Kwenye nchi zetu hizi masikini za Afrika, anahitajika dikteta kwa sababu wajinga ni wengi sana. Wanaoweza kudanganyika kirahisi tu ni wengi sana. Ndio maana waganga wa kienyeji na wachawi wanalo soko kubwa sana, ujinga ni mwingi, hivyo dikteta anasaidia katika kuwarudisha watu kwenye mstari.
Fisadi anaongeza ujinga kwenye jamii, tukumbuke kuwa kile anachokimiliki kinaongeza dhiki kwa mwananchi wa kawaida ambaye amezongwa na elimu duni, maradhi na shida nyingine nyingi tu. Fisadi mmoja asiyeona aibu kwenda Dubai kila mwisho wa wiki, wala hajiulizi kwamba kwa kufanya hivyo kuna watu wanaokufa kwa ubinafsi wake.
Udikteta wa JPM unazo neema kubwa sana kwa nchi hii, wakuu wa mikoa wamepelekeshwa mara moja tu tayari madawati yameshapatikana mengi sana, juzi waalimu wamepigwa mkwara mzito kule kanda ya ziwa kuhusu fedha za elimu bure.
Nchi za kiafrika zinahitaji madikteta wenye utu, wenye uthubutu wa kumpigania masikini, vinginevyo masikini atazidi kubaki masikini kwa sababu ya ubinafsi na roho mbaya ya fisadi.