...tick-tick!...Mke kanogewa na Ufisadi; Mume hajui la kufanya

Umenikumbusha tukio la muda kidogo, kuna mdada alipata position ya mizani akiwa ndio tu ameolewa na katokea familia za kawaida kabisa huko vijiji fulani huko kanda ya ziwa.
Alipata pesa nyingi sana, akajenga na mumewe, wakabadili kabisa mfumo wa maisha, magari, manguo, ili mradi tu ahueni, na wapambe bahati nzuri wakawashauri waanzishhe biashara, basi wakanunua masemi trailer kama 5 ya kubeba mafuta.
LAkini ajabu ni kuwa ilitokea akafukuzwa kazi, magari ya mafuta yakapata ajali baadhi, nadhani alipata shock, manake alianguka na kuzimia alipoamka alikuwa kichaa wa kuvua nguo, muda mfupi bdae akafariki, hata miaka 30 hajafikisha,
nikimkumbuka inanifanya nijifikie sana, naweka wapi uzito katika maisha yangu,
yale magari yaliobakia na nyumba, kwa hasira mumewe aliuza, na kuanza maisha tofauti kabisa.
 
Umenikumbusha tukio la muda kidogo, kuna mdada alipata position ya mizani akiwa ndio tu ameolewa na katokea familia za kawaida kabisa huko vijiji fulani huko kanda ya ziwa.
Alipata pesa nyingi sana, akajenga na mumewe, wakabadili kabisa mfumo wa maisha, magari, manguo, ili mradi tu ahueni, na wapambe bahati nzuri wakawashauri waanzishhe biashara, basi wakanunua masemi trailer kama 5 ya kubeba mafuta.
LAkini ajabu ni kuwa ilitokea akafukuzwa kazi, magari ya mafuta yakapata ajali baadhi, nadhani alipata shock, manake alianguka na kuzimia alipoamka alikuwa kichaa wa kuvua nguo, muda mfupi bdae akafariki, hata miaka 30 hajafikisha,
nikimkumbuka inanifanya nijifikie sana, naweka wapi uzito katika maisha yangu,
yale magari yaliobakia na nyumba, kwa hasira mumewe aliuza, na kuanza maisha tofauti kabisa.

...haya sasa. Ngoja niwa printie hii wakasome. Labda mdada atapata "wake up call."
Wengi mmeshauri Immovable assets. :lol::lol::lol:...inafurahisha wengi mnafikiria kuwekeza huko.

Duh, Haika kisa chako kinasikitisha, "Easy come easy go!" lakini isifikie mpaka mmoja akawa chizi.
Hiyo ni hatari!
 
Kuna wakati wanawake tunawehuka kwa ajili ya pesa, ni kitu cha kusikitisha sana, mie nikimkumbuka yule dada huwa naumia roho sana, alikuwa si mchoyo hata kidogo, basi tu ulimbukeni na hasira zinazotokana na maisha ya shida tangu utotoni.

Mwanamke kama huyo ni ngumu kushaurika, mie naelewa. Saa hizi ana mawenge tu huko kicwani.
Labda watoto wake wamwambie, wamuulize mama yao 'kama alikuwa masikini utotoni, mbona ameweza kuwa mama mzuri? kwanini anaogopa watoto wakipata shida kidogo? wamjulishe kuwa wanaweza kuhimili maisha bila yeye kujitoa sadaka, kuwa wamefundishwa shule kuwa wizi ni mbaya, wamchimbe mshahara wake, mpaka aone aibu kuwatazama, wamuambie kuwa wataona aibu sana akifungwa jela, kuliko wakihamia shule nyingine'

Nilishawahi kutumia silaha ya watoto
 
...Amen LD, Amen...hata mimi nawaombea waendelee tu "for better or worse til death do them apart!"

Hivi ni aje tena?
MLA HULIWA!!!!
Wamekula wasubiri kuliwa.
 
02D78330.jpg
...ni mke na mume waliodumu miaka 15 ya ndoa. Wamejaaliwa watoto wawili, miaka 12, na miaka 9. Wazazi wote ni waajiriwa wa serikali. Baada ya kujinyima hapa na pale, mume akaweza kujenga nyumba ya vyumba viwili, wakajistiri. Mke nae akajitahidi kukopa hapa na pale angalau wakaweza kununua 2nd hand (reconditioned) corolla tokea japan.


Kimbembe kimeanza miaka mitatu iliyopita. Mke amebahatika kupangiwa ofisi nyeti ambayo inajihusisha na upatikanaji wa mapato ya serikali. Kufumba na kufumbua, mke kajenga nyumba mbili za kisasa kisha kazipangisha. Nyumba waliyokuwa wanaishi ameiongezea vyumba vingine vinne pamoja na vikorombwezo na nakshi mbali mbali. Almuradi maisha yao shwari mara kumi ya hapo awali.

Kama hilo halitoshi, kawahamisha watoto public school na kuwapeleka kwenye Academy ambako kwa mwaka pamoja na vikorombwezo vingine, anawalipia mara kumi ya mshahara wake. Haikupita muda, kanunua brand New Toyota VX, na sasa ameagiza Range Rover Vogue (Sport) toka Uingereza kwa ajili ya mumewe.

Jamaa (mume) pamoja na unafuu wa maisha, roho yake haimpi! anaona "likibumbuluka" ofisini kwa mkewe, watakumbwa waliokuwamo na wasiokuwamo. Kajaribu kumsahuri mkewe aachane au apunguze mabomu kazini, Mke hasikii la mwadhini wala mnadi swala!... anasema "tumeteseka sana kimaisha, acha nasi tujiliwaze kidogo!"

Jamaa hajielewi elewi kabisaaa. Akifikiria ndoa, yake haijwahi yumbishwa kwa lolote miaka yote kumi na tano. Lakini, kasi ya mkewe na likilipuka, watataifishwa mali zote na huenda mkewe akaishia jela. Mzee wa watu anafikiria aanzie wapi kuepusha 'bomu hili la kutega'

Mna maoni gani.


Mkuu Mbu, binadamu tunatofautiana katika mambo mbali mbali. Kuishi maisha ambayo una wasiwasi kwamba wakati wowote ule familia inaweza kuathirika sana kwa mambo ambayo mke na mume katika familia hiyo wanaweza kabisa kuyazuia ni upumbavu wa hali ya juu. Huyo mume pamoja na kuwa maisha yao yamekuwa mazuri sana lakini inaelekea hana furaha hata kidogo kwa kujua kabisa maisha yanaweza kubadilika wakati wowote ule na familia kusambaratika. Inaelekea Mume hana msimamo maana kama angkuwa na msimamo angekaa chini na mkewe kumwambia mambo aliyoyafanya yanatosha na sasa aachane nayo kabisa kwa faida ya familia yao, lakini kulalama tu bila kuchukua hatua madhubuti za kuzuia/kukomesha kabisa ufisadi mkubwa unaofanywa na mkewe haisadii chochote familia hiyo na waswahili walisema ZA MWIZI NI AROBAINI!

YouTube - Jamie Foxx featuring T-Pain - Blame It ft. T-Pain
 
Back
Top Bottom