Time line ya ugonjwa wa maburg

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
TIME LINE YA UGONJWA WA MARBURG DUNIANI​
MwakaNchiUgonjwa ulipotokeaRipoti ya idadi ya wagonjwaIdadi ya vifo(%)Kilichotokea
2023
Tanzania​
Mkoa wa Kagera​
8​
5(63%)​
March 21, 2023, Maofisa wa serikali ya Tanzania watangaza mlipuko kwa mara ya kwanza nchini wa ugonjwa wa Marburg.Tukio hili limetangazwa sehemu ya Kagera ambapo ni kaskazini magharibi mwa nchi.Habari za kupatikana au kusambaa kwa ugonjwa bado hazijatolewa.​
2023
Equatorial Guinea​
Jimbo la Kie-Ntem​
9​
7(78%)​
February 13, 2023,maofisa wa serikali ya Equatorial Guinea watangaza mlipuko wa Maburg.Wizara ya afya mwanzoni ilithibitisha kesi moja na kesi nyingine ikaongezeka kutoka jimbo la Kie-Ntem kaskazini mashariki mwa nchi hiyo hadi sasa hakuna taarifa zaidi​
2022
Ghana​
Mkoa wa Ashanti​
3​
2(67%)​
Tuko la kutisha la Maburg lilitokea mkoa wa Ashanti July 2022.Lakini mwanzoni ugonjwa huu ulionekana kwenye maabara ya taifa na ukathibitishwa zaidi kwenye taasisi ya Pasteur mjini Dakar Senegal na kufanya ugonjwa huu kuonekana Ghana kwa mara ya kwanza.Muda mfupi tu baadae watu wawili wa familia moja walionekana na ugonjwa huo hakukuwa na tukio lingine tena lilitokea nje ya familia hiyo.Ugonjwa huo ulitangazwa kutoweka September mwezi huo huo.​
2021
Guinea​
Guéckédou​
1​
1(50%)​
Kesi moja iliripotiwa na kuthibitishwa na wizara ya afya ya Guinea kwa mgonjwa ambayo aligundulika nao baada ya kufariki.Hakuna kesi nyingine iliyothibitishwa baada ya cases 170 zilizoonekana zilikuwa karibu na ugonjwa kufuatiliwa kwa siku 21​
2017
Uganda​
Kween​
4​
3(75%)​
Sampuli ya damu kutoka wilaya ya Kween mashariki mwa Uganda iliionyesha positive virusi vya Marburg.Ndani ya masaa 24 ya uthibitisho mpasuko wa ugonjwa wa haraka ukatokea.​
2014
Uganda​
Kampala​
1*​
1​
Kwa ujumla wake,case moja ilithibitishwa(mbaya) na watu waliokaribu na ugonjwa 197 walifuatiliwa kwa wiki 3.Kati ya hawa 197, 8 walionyesha dalili zinazofanana na Marburg, lakini wote walionekana negative​
2012
Uganda​
Kabale​
15​
4(27%)​
Majaribio katika CDC/UVRI yalionyesha mpasuko wa ugonjwa katika wilaya za Kabale, Ibanda, Mbarara, na Kampala katika kipindi cha zaidi ya wiki 3​
2008
Raia wa Uhonzi aliyekuwa Uganda​
Pango la msitu wa Maramagambo huko Uganda, kwenye ukingo wa mbuga za wanyama za malkia Elizabeth​
1​
1 (100%)​
Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 wa kidachi ambaye alikuwa na historia za kusafiri Uganda alilazwa hospitali huko kwao Uholanzi.Siku 3 baada ya kulazwa akasikia dalili za homa na kutetemeaka,ikifuatiwa na kudhoofika kiafya.Mwanamke huyo alifariki siku 10 baada ya kulazwa.​
2008
Raia wa Marekani aliyekuwa Uganda​
Pango la msitu wa Maramagambo huko Uganda, kwenye ukingo wa mbuga za wanyama za malkia Elizabeth​
1​
0 (0)​
Msafiri wa Marekani alirudi kwao akitokea Uganda January 2008. Mgonjwa alionyesha ugonjwa kwa siku 4 baada ya kurudi,alilazwa,na kuruhusiwa kuhakika alionekana kuwa na ugonjwa wa Marburg.​
2007
Uganda​
Mgodi wa madini ya risasi na dhahabu katika wilaya ya Kamwenge​
4​
1 (25%)​
Mpasuko mdogo wa ugonjwa ulitokea kwa matukio ma 4 ya vijana wa kiume waliokuwa wanafanya kazi mgodini,hadi leo hakuna tukio lingine limetokea​
2004 hadi 2005
Angola​
Jimbo la Uige, Angola​
252​
227 (90%)​
Mpasuko ulitokea jimbo la UIGE October 2004.Matukio mengine yaligunduliwa yakiunganishwa na ugonjwa huo moja kwa moja​
1998 hadi 2000
Democratic Republic of Congo (DRC)​
Durba, DRC​
154​
128 (83%)​
Matukio mengi yalionekana kwa vijana wakiume katika mgodi wa dhahabu wa Durba,kaskazini mashariki mwa nchi hiyo,ambapo ndio palionekana ugonjwa huo umeshamiri.Matukio mengine yaliionekana kijiji jirani cha Watsa​
1990
Urusi​
Urusi​
1​
1 (100%)​
Maambukizi yalitokea maabara yakaua mfanyakazi mmoja​
1987
Kenya​
Kenya​
1​
1 (100%)​
Kijana wa Denmark mwenye umri wa miaka15 alilazwa akiwa na historia ya siku tatu ya kuumwa kichwa, uchovu,homa na kutapika.Siku 9 kabala ya dalili,alitembelea mapango ya Kitum mlima Elgon mbuga za wanyama.Pamoja na juhudi kubwa za kumsaidia mgonjwa alifariki siku ya 5 hakuna matukio mengine tena yaliendelea.​
1980
Kenya​
Kenya​
2​
1 (50%)​
Katika pango la Kitum mbuga za wanyama za mlima Elgon.Pamoja na uangalizi maalum akiwa Nairobi mgonjwa alifariki daktari aliyekuwa anampa huduma ya kupumua naye alipata dalili siku9 baadae lakini akapona siku 4 baadae​
1975
Johannesburg, South Africa​
Zimbabwe​
3​
1 (33%)​
Msafiri alikuwa amesafiri muda si mrefu kwenda Zimbabwe na akalazwa hospitali nchini Afrika kusini.Maambukizi yalikwenda kwa abira mwenzake na nurse aliyekuwa anamhudumia.Msafiri huyo alifariki lakini huyu msafiri jirani yake na nurse walipona baada ya kupatiwa matibabu ya hali ya juu.​
1967
Germany and Yugoslavia​
Uganda​
31​
7 (23%)​
Matukio ya pamoja yalitokea kwa wafanyakazi wa maabara ambao walikuwa wanafanya kazi kuwahudumia nyani wa kijani walioingizwa kutoka Uganda.Kwa nyongeza zaidi pamoja na matukio 31 kutangazwa kuna cases nyingine ziligunduliwa kwenye vipimo vya damu kwa wanyama wanyama hao.​
* maana yake ni tukio lililothibitishwa na maabara peke yake​
 
Back
Top Bottom