Kimsingi Tanzania tulipokuwa tumefikia tulihitaji mtu wa kurudisha utawala wa sheria. Sijaelewa vizuri kusema Serikali ya Tano inavunja haki za binadamu. Hivi mtu mmoja mwenye fedha kuzuia mradi wa maji wenye manufaa ya watu zaidi ya 4millioni huko siyo kuvunja haki za msingi za raia? Huduma za jamii ni kitu cha msingi katika taifa lolote linalojali maisha ya watu wake. Huyo jamaa ametia Serikali hasara kwa kuzui mradi huo kwa muda mrefu sana. Bei za vifaa vya ujenzi zimeongezeka, ufundi gharama zimeongezeka. Zaidi Serikali na Shirikia la maji limepoteza cash flow kwa zaidi ya 3 to 4 years kutoka mradi huo ulipotakiwa kuanza. Kilichokuwa kinaonekana kwa Tanzania ni watu wengi kujiweka kwenye kivuli cha haki za binadamu hata pale wao wenyewe wanapokuwa wanavunja haki kubwa za msingi. Tofauti ya upatikanaji wa haki ilikuwa tu nani mwenye uwezo wa kuhonga na nani hana. To me kinachoendelea ni muhimu ili kuweka mambo sawa na watanzania kujua kuwa kuna sheria na kuna mamlaka. Serikali katika kutoa huduma za jamii ina haki ya kubadilisha matumizi ya ardhi kwa maslahi mapema na nchi. Hili linafanyika hata katika nchi ambazo ndiko tunako copy haya mambo ya haki za binadamu. Kwa kweli tulifikisha nchi pabaya kwa mwavuli wa haki za binadamu wakati hizo haki na vyomba vya kaki vilikuwa vimetekwa na wenye hela. Haki za watu zinatenguliwa. Mtu anauza dawa za kulenvya akikamatwa unasema amevunja haki za binadamu. Nchi ya ajabu sana. Mkuu wa Wilaya ana haki na ana mamlaka na kuweka mtu mtu ndani kwa mamlaka yake pale anapoona kunatatizo. Soma katika mamlaka ya Mkuu wa Mkoa. Tatizo kubwa ni kuwa tulisahau kama Tanzania kuna sheria. Kila mtu Tanzania amekuwa mtaalamu, kila kona wababe, kila mtu yupo juu ya sheria. No Magufuli is doing just right at least for now.