Abdull Kazi
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 322
- 255
Kampuni ya simu ya tigo imekuwa ikinikata kiasi cha fedha mara kwa mara huku wakinitumia ujumbe kuwa nimesikiliza hadithi wanazozijua wao,binafsi sikuwahi kujiunga na huduma yoyote zaidi ya ile ya kupiga mitandao tofauti,awali nilipokuwa ninapata ujumbe wMao unaonieleza kuwa nimekatwa kiasi cha sh.320 kwa kusikiliza hadithi hizo nilijibu kwa kuandika neno ondoa na kutuma katika namba iliyoniletea ujumbe na zoezi lilikuwa linasitishwa kwa muda sasa wameanza tena.Nimedhamiria kuwashitaki kwa kuwa suala hili limepigiwa kelele bungeni na kwenye vyombo vya habari bila mafanikio nafanya hivi kwa ajili ya kutetea haki yangu na wengine dhidi ya wizi wa aina hii ninazo mesegi zote kama ushahidi na ninawaomba na wengine waliokutwa na madhila kama yangu tuungane ktk hili