An anal fistula is a small tunnel that develops between the end of the bowel (anus or rectum) and the skin near the anus. It's usually the result of an infection or abscess that didn’t heal properly.
Visababishi Vikuu vya Fistula ya Njia ya Haja Kubwa:
1. Majipu ya njia ya haja kubwa. Tezi ndogo ndani ya njia ya haja kubwa inaweza kuziba na kusababisha jipu. Jipu likipasuka au kutibiwa nusu, linaweza kuacha shimo au njia ndogo (fistula) kutoka ndani ya njia ya haja kubwa hadi kwenye ngozi ya karibu.
2. Ugonjwa wa Crohn. Huu ni ugonjwa sugu wa kuvimba utumbo (Inflammatory Bowel Disease). Wagonjwa wa Crohn huwa na hatari kubwa ya kupata fistula ngumu.
3. Kifua kikuu (TB) Ingawa ni nadra, TB inaweza kuathiri utumbo na kusababisha fistula.4. Majeraha katika eneo la njia ya haja kubwa kutokana na upasuaji, kujifungua, au majeraha ya kimwili.
4. Maambukizi ya ngono (STIs) kama HIV, kaswende, au kisonono huweza kudhoofisha kinga ya mwili na kuruhusu maambukizi ya mara kwa mara.
5. Matibabu kwa mionzi (radiotherapy)hasa kwa wagonjwa wa saratani ya sehemu za nyonga au njia ya haja kubwa, mionzi inaweza kuharibu tishu na kusababisha fistula.
6. Saratani. Ingawa ni nadra, saratani ya rektamu au ya eneo la njia ya haja kubwa inaweza kusababisha fistula.
7. Kufanya mapenzi ya kinyume na maumbile a.k.a kula tigo (yaani, kujamiiana kupitia njia ya haja kubwa) ni sehemu ya chanzo au kuchangia kutokea kwa fistula ya njia ya haja kubwa, hasa iwapo hufanyika bila tahadhari au kwa namna inayosababisha majeraha.
(Hapa inabidi tuweke kambi ndogo kabla hatujahitimisha na nataka
cocastic na group lake wasome kwa umakini kisha wajitathimini mwenendo wao)
Jinsi Mapenzi ya Kinyume na Maumbile Yanavyoweza Kuchangia Fistula:
1. Majeraha ya ndani : Ngozi na kuta za njia ya haja kubwa ni laini sana na hazijatengenezwa kwa shughuli ya kuingiziwa kitu mara kwa mara. Zinaweza kupasuka au kuumia, hasa kama hakuna ulainishaji wa kutosha (lubrication) au kama tendo linafanyika kwa nguvu kupita kiasi.
2. Maambukizi katika njia na mlango wa haja kubwa. Majeraha madogo madogo yanaweza kuruhusu bakteria kuingia na kusababisha abscess (jipu) ambalo baadaye linaweza kugeuka kuwa fistula. Visababishi kama mabaki ya shahawa za mwanaume,mafuta yasiyo rafiki na tussue na maumbile ya njia ya haja kubwa vinaweza tengeneza mazingira mazuri ya colon la bakteria hatarishi kuzaliana.
Pia kuna hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama HIV, kaswende, kisonono, na mengine yanayoweza kusababisha maambukizi ya kudumu sehemu hiyo.
3. Kuvurugika kwa tezi za njia ya haja kubwa. Tezi hizi hutoa ute na zinaweza kuzibwa au kuambukizwa kutokana na msuguano au majeraha yanayotokana na tendo hilo la kingono.
🚫 Tahadhari
Kuepuka kufanya ngono kinyume na maumbile kwasababu halina faida wala sio asili ya kimaumbie kuingiliwa njia ya haja kubwa kwaajiri ya starehe za kimwili. Ingawa si sababu na chanzo pekee au kikuu ya fistula ya njia ya haja kubwa, mapenzi ya kinyume na maumbile yanaweza kuongeza hatari, hasa kutokana na majeraha na maambukizi yanayoweza kufanyika bila tahadhari. Kwa hiyo, ni vyema kuachana na tabia hii chafu isiyo ya kiasili wala kibinadamu.
Namna zingine zinazochangia tatizo:
Usafi duni wa sehemu ya haja kubwa au maambukizi ya mara kwa mara vinavyoweza kutokana na kuugua Kisukari au kinga ya mwili dhaifu (mfano kutokana na HIV au dawa za saratani)
Upatwapo na hali hii wasiliana na watoa huduma za afya kwa maelezo na taratibu za kimatibabu.