Tigo ni jipu Arusha

daud donasian

Senior Member
Nov 6, 2015
101
33
Kwa wateja wa mtandao wa tigo jijini Arusha watakua wana nielewa point yangu.Katika maeneo mengi ya mji wa Arusha mtandao wa tigo umekua ovyo sana haswa kwa matumizi ya internet.

Kabla ya ku access internet utaona network iki approach H+ lakini ukianza ki access maramoja utaona network iki mbwelambwela mara E, 3G na hata mara zingine kukata mtandao kabisa (emergency call)

Lakini cha kushangaza zaidi tofauti na mitandao kongwe kabisa hapa nchini, tigo wameanza kurukia mtandao wa 4G bila kujali kuwa mtandao wa 3G hauja kidhi viwango. Kama waasisi wa 4G wangekuwa Airtel pengine angalau na Vodacom ukizingatia mtandao wao uliopo walau una kidhi mahitaji ya watumiaji.

Waimarishe minara yao kwanza wakisha faulu hilo mengine yata fata automatically tu na sio vinginevyo.

WALENGWA, WADAU ARUSHA

Naomba kuwasilisha hoja wakuu!
 
Back
Top Bottom