Tigo ni matapeli?

Tigo ni matapeli?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,497
Reaction score
5,271
Nimekopa sh. 200 kutoka tigo.
cha ajabu wameniambia salio la account yangu halitoshelezi kupiga simu,
na wakati huohuo nikiangalia salio
kuna jumbe usemao SALIO LAKO ULILOKOPA KUPITIA TIGO NIWEZESHE NI SH. 200.00/-
JAMANI JE HUU SI UTAPELI?
HELA ya mkopo iko kwenye simu lakini simu hazitoki kwa sababu salio langu halitoshelezi kupiga.
:juggle:
 
Bure gharama, hebu fasta kanunue vocha ndio ulete malamiko.
Mtapenda mitelemko hadi lini?
Ana haki ya kulalama make hakuna aliye waambia kuwa kuna huduma hiyo. Wameshikwa pabaya na Zein
 
Itakuwa ni system error kuna siku ilishawahi kunitokea hivyi hivyo kama wewe then baada ya dakika kadhaa wakarekebisha
 
Tigo mtandao wao umeanza kuleta kwikwi kama leo majira ya saa5 mpaka mida hii bado simu za tigo zinagoma kutoka hata msg pia!!
 
Mm nilikopa kisha nikaambiwa nimekopeshwa 200 nadaiwa 220, mazingaombwe yake nikiangalia salio ziro nikipiga simu salio halitoshi, balaa zaidi nilivyo weka pesa wakakata 220. wezi wakubwa hao, wanajua hatuwezi kwenda kuwadai 220.
 
Hakuna biashara inayolipa tanzania na africa kwa ujumla kama huduma za simu,utapeli ni mkubwa sana

ndiyo maana kila siku makampuni ya simu yanaibuka.

ebu jiulize makampuni yote ya simu yanatoia matangazo katika redio zaidi ya 60,tv zaidi ya 7 na magazeti karibu yote,mitandao,blogs nk

kwa ufupi kampuni moja inatumia zaidi ya bilioni 1 kwa mwezi kunako matangazo tu unadhani wanaingiza shilingi ngapi na zinatolewa na nani ni watu kama nyie

pole na ujifunze

labda turudie mfumo wa posta wa kuandika barua
 
Mkuu, solution ya hii kitu huwezi kupata JF, wapigie wahusika kwa 100 waambie, kuna siku waliniibia elfu 3, nilikomaa nao mpaka wakarudisha!
 
wizi mtupu...................sh1 yenyewe kwa sekunde noma.....hiyo dakika inavyokimbia we acha tu...........tigo jamani
 
Back
Top Bottom