Tija na ufanisi- tujadiliane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tija na ufanisi- tujadiliane

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mtazamaji, Feb 22, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Maneno haya si mageni wengi wetu kwa hasa kuyasikia katikalugha ya kigereza ya kitamkwa na viongoziwetu wa siasa, makaazini na hata sisi wenyewe kuyasistiza manyumbani na sehemu nyingine.

  Kwa kingereza ni effective na Efficiency.

  Napenda kuleta mada hii kujadiliana dhana nzima ya haya maneno dhana ya utendaji ma mashirika ya ummma na hata ya sisi binasfi kuyafikiria kabla ya kushauri au kufanya jambo.


  • Je maana/defintion ya maneno haya ni nini
  • Kipi ni cha muhimu kati ya tija na ufanisi?
  • je inawezekana kuwa na tija bila ufanisi au ufanisi bila tija?
  • Je tunaweza kutolea mfano utendaji wa shirika lolote la kwa kutumia maneno haya mawili

  Naanza kwa observation yangu ya kichokozi . Mara nyingi mashirika yetu ya umma viongozi na hata sisi binafsi katika maamuzi na utendaji na utumiaji wa rasilimali za ofisi ,shirika hata binafsi tumekuwa tunafanya maamuzi amabayo ni ya kitija(effective) lakini si ya kifanisi ( efficiency)

  Nawasilisha
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tija= Ni ile hali ya kitu kuwa na faida au matokeo chanya, ni hali kitu, jukumu,mfumo ambao unamletee mtu manufaa
  ufanisi- Ni namna ya kulifanya jambo kwa ubora na uangalifu wa hali ya juu. Pia ni hali ya umakini katika kufanya mambo yako
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Efficency/ Ufanisi ni hali au uwezo wa kutumia rasilimali chache au ndogo kuzalisha au kutoa huduma kubwa

  kwa maelezo haya inaonyesha maamuzi hayaya serikali yanalenga kwenye tija nasi ufanisi

  • Ofisi ya serikali kutumia shangingi just kusafirisha mtu au nyaraka ndogo kutoka mkoa mmja kwenda mwingine kwangu ni maamuzi yanayolenga tija na si ufanisi. kwa nn wasitumie Courier service na wafanyakazi kusafiri kwa mabasi.

  • Tume ya uchaguzi kuongeza idadi ya majimbo vile vile ni mamuzi ya kuuongeza tija bila kuzingatia ufanisi.

  • Serikali kutumia shangingi kumepeleka ofisa kutoka nyumbani kwenda kazini maamuzi yasiyo na tija na wala sio ufanisi. kwa nini wasitumie vitara au Mark II?
   
Loading...