TIGO PESA mnavyofanya si haki hata kidogo

TIGO PESA mnavyofanya si haki hata kidogo

BURUTA

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2015
Posts
639
Reaction score
824
Leo tangu asubuhi mapema na takriban kutwa nzima - kulikuwa na hitilafu mfumo wenu wa kununua vifurish lkn hamkutuambia wateja wenu tangu awali- mlikaa kimya. Mimi nimekuwa nikijaribu kununua kifurushi cha intanet cha wiki cha sh 2500 sikuwa napata jibu lolote wala kifurushi. Nimejaribu mara 4 bila mafanikio.
Kufika mchana saa 9 hivi nikajaribu tena ndiyo ikakubali. Lakini baadaye kidoga mkaleta msg ya kuomba radhi kutokana na ttzo hilo. Hata hivyo baadaye kucheki salio lamgo la Tigo pesa nikakuta nimekatwa manunuzi ya vifurushi 4 vya sh 2500 yaani jumla sh 10,000 ingawa kifurushi nilichopata ni kimoja tu kinachoisha tar 12/9 na nikaona jumla ya msg 4 za manunuzi ya vifurushi. Yaani kila nilipokuwa najaribu kununua kifirushi hela imekatwa kutoka acct yangu ya Tigo pesa. Sio haki.
 
Nami pia yamenikuta nimekuja kukatwa shs 4000 kwa mara zote nne nillzokuwa nikijaribu kununua kifurushi cha intaneti cha sh 1000 bila kupata majibu.
Mwishowe jaribio la mwisho mchana ndiyo kikaja kifurushi kimoja na msg 4 za mrejesho wa manunuzi lkini nimekatwa hela ya vifurushi 4.
Acheni uhuni kama tatizo lipo tuambieni mapema ili tusiwe tunajaribu jaribu kununua vifurushi
 
Mimi wamenifanyia ujinga mkubwa sijajiunga kifurushi afu wananiunganisha wenyewe kupitia tigopesa.
 
Back
Top Bottom