...tick-tick!...Mke kanogewa na Ufisadi; Mume hajui la kufanya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

...tick-tick!...Mke kanogewa na Ufisadi; Mume hajui la kufanya

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Mar 27, 2011.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  [​IMG]...ni mke na mume waliodumu miaka 15 ya ndoa. Wamejaaliwa watoto wawili, miaka 12, na miaka 9. Wazazi wote ni waajiriwa wa serikali. Baada ya kujinyima hapa na pale, mume akaweza kujenga nyumba ya vyumba viwili, wakajistiri. Mke nae akajitahidi kukopa hapa na pale angalau wakaweza kununua 2nd hand (reconditioned) corolla tokea japan.

  Kimbembe kimeanza miaka mitatu iliyopita. Mke amebahatika kupangiwa ofisi nyeti ambayo inajihusisha na upatikanaji wa mapato ya serikali. Kufumba na kufumbua, mke kajenga nyumba mbili za kisasa kisha kazipangisha. Nyumba waliyokuwa wanaishi ameiongezea vyumba vingine vinne pamoja na vikorombwezo na nakshi mbali mbali. Almuradi maisha yao shwari mara kumi ya hapo awali.

  Kama hilo halitoshi, kawahamisha watoto public school na kuwapeleka kwenye Academy ambako kwa mwaka pamoja na vikorombwezo vingine, anawalipia mara kumi ya mshahara wake. Haikupita muda, kanunua brand New Toyota VX, na sasa ameagiza Range Rover Vogue (Sport) toka Uingereza kwa ajili ya mumewe.

  Jamaa (mume) pamoja na unafuu wa maisha, roho yake haimpi! anaona "likibumbuluka" ofisini kwa mkewe, watakumbwa waliokuwamo na wasiokuwamo. Kajaribu kumsahuri mkewe aachane au apunguze mabomu kazini, Mke hasikii la mwadhini wala mnadi swala!... anasema "tumeteseka sana kimaisha, acha nasi tujiliwaze kidogo!"

  Jamaa hajielewi elewi kabisaaa. Akifikiria ndoa, yake haijwahi yumbishwa kwa lolote miaka yote kumi na tano. Lakini, kasi ya mkewe na likilipuka, watataifishwa mali zote na huenda mkewe akaishia jela. Mzee wa watu anafikiria aanzie wapi kuepusha 'bomu hili la kutega'

  Mna maoni gani.
   
 2. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,137
  Likes Received: 851
  Trophy Points: 280
  Hapo jamaa ajaribu kutoka naye out, wakae, waongee na amshauri kwa uzuri kabisa hatari za ufisadi. Hapo walipofika inatosha, waendeleze walichokipata sasa!!
  Eeeeeh!!! Pia nimpe pongezi jamaa kwani inaonekana hiyo ndoa ni ya UKWELI!!
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...umeona ee? ndoa haina nyufa wala mpasuko,
  sema huyu ibilisi alivyomkaa huyu mama, anaona bado kwanza...
  mavuno nje nje...

  halafu unajua wengine tumekuzwa mwambao,
  kila nikitafakari, nawahofia na msemo "za mwizi arobaini"...
  Huyu mama anakula akimshika mkono kipofu.

  Anaona kwanini atoke jasho na kuumiza kichwa kwenye biashara,
  wakati anapanda, kupalilia na kuvuna kwenye kiti nyuma ya computer.
  Jioni anagawana mapato na serikali.

  Wakifanya mchezo, mume anaweza kusimamishwa mahakamani
  kama shahidi upande wa mashtaka!
  Si ushawahi sikia perversion of justice?
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Amtishe kwa yanayoweza kutokea akigundulika!Huyo mama nae kama ameshaboresha maisha si aache hako kamchezo?Japo kuiba sio sahihi ila atleast ukiiba iwe kwa kiasi sio anabeba mpaka upungufu uwe wazi!Alizochukua tayari awekeze ili awe na uhakika wa kesho the asafishe mikono!
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...bosi keshamaliza darasa na madaftari yote, kanukuu vifungu vya msahafu na biblia, mama haelewi somo.
  Imekuwa kama 'sikio la kufa!,' ndio maana huyu mheshimiwa ka panic! Mke jeuri ya pesa inaanza kuota mzizi,
  no wonder jamaa anatafuta njia achimbue kabla mmea haujakua na kuzaa matunda.

  Hivi mafisadi huanzia hivi hivi ee? haba na haba, tabia inazoeleka...
  Siku Auditors na vijana wa Hosea wakivamia ofisi, amekwisha.
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Duh! Huyo mama nae hashibi. Lol!
  Huyo baba aendelee tu kumsihi mkewe ila nae asiropoke ropoke maana kashakwambia wewe. Wewe nawe umeileta jf. Kabla ya hapa au baada ya hapa sijui utamwambia nani. Na huyu baba cjui kashawaambia wangapi. Kama namuona vile kwenye milango ya jela.
  Hilo dili habari yake kwishney.
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kweli nimeamini binadamu hatosheki, haridhiki
  Mama naona anatimiza ile PONDA MALI KUFA KWAJA

  Maisha yalimtesa weeeeeeeeeeeeeeeeeeee, sasa ni zamu yake kuyatesa maisha.
  Huyo mama hajashindikana ila hajapata usumbufu kisawasawa. Kama ni muumini mzuri wa dini basi inafaa watumike hata viongozi wake wa dini kumuonya kwamba Mungu hapendi anavyofanya (japo kufanya hivyo ni risk pia hasa ukizingatia siku hizi tuna viongozi wa dini wapenda mali)
  Jamaa aendelee kumsumbua tu waif mpaka ataacha
   
 8. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  dah! mama kaamua kuangamiza uchumi wa bongo kisayansi kabisa. dah!
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Mambo mengine inabidi uresort kwenye 'maombi' tu, watoto wamalize shule basi!
   
 10. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  apunguze kutumia hela kwenye magari,afanye investment za maana zaidi ya hizo nyumba......magari ni vitu vinavyoweka attention kubwa sana na ni rahisi kushtukiwa na kufuatiliwa....kama yuko dar,wajipange yeye na mume wake wafanye investment za maana nje ya Dar na iwe siri yao.....likibumbuluka huko awe na pa kuzamia,anaweza hata kuziweka kwa majina ya ndugu......!!!!

  Pia,atufikirie na sisi tunaohitaji hiyo kodi mahospitalini na kujenga miuondombinu.......aanzishe biashara amabyo itatengeneza ajira kwa wengine kupitia hiyo kodi yetu anayokula hapo.....kazi kweli kweli!!:washing:
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...aha ha ha ha!...aisee mmeniacha hoi kwa kicheko hapa.
  SMU by the time watoto wanahitimu shule huyu mzee si atakuwa keshakufa kwa woga?
   
 12. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  khaaaa! bado unampa maujanja ya wizi zaidi wakati sisi vibaka tukiiba sidiria ilioanikwa tu tunachomwaga moto? think! michelle think! utanipoteza kwa hali hii.
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Michele, jamaa mbinu zote hizo anazijua, tatizo shemeji yumo ki "rusha roho" zaidi!
  Nadhani aim yake, wote waliokuwa wanambeza enzi za ulala hoi 'waipate fresh!'
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Sasa huyo mwanaume hapo akileta ujuaji si anaweza 'kuchezea' talaka hivi hivi!?:glasses-nerdy:
   
 15. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mwache achimbe mafuta hayo,kikisanuka si basi.....lol, kama namuona huyo baba alivyokuwa 'mpole' baada ya hizo changes?!:lol::ballchain:
   
 16. S

  Smarty JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  hiv mbu huyu mama ni nani vile na yuko wizara gani vile???
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mnh, nakweli. Halafu umeshtukia mwanamke alivyo invest hata kwenye nyumba aliyojenga huyu mheshimiwa? Yaani kama kuondoka, jamaa ataondoka na mashati na suruale zake tu!
  Kweli hapo inabidi awe mpole akiombea wimbi la tsunami liwapitie mbali.

  Situations hii, mwanaume ametegeka sana. Hakuna Ujanja hapo.
  Mwanamke anasomesha watoto na kuitunza familia. Baba mwenye nyumba hana sauti tena.
  Inanisikitisha sana aisee...
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...duuuh, utanipa kamisheni % ngapi ku reveal info? miaka ile kulikuwa na fungu la 'tajirika na mrema'
  Anyway, classified Infos hazitolewi hadharani namna hii.
   
 19. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Cha muhimu wakae chini wajadiliane namna ya kuiba kwa Busara, kugawana pasu kwa pasu na Serikali siyo salama sana,, angalau apunguze achukue kama 20% kisha awe makini kwenye ku-clear documents, in case auditors wakitimba ofisini wasikute ushahidi..
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mbu embu naomba unifungue macho kidogo hapo nilipopigia mstari!!Kuna kitu hua kinanitatiza kutokana na hiyo kitu~!

  Alafu huyo mama shauri yake....kama nia yake ni kujionyesha hata siku akikamatwa ajue ataonyeshwa sana mpaka kwa ambao hakutaka wamuone!
   
Loading...