Tigo nirudishieni kifurushi changu!

Sinewy

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
366
170
Jana nimeunga kifurushi cha mwezi cha ofa maalum cha 20000,GB20 wakaniletea confirmation mesage lakini mpaka leo hakifanyi kazi na ukiangalia salio wamekata ningekuwa dar ningewashitaki TCRA ila sema niko huku shinyanga
 
mbaya zaidi ukipiga customer care wanakwambia hicho kifurushi hakipo
 
Jana nimeunga kifurushi cha mwezi cha ofa maalum cha 20000,GB20 wakaniletea confirmation mesage lakini mpaka leo hakifanyi kazi na ukiangalia salio wamekata ningekuwa dar ningewashitaki TCRA ila sema niko huku shinyanga
Sio lazima kufunga safari ya kwenda Dar kushtaki.Tumia tovuti ya tcra sehemu ya malalamiko.
 
Wezi tu hawa tigo nao jana iringa kulikua hakuna network masaa 7 hadi sasa hawajasema chochote ikiwepo kuongeza muda kwa vifurushi vyetu kushindwa kutumia.
 
Tigo lazma warudishe vifurushi vya watu wa Iringa.

Tuungane kumpelekea waziri malalamiko.

Wawekezaji hawa hatuwataki.

Naikumbuka tritel sijui imeishia wapi
 
Tigo wanaanza kuwa jipu kuna mama mmoja aliibiwa simu ktk lain kuna laki tano alichofanya akaenda kurenew laini akakuta pesa haipo sasa akaenda Tigo hapo mlimani city wakamwimbua wee umeibiwa huko unakuja huku nenda polis huko napo wanamzungumsha sasa kaenda tcra sijui watamsaidia.....jamani laki tano......
 
Tigo ni janga tena kubwa mno ,sijui kwa nini mtumiaji simu huwa Hana thamani kabisa kwao,
 
Back
Top Bottom