tiGO mnatufukuza wateja wenu bila kujijua

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,031
21,499
hawa tigo walitangaza kwamba uki top up salio lako kwanzia buku litakua doubled. cha ajab kila nkiweka wanauchuna af kesho yake wanajifanya kuommba radhi na wananipa dk.13 za kuongea. nikafanya calculcation nikagundua hata hzo dakika wanazokupa sio actual. je hili tatizo ni kwang peke yang au kuna wakuu wengine limewakuta?
 
hawa tigo walitangaza kwamba uki top up salio lako kwanzia buku litakua doubled. cha ajab kila nkiweka wanauchuna af kesho yake wanajifanya kuommba radhi na wananipa dk.13 za kuongea. nikafanya calculcation nikagundua hata hzo dakika wanazokupa sio actual. je hili tatizo ni kwang peke yang au kuna wakuu wengine limewakuta?

no wonder ule mchezo wa kipwani unakuwa reffered na jina lao....
 
i hate it,siku lazima nitinge ofisini kama kichaa ivi
mimi nilishaacha kununua salio kbs,labda nipigiwe tu washenzi sana na zile sms zao za kila dk
 
hahahahahaaaaa....nlifikiri yamenikuta mimi peke yangu..kumbe tupo wengi...THIS IS BONGO LAND....!! Hakyanan tena...!!
 
TCRA wamelala baada ya shibe ya takrima kutoka kwa hawa jamaa wa mitandao. Hawana habari ya kinachoendelea huku.
 
Tigo vipi ndo matangazo mnayafanya ivo? Mana ukiuliza salio unaambiwa pata sms 100 na dakika tano kwa kutuma mia zaidi katika namba 15313,mbona inachanganya sasa ivi ni dk 5 si 10 tena!
 
Mimi nilikuwa naanzisha thread kuhusu hawa Tigo ila baada ya kuiona hii basi sivibaya kuongezee hapahapa.Nimeingia ndani ya nchini wiki kadhaa sasa nanilipofika tu nikawa nimejiunga na mtandao wa airtel lakini cha kushangaza nilishindwa kutumia internet nanikawa nimekwenda customer care kuwaeleza tatizo langu nanikawapa simu yangu wakacheki na kuniambia kuwa saa moja baadaye ningelianza kutumia internet kwa bahati mbaya sikuweza;kwa hiyo wiki baadaye nikaamua kwenda Tigo.Nilianza kutumia pay as you go surfing mpaka nilipoelezwa kuna kitu wanaita kifurushi,hivyo tangu hapo nimekuwa nikitumia internet bila tatizo ingawa sio faster sana ila walau inatosha.
Tatizo ni customer care,tigo pesa au Tigo sevice.Hivi inakuwaje unapotaka kuongea nao lazima ulipie pesa?Yaani mtu ninashida ya kutaka kupata ufafanuzi wa aidha gharama,pesa au tatizo lolote lile,yaani hawapatikani hata upige siku nzima je wapo kwa ajiri ipi?mbaya zaidi ukipiga namba 150. Ambayo sijui inahusu pesa ile namba kwanza kabisa inaita tu na hakuna mpokeaji na kila ukikata tayari unakuwa umeshakatwa pesa yao? Je inakuwaje mimi kama mteja sijapata huduma yeyote hata ile kupokelewa tu simu haipokelewe bado nakatwa pesa .je hii ni haki kweli kama sio wizi?na kila ukiwapigia watakata pesa tu..agh!halafu ile namba 100 nasikia haiganyi kazi siku hizi hata kama ukiipata. Ile huwezi kuongea na wahudumu. Hadi upige namba nyingine 0713800800 ambayo utachajiwa kila upigapo .je kwa nini iwe hivyo? Nimewauliza wanasema eti kisa ni kuwa watu walikuwa wanapiga sana simu bila sababu maalum kwa hiyo wanafanya hivyo ili kupunguza usumbufu..mmh hivi kweli mteja wako anaauliza swali au tatizo lolote unamwona kuwa msumbufu? Is this our services to customers?
 
Nimekuwa nje ya nchi nyingi tu zingine zina wananchi wengi sana tu ukilinganisha na tz lakini bado kupata huduma ya maulizo ni bure na hakuna shida kubwa ya kuwapata customer cares kama jinsi ilivyo hapa. Je tatizo ni nini?
 
nyie hamuelewi tu wamefanya equivalent, manake tigo kwenda mtandao mwengine dk 1 ni kama 450 sasa wakikupa dk 2 ni sawa na 900 na hizo dk 2 nyengine si buku hilo??? Au nyie mwataka mpewe hela kabisa, dah wabongo kwa ofa
 
Mimi hawa tigo wananishangaza. Nikitumia internet ya simu hawanikati hela.
 
Kwani SALIO MARA MBILI maana yake ni DOUBLE SALIO? wajinga ndio mliwao... (HAMIA AIRTEL!!!!)
 
hawa tigo walitangaza kwamba uki top up salio lako kwanzia buku litakua doubled. cha ajab kila nkiweka wanauchuna af kesho yake wanajifanya kuommba radhi na wananipa dk.13 za kuongea. nikafanya calculcation nikagundua hata hzo dakika wanazokupa sio actual. je hili tatizo ni kwang peke yang au kuna wakuu wengine limewakuta?

Hayo maigizo na wizi ulio kubuhu , leo nime weka 5,000 sijaona hiyo double double , hata mimi nilidhani labda sababu hiyo vocha nilinunau muda mrefu , kumbe ni kwe wengine pia.
 
Nani anahusika na wizi huu unaoendeshwa na TIGO.
Kuna matangazo ya promotion mbalimbali za TIGO ambayo hayaendani kabisa na promotion zenyewe. Mfano ni ile ya nunua muda wa maongezi kupitia tigo pesa ili upate salio marambili na hii promition mpya iliyoanza tar 3 mwezi huu september ya nunua na kuweka salio la kuanzia 500 iliupate mara mbili. Jambo lakusikitisha ni kua wanachokitangaza hakiendani kabisa na huduma yenyewe kwani ukinunua hilo salio utakachopata ni dakika za bure tu hakuna cha salio kua mara mbili ya ununuacho!
Hofu yangu ni kwanini vyombo au mamlaka zinazohusika zinaacha kampuni hii kuendelea kufanya utapeli kama huu mchana kweupe?
 
wanasema eti ukiongeza salio utapata mara mbili ya fedha ulizoongeza, kitu ambacho si kweli kabisa. Wanachokuongezea ni robo tu ya salio uliloongeza.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom