TICTS yawa kisiki kwa serikali ya Tanzania!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TICTS yawa kisiki kwa serikali ya Tanzania!!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vitendo, Apr 25, 2010.

 1. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ASA ni dhahiri kwamba, mkataba kati ya Serikali na Kitengo cha Kuhudumia Kontena Bandarini - TICTS, hauwezi kuvunjwa.

  Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, kazi ya kuuvunja itaambatana na gharama kubwa ambazo kwa sasa Serikali haiwezi kuzimudu.

  Akitoa taarifa ya Serikali kuhusu hatua za utekelezaji wa Azimio la Bunge juu ya utendaji usioridhisha wa TICTS mjini Dodoma, Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema busara imeonesha hakuna haja ya kuvunja mkataba huo kwa sasa.

  Kama mkataba ukivunjwa, Serikali itapaswa kulipa fidia ya Sh bilioni 645, hali ambayo ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi wa Tanzania.

  Alisema Serikali ilimuuliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Taifa linaweza kushinda kesi hiyo ya mkataba na kubaini kwamba haiwezi kushinda kwa sababu uliingiwa kihalali.

  “Mkataba huu ni halali na iwapo Serikali itatumia nguvu kuvunja au kusitisha nyongeza ya muda wa ukodishaji, na suala hili likafikishwa kwa msuluhishi, Serikali ingepata hasara kwa kuilipa TICTS fidia iliyokadiriwa kuwa Sh bilioni 645,” alisema Waziri Kawambwa.

  Bunge lilitaka kusitishwa kwa nyongeza ya muda wa miaka 15 iliyopewa TICTS kwa kuwa nyongeza hiyo ilitolewa kinyume cha utaratibu, kwani katika mkataba wa awali kifungu cha 9.1 kiliweka bayana kuwa kifungu cha muda wa mkabata hakitafanyiwa marekebisho yoyote bila kufuata taratibu zinazooneshwa katika mkataba wa kwanza.

  Aidha, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka 2007/2008 alieleza kuwa nyongeza ya miaka 15 waliyopewa TICTS haikuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 21 ya mwaka 2004, na hivyo nyongeza hiyo ni batili.

  Katika mkutano wa 11 wa Bunge, hoja binafsi iliwasilishwa ya kuvunja mkataba na TICTS kutokana na utendaji wake usioridhisha na Bunge kupitisha azimio Aprili 25, 2008.

  Pamoja na kushindwa kuvunja mkataba huo wa nyongeza, Dk. Kawambwa alisema Serikali imefanikiwa kuondoa ukiritimba wa TICTS bandarini na pia kufanya marekebisho kadhaa ya msingi yanayotaka TICTS kuwajibika zaidi bandarini na pia kuondolewa kwa nafasi yao ya kukusanya tozo na kwamba sasa bandari itafanya kazi yake hiyo yenyewe.

  Mambo mengine ambayo Serikali iliibana TICTS ni pamoja na kutayarisha na kuwasilisha mpango wa uwekezaji wa miaka mitano mitano kwa kipindi cha Januari 2009 mpaka 2013, Januari 2014 mpaka 2018 na wa miaka saba, kuanzia Januari 2019 mpaka 2025.

  Pia viwango vya vigezo kwa ajili ya kupima utendaji vimebadilishwa na sasa vitapimwa kwa ufanisi wa matumizi ya yadi; ufanisi wa mitambo inayotumika kuhudumia kontena katika yadi.

  Aidha, TICTS kurudisha vifaa vilivyokwisha muda wake wa matumizi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na kurekebisha utaratibu wa kukusanya tozo kwa wanaotumia miundombinu ya bandari.

  “Katika hili, TICTS walikuwa wanakusanya tozo kila siku na kuilipa TPA mwisho wa mwezi, kwa sasa ukusanyaji huo wa kila siku utafanywa na bandari yenyewe,” alisema Dk. Kawambwa.

  Alisema Serikali na TICTS wametiliana saini mkataba mpya wa nyongeza namba tatu wa kuelewana katika utekelezaji wa masuala yaliyokubaliwa na pande zote mbili.

  Dk. Kawambwa alikiri kuwapo upungufu katika baadhi ya vipengele vya Mkataba huo uliosainiwa Mei 5, 2000 ukiwa awali wa miaka 10 na kutarajiwa kwisha mwaka huu.

  Mwaka 2005 mkataba huo uliongezwa kwa miaka 15 kabla ya muda wa ukodishaji wa awali kumalizika.

  Utaratibu wa kubinafsisha kitengo hicho ulitumia mfumo wa Mamlaka ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) ambapo ulikubaliwa na taasisi hiyo, Serikali na Benki ya Dunia.

  Hata hivyo, Waziri Kawambwa alisema hatua zilizokwishachukuliwa zimesaidia kuongeza ufanisi katika bandari na kwa sasa utendaji kazi wa bandari hiyo unaridhisha.

  Awali wadau walibainisha kuwa pamoja na matatizo katika mkataba huo, pia yapo matatizo mengine yanayozorotesha ufanisi wa utendaji katika bandari.

  Matatizo hayo ni ya kukosekana kwa ufanisi wa kushughulikia kadhia ya forodha, upatikanaji wa haraka wa taarifa za malipo na uwekaji tozo ili watumiaji wa bandari wasiigeuze kuwa ghala la bidhaa zao.

  Baada ya kuiondolea ukiritimba TICTS, Serikali kupitia TPA, imeanza kutekeleza mpango wa kuboresha miundombinu ya bandari kwa kujenga gati mbili mpya na kuboresha zilizopo ili kuongeza uwezo wa kuhudumia meli kubwa.

  Kutokana na juhudi za kuboresha huduma ya bandari, Waziri Kawambwa amesema kwa sasa muda wa kontena kukaa bandarini umepungua kutoka wastani wa siku 20 Januari 26, 2009 kufikia siku 12 Februari mwaka huu, huku muda wa meli za kontena kusubiri nje ya lango la bandari umepungua kutoka wastani wa siku 25 Januari mwaka jana mpaka siku 3.5 Februari mwaka huu.

  Taarifa hiyo haikujadiliwa na Bunge baada ya Spika Samuel Sitta kutumia vifungu vya kanuni zinazoendesha Bunge na badala yake kuiagiza Kamati ya Miundombinu kuendelea kufuatilia ufanisi wa TICTS na kulipa Bunge taarifa mara kwa mara.

  Alisema Serikali imefanya inachoweza kufanya na imefikia hapo na hakuna sababu za kuendelea kulumbana.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  ".....Kama mkataba ukivunjwa, Serikali itapaswa kulipa fidia ya Sh bilioni 645, hali ambayo ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi wa Tanzania..."
  ....Nini maana ya hii maneno?, ...na ninini hasara ya kuendelea na mkataba?...whats cost-benefit balance here?..Hivi hatuna wataalamu kiasi cha kusikitisha hivi
   
 3. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  NI BORA TULIPE 645 bn/ kuliko upotevu mkubwa wa hela, nadhani ni busara mkataba ungevunjwa,tulipe hizo bilions halafu tujipange upya
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ina maana zile mbwembwe za kipindi kile kwamba mkataba ulio ongezwa kinyemela umesitishwa ilikuwa ni danganya toto? Na hii habari ya kwamba "busara imeonesha hakuna haja ya kuvunja mkataba huo kwa sasa." Ni busara ya nani? Bongo bana muda si mrefu tutasikia hata ule wa Rites kuna busara imetumika. Hivi hao watu walioingia mikataba hiyo si wapo? Nini kinafanyika au kimefanyika kuhakikisha mikataba feki na ya wizi haaingiwi tena na serikali?
   
 5. s

  smilingpanda Member

  #5
  Apr 25, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani hakuna serikali pumbavu kama hii yetu,ukiangalia maelezo yaliotolewa hapo juu utaona dhahiri kwamba makataba huo hauko 50/50.Ni sawa sawa na mtu atake kukuuzia kwamfano sindano na uzi kwa milioni 1,ukikubali we si kichaa.
  na pia tusisahau wasemavyo waswahili "kiendacho kwa mganga,hakirudi"
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini mkataba usivunjwe na haya mabilioni wakalipa wale waliotuingiza mkenge?
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hakuna straight agenda katika siasa za TZ. Serikali inapobadili badili statement zake haioni kama inaonesha kukosa umakini na kufanya usanii uliotukuka?
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Serikali ingekuwa serious na kuuvunja huu mkataba mbona ni rahisi sana! Ni kiasi cha kutumia mbinu za kijasusi na wao TICTS wenyewe wanafungasha! Akuanzae mmalize! Wao kama walitumia mbinu chafu kuingia mkataba kwanini tusitumie hizo hizo mbinu kuuvunja?
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ni serikali ya wahuni inayoendeshwa kihuni.
   
 10. w

  wakubaha Member

  #10
  Apr 25, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Yani hii nchi inashangaza sana...hivi hamna wanasheria wenye uchungu na nchi hii wakuweza kuangalia mikataba hii na kueleza uma ukweli ni upi? tuachane na maneno ya wanasiasa tupiganie haki yetu.
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Jamani muelewe kuwa TICTS ni mali ya vigogo ambao wengi ndo wako serikalini so kwa vyovyote vile serikali haiwezi kuuvunja. Kumbukeni Ka'magi wakati wa kampeni za Kikwete mwaka 2005 kule Bukoba wakati K'wete ameitisha harambee na wafanya biashara wa mkoa, K'magi alichangia zaidi ya millioni 85 na huu ndo ulikuwa kama mtaji hadi leo anakula faida kupitia hii TICTS. Ni wakati wa kufanya kitu tuacheni hivi vilio vya kila siku. let's go to October!
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  But isn't it the same thing Kawambwa said about RITES? That breaking the mkataba would put the government in the quandaray of paying the Indian company humongous amounts of money. Guess what, the Indian company turned around and broke the mkataba. Kama TACTICS iliongezewa mkataba kinyume na tararibu hawana sababu ya kwenda mahakamani kama serikali ingeuvunja huko mkataba. Hawa mawaziri wetu wamesoma wapi?
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tunahitaji overhaul ya system nzima.................wote wameoza...............kweli mtu unaingia mkataba kama serikali halafu huna hata sehemu ya kujilinda?.........damn
   
 14. T

  Tom JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uko sawa, CCM ni kichaa fulani hivi.
   
Loading...