Mimi nilikuwa naanzisha thread kuhusu hawa Tigo ila baada ya kuiona hii basi sivibaya kuongezee hapahapa.Nimeingia ndani ya nchini wiki kadhaa sasa nanilipofika tu nikawa nimejiunga na mtandao wa airtel lakini cha kushangaza nilishindwa kutumia internet nanikawa nimekwenda customer care kuwaeleza tatizo langu nanikawapa simu yangu wakacheki na kuniambia kuwa saa moja baadaye ningelianza kutumia internet kwa bahati mbaya sikuweza;kwa hiyo wiki baadaye nikaamua kwenda Tigo.Nilianza kutumia pay as you go surfing mpaka nilipoelezwa kuna kitu wanaita kifurushi,hivyo tangu hapo nimekuwa nikitumia internet bila tatizo ingawa sio faster sana ila walau inatosha.
Tatizo ni customer care,tigo pesa au Tigo sevice.Hivi inakuwaje unapotaka kuongea nao lazima ulipie pesa?Yaani mtu ninashida ya kutaka kupata ufafanuzi wa aidha gharama,pesa au tatizo lolote lile,yaani hawapatikani hata upige siku nzima je wapo kwa ajiri ipi?mbaya zaidi ukipiga namba 150. Ambayo sijui inahusu pesa ile namba kwanza kabisa inaita tu na hakuna mpokeaji na kila ukikata tayari unakuwa umeshakatwa pesa yao? Je inakuwaje mimi kama mteja sijapata huduma yeyote hata ile kupokelewa tu simu haipokelewe bado nakatwa pesa .je hii ni haki kweli kama sio wizi?na kila ukiwapigia watakata pesa tu..agh!halafu ile namba 100 nasikia haiganyi kazi siku hizi hata kama ukiipata. Ile huwezi kuongea na wahudumu. Hadi upige namba nyingine 0713800800 ambayo utachajiwa kila upigapo .je kwa nini iwe hivyo? Nimewauliza wanasema eti kisa ni kuwa watu walikuwa wanapiga sana simu bila sababu maalum kwa hiyo wanafanya hivyo ili kupunguza usumbufu..mmh hivi kweli mteja wako anaauliza swali au tatizo lolote unamwona kuwa msumbufu? Is this our services to customers?