Tigo 4g ( 1 )vs halotel 3g( 3)

Tigo 4g ( 1 )vs halotel 3g( 3)

Halotel wako juu sana, nimefanikiwa kusafiri kwa basi kutoka Dar mpaka Mbeya, njia yote network iko vizuri. Tigo network yake inaishia Ubungo tu
 
Mara mia utumie tigo 3g kulilo tigo 4g... Nipo kimara mwisho ila najuuuuuta kupata hiyo line ya 4g
 
Halotell ndo mpango, iko swafi kabisa, hizo vifaaa vyenu vitakuwa kimeo
 
Vijijini ndo usiseme kuusu halotel,kwa internet ina kimbiza Tigo3G,Tigo4G,Voda3G pamojana Airtel3G.
 
Baada ya kuona kichwa kilivyo kizuri nika-like bila hata kusoma main body,baada ya kusoma maelezo yenyewe naona bora ni-unlike tu.
 
Watumiaji wa Halotel hapa Dar wamekuwa ni wengi mno hata Ile spidi ambayo ilikuwa inapatikana mwanzo sasahivi haipatikani tena
 
same here hata 1mbps kufika tabu, wakati 4g tigo ni 10mbps kupanda juu
Faida ya Halotel ni kupatikana maeneo mengi kwa spidi ya kawaida.
Kwa mfano ukiwa unatoka Moro kuja Dar, hata ukiwa porini kama mtandao wa halotel upo basi ni 3G, wakati hawa wengine 3G unaiacha Moro mjini.
Pia mitandao mingine inachagua sana maeneo, yaani katika mji mdogo tu, ukiwa mtaa huu 2G na huwezi kufungua hata web page ukiwa mtaa mwingine 3G na spidi imepanda kidogo, wakati kwa Halotel haiko hivyo, ingawa si kwa 100% ila inaizidi mitandao mingine.

Kwenye suala la spidi tigo 4G iko juu, ingawa sijawahi kupima ila nimetumia router za tigo (Huawei) 4G na halotel natumia pia. Ila udhaifu ndio huo nilioueleza hapo juu.
 
Back
Top Bottom