". Hii maana yake nini? Kwa vipi ni tofauti na: 'hakuna anaejua umbile la Mola'?
 
Mwanadamu daima yupo katika hasara isipokuwa wale kuhusiana kuhusu subira na kufanya mema. Mola aliyajua yote haya na uhuru ulikuwa kwa Adamu na akili na tahadhari alipewa kama ilivyo kwetu,kwahiyo kukosea ni katika maumbile ndio maana kuna moto na kuna pepo,na mbora kati mwanadamu ni yule mwenye kukosea kisha akatubia.
Ni kama unashindwa kuelewa ."Utakatifu na Asili ya Mungu kwa Adamu, Adamu aliiharibu". Hivi ndivyo nilivyokujibu.
Ungetafakari jibu hilo. Au kama hukuelewa ungeuliza.
Lakini umeacha hilo umerukia dhambi binafsi.
 
Misingi ya uandishi wa Historia katika upande wenu na upande wa secular una madhaifu sana na hili nimeliona mpaka kwako na umejaribu kutenganisha Historia na vitabu vya dini,jambo ambalo ni kosa kubwa.
Upande wangu na upande wako, huo ni udhaifu tayari - ni kosa.
Kama wewe una upande, na mimi nina upande maana yake tumegawanyika.
Sasa tumegawanyika kutoka kwenye nini na nani amegawanyika na nani hajagawanyika, ni suala la ukweli wenyewe wa dini.
Na dini inakusudia nini? Mungu? Binadamu - maisha ya ndoa na uchumi?
Tuache hayo. Tuje kwenye swala la msingi: Historia ya nini?
 
Kwa hayo uliyosema kama nilivyo ya -highlight hapo, unakusudia kusema nini? "...Mola ana umbile na umbile lake halifanani na kiumbe chochote...". Hii maana yake nini? Kwa vipi ni tofauti na: 'hakuna anaejua umbile la Mola'?

Kutokana na kuwa hakuna anae weza kumuelezea Mola mlezi,yeye mwenyewe akaamua kujielezea alivyo kwa sifa zake na umbile lake,katika hilo alimtumia mtume wake.

Umbile la Mola wetu mtukufu hakifanani na la kiumbe chochote,na yeye kama alivyojipambanua ya kuwa hafanani na kiumbe chochote wala hana mfano.
 
Sasa ndio utuambie wewe umejuaje kama mtu wa kwanza sio Adamu ? Na utuambie chimbuko la mtu huyo ni nini ?

Huku mwisho naona umesema "Ukweli hata hivyo ,unabaki kuwa mtu aliumba". Hivi ndivyo ulikusudia kuandika au ulimaanisha "kuumbwa" ? Maana nina maswali pia kutokana na kauki yako hii.
Biblia si kwa ajili ya kutufahamisha mwanadamu au mtu wa kwanza alikuwa nani au aliitwa nani. Siyo kazi ya masimulizi ya biblia au, hata Quran kutupa habari za mtu wa kwanza aliitwa nani au alikuwa nani au aliishi wapi.
Nimeshaeleza hili. Lakini kwa ufahamu zaidi, waandishi wa biblia au quran wametumia fasihi.
 
Kutokana na kuwa hakuna anae weza kumuelezea Mola mlezi,yeye mwenyewe akaamua kujielezea alivyo kwa sifa zake na umbile lake,katika hilo alimtumia mtume wake.

Umbile la Mola wetu mtukufu hakifanani na la kiumbe chochote,na yeye kama alivyojipambanua ya kuwa hafanani na kiumbe chochote wala hana mfano.
Unajidanganya tu, hayo uliyosema hayana uthibitisho zaidi ya hicho kitabu chenyewe...
 
Ni kama unashindwa kuelewa ."Utakatifu na Asili ya Mungu kwa Adamu, Adamu aliiharibu". Hivi ndivyo nilivyokujibu.
Ungetafakari jibu hilo. Au kama hukuelewa ungeuliza.
Lakini umeacha hilo umerukia dhambi binafsi.
Kaka kwani kuharibu si ndio dhambi hilo kosa ambalo wewe unadai tumeridhi sio dhambi ?

Bila shaka wewe ndio hukunielewa mimi,sababu kosa ndio hiyo hiyo dhambi. Kwani kosa lile la Adamu si kosa binafsi vipi liwe mpaka kwetu ?
 
Bila shaka wewe ndio hukunielewa mimi,sababu kosa ndio hiyo hiyo dhambi. Kwani kosa lile la Adamu si kosa binafsi vipi liwe mpaka kwetu ?
Kama ingekuwa dhambi binafsi ya Adamu kwanini tuhusishwe nayo, hata sisi - uzao wake?
Hapo ndipo hatuelewani ndugu yangu.
Dhambi binafsi ni tofauti na 'kuharibu utakatifu na asili ya Mungu', yaani dhambi ya asili. Hili ndilo kosa alilolitenda Adamu na siyo dhambi binafsi.
Ndiyo sababu nikasema, kama hujaelewa uliza.
 
Biblia si kwa ajili ya kutufahamisha mwanadamu au mtu wa kwanza alikuwa nani au aliitwa nani. Siyo kazi ya masimulizi ya biblia au, hata Quran kutupa habari za mtu wa kwanza aliitwa nani au alikuwa nani au aliishi wapi.
Nimeshaeleza hili. Lakini kwa ufahamu zaidi, waandishi wa biblia au quran wametumia fasihi.

Sasa kaka naona unakimbia kivuli chako na hakuna kitabu cha Mola kutoka mbinguni kinaitwa Biblia,bali vitabu ni Injili,Zaburi,Torati na Qur'aan na kuna kurasa za Ibrahiim na Musa.

Ukisoma Historia ya uandishi wa Injili ya Mathayo au Yohana (Sikumbuki vizuri utanisahihisha) yeye aliandika matukio na miujiza ya Yesu na alifanya hivi baada ya miaka kadhaa ya Yesu kufa,mule kuna historia na vitabu vya muongozo vinakuwa vinasimulia matukio ya watu waliopita kwa lengo la sisi kujifunza ndio maana vinaitwa vitabu vya muongozo kuwaongoza watu.

Kaka nakusihi kitu kimoja,usiizungunzie Qur'aan sababu huijui,katika Qur'aan mule hakuna hata herufi moja ya mwanadamu yaani ule ni ufunuo moja kwa moja toka kwa Mola wetu mlezi. Mule hakuna fasihi ya Mwanadamu ndio maana hata wale mabingwa wa lugha ya kiarabu wa zama za mtume waliishangaa sana Qur'aan.

Kwa maneno yako hayo yanazidi kuitia dosari Biblia kuonekana ya kuwa katika Biblia kuna ufundi wa mwanadamu ndio maana ina makosa mengi.

Vitabu vya dini vimekusanya habari za kale na kuumbwa kwa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ili sisi waja tupate kujua wapi tumetokea,na hili jambo la dharura kulijua.
 
Historia ya nini?

Historia ya matukio ya kabla ya umma husika,mathalani katika Qur'aan kumeelezewa habari za Ibrahim na watoto wake,habari za nabii Luti,habari za Sodoma na Gomora iki watu wajue ubaya wa vitendo kuingiliana nyuma na matukio mengine mengi.
 
Upande wangu na upande wako, huo ni udhaifu tayari - ni kosa.
Kosa kwa nani ? Suala la kutofautiana ni suala la kimaumbile haliepukiki,sababu kuna watu tayari wameshajichagulia njia zao na kuacha njia sahihi. Ila kosa linaingia pindi mtu atakapo acha haki akafata uovu.Haya
Kama ingekuwa dhambi binafsi ya Adamu kwanini tuhusishwe nayo, hata sisi - uzao wake?
Hapo ndipo hatuelewani ndugu yangu.
Haya ni kwa mujibu wa mafundisho yenu,na nilikunukulia aya huko nyuma ya kuwa katika Uislamu hakuna mmoja kubeba mzigo wa mwenzake.

Hili swali unatakiwa ukijibu wewe unae amini katika hilo na hili nilikuuliza huko nyuma.
Dhambi binafsi ni tofauti na 'kuharibu utakatifu na asili ya Mungu', yaani dhambi ya asili. Hili ndilo kosa alilolitenda Adamu na siyo dhambi binafsi.
Ndiyo sababu nikasema, kama hujaelewa uliza.
Hilo kosa ni dhambi sababu alishaambiwa juu ya kutokuukaribia ule mtu,na ndio maana alipoomba msamaha akasamehewa na hili lipo mpaka kwetu kwamba ukifanya dhambi ambayo ndio kosa lenyewe ukitubia unasemehewa.

Mimi nakuelewa vyema na tofauti yetu ni ya kiitikadi ila kila mtu anatajiwa kuijengea hoja itikadi yake na kuonyesha ukweli wa itikadi yake.
 
Kaka nakusihi kitu kimoja,usiizungunzie Qur'aan sababu huijui,katika Qur'aan mule hakuna hata herufi moja ya mwanadamu yaani ule ni ufunuo moja kwa moja toka kwa Mola wetu mlezi. Mule hakuna fasihi ya Mwanadamu ndio maana hata wale mabingwa wa lugha ya kiarabu wa zama za mtume waliishangaa sana Qur'aan.

Kwa maneno yako hayo yanazidi kuitia dosari Biblia kuonekana ya kuwa katika Biblia kuna ufundi wa mwanadamu ndio maana ina makosa mengi.

Vitabu vya dini vimekusanya habari za kale na kuumbwa kwa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ili sisi waja tupate kujua wapi tumetokea,na hili
Ndugu yangu, siandiki kwa lengo la kukuondoa kwenye msingi wako.
Hakuna jambo linalopotosha kama hili la kusema, kwamba, Qur'aan haijaandikwa na wanadamu. Mawazo hayo ni kujidanganya.

Kuhusu Biblia hiki ni kitabu kimoja kilicho na ndani yake mkusanyiko wa vitabu mbalimbali na siyo pekee hivyo ulivyovitaja.
Kuhusu Qur'aan hatuoni ikitofautiana na baadhi ya vitabu vya Agano la Kale na pia vya Agano Jipya.
 
Kama wewe una upande, na mimi nina upande maana yake tumegawanyika.
Kugawanyika ni jambo la kimaumbile na haliepukiki,na kugawanyika kuna letwa na sababu nyingi.
Sasa tumegawanyika kutoka kwenye nini na nani amegawanyika na nani hajagawanyika, ni suala la ukweli wenyewe wa dini.

Migawanyiko ya kiimani mara nyingi husababishwa na ujinga wa watu na kufata matamanio yao ya nafsi.
Na dini inakusudia nini? Mungu? Binadamu - maisha ya ndoa na uchumi?
Tuache hayo. Tuje kwenye swala la msingi: Historia ya nini?
Dini imejumuisha yote hayo na dini imekuja kwa ajili ya kulinda mambo matano,nayo ni :

1. Kuhifadhi dini
2. Kumuonyesha mja lengo la yeye kuishi ni lipi
3. Kuhifadhi akili ya mwanadamu,kwa kumuonyesha vitu gani uharibu akili yake.
4. Kukinda kizazi,hapa kumuonyesha mja ubaya wa kuzaa nje ya ndoa na mfano wake.
5. Kuhifadhi Mali,hapa kumfunza mwanadamu namna ya kutumia mali vizuri.

Suala la Historia nimeshakulezea huko nyuma.
 
Jamaa kaikopi kama ilivyo na anapiga pesa huko YouTube
Screenshot_20190910-114837.jpeg
 
Ndugu yangu, siandiki kwa lengo la kukuondoa kwenye msingi wako.
Hilo nalijua na huna uwezo wa kunitoa katika msingi,ila nakusahihisha ili usiendelee kukosea na kushughulika na jambo usilolijua,kwani litakuumiza zaidi.
Hakuna jambo linalopotosha kama hili la kusema, kwamba, Qur'aan haijaandikwa na wanadamu. Mawazo hayo ni kujidanganya.

Hapa bila kuonyesha ushahidi wapi tunajidanganya wewe ndio utakuwa muongo.

Kila kitu kipowazi,mtume amefariki Qur'aan imeshakamilika walichokifanya maswahaba ni kuikusanya na kuiweka katika mfumo wa kitabu,na kunakili na kutoa nakala kadja wa kadha. Lakini mule hakuna hata herufi moja ya mwanadamu.

Nakuuliza swali la msingi,unaweza kunionyesha wapi tunajidanganya ?
 
Back
Top Bottom