Tiba ya mafuta ya ubuyu

Tiba ya mafuta ya ubuyu

mpungara

Member
Joined
Nov 16, 2011
Posts
75
Reaction score
17
ndugu zangu wana JF nimepita kona frani nikakuta jamaa wanajadiliana juu ya mafuta ya ubuyu kuwa yanatibu magonjwa mengi.sasa kwa wale wanaofahamu zaidi juu ya hili, naomba kujuzwa zaidi.
 
Tiba ya mafuta ya ubuyu




  • Kutibu na kurekebisha ngozi(kuimarisha ngozi) -Kuondoa makunyanzi,madoa meusi,chunuzi na mabaka
  • Kuimarisha ngozi na nywele
  • Kutibu moyo, Ini na figo
  • Kuondoa mafuta katika damu na mishipa ya damu
  • Kutibu vidonda na vidonda vya tumbo
  • Kurekebisha nuru ya macho na kusaidia macho kuona vizuri
  • Kusaidia utengenezaji wa chembe za mwili (seli) na kuimarisha kinga ya mwili kwa kuongeza CD4 kwa haraka
  • Kurudisha kumbukumbu
  • Na nyingine nyingi------------------------------Waweza kujipaka kama losheni,mafuta au waweza kunywa kijiko kimoja asubuhi na jioni kwa siku 15 au mara kwa mara...yatafute uanze kuyatumia....yanapendekezwa kwa wote

Ina aminika na baadhi ya watu kuwa ubuyu ni tunda lisilokuwa na thamani sana, kwani hata mtu akiwa anafanya biashara ya kuuza ubuyu hudharaulika, pengine ni kutokana na watoto na watu wa hali ya chini kupenda kutumia.

Lakini habari za hivi karibuni zinatoa taswira tofauti kuhusu tunda hili. Taswira hii inaweza kabisa kubadilisha mtazamo wa baadhi ya watu waliokua wakilidharau tunda hili. Hivi karibuni Jumuiya ya Ulaya (EU) imeidhinisha

kuingizwa kwa tunda hili barani humo kama tunda la kibiashara baada ya kampuni ya PhytoTrade Africa kupewa kibali cha kuingiza tunda hilo kutoka Afrika. Kampuni hiyo hivi sasa imeruhusiwa kuingiza ubuyu katika bara hilo na kutumiwa na wananchi wake kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuchanganya na vyakula mbalimbali vya nafaka ili

kuongeza virutubisho. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi,
Ubuyu una kiwango kikubwa cha Vitamin C kuliko chungwa. Imegundulika kuwa kiasi cha gramu 100 ya ubuyu ina miligramu 300 za vitamin C, kiasi ambacho ni

mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye tunda kama
chungwa ambalo ndilo linaaminika kuwa na kiwango kikubwa cha vitamin hiyo. Kama inavyojulikana, Vitamini C ni muhimu sana mwilini kwani ndiyo inayotukinga dhidi

ya magonjwa nyemelezi mbalimbali yanayoweza kutupata pale mwili unapokuwa hauna kinga ya kutosha, ndiyo maana hata hapa nchini imekuwa ikisisitizwa na wataalamu wetu wa lishe kuwa wagonjwa wenye upungufu wa kinga mwilini au wenye virusi vinavyosababisha
Ukimwi, wapende kutumia ubuyu ili kuongeza kinga zao. Hii

inatokana na ukweli kwamba ubuyu una virutubisho vingi vya kulinda mwili. Inaelezwa pia na watafiti kuwa ubuyu una vitamini muhimu inayojulikana kama
Vitamini B2 ambayo huimarisha ukuwaji wa nyama, ngozi na wa nuru ya macho. Halikadhalika kunavitamini B3 ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mchakato wa umeng'enyaji wa

chakula mwilini. Mbali ya vitamini, ubuyu pia una madini na mafuta aina ya
‘fatty acids'. Gramu 100 za ubuyu ina kiasi cha miligramu 293 za madini aina ya kalisiamu, miligramu 2.31 za potasiamu na miligramu hadi 118 za fosforasi (phosphorus). Hivyo utaona ubuyu ni muhimu kiasi gani kwa mwili wa binadamu kutokana na kusheheni

vitamini na madini hayo kwa wingi. Aidha, ubuyu unatibu pia ugonjwa wa
kuharisha kama vile ambavyo umekuwa ukitumiwa enzi na enzi na mababu zetu walipokutwa na tatizo la Kipindupindu au mfumko wa magonjwa ya

kuharisha na kutapika. Kwa mujibu wa habari za hivi karibuni, biashara ya ubuyu na Mafuta yake inatarajiwa kuongezeka barani Afrika, hasa nchini au mikoa inayolima tunda hili kwa wingi, kama vile Mkoa wa Dodoma na mingine.
UBUYU.jpg
 
Mkuu ile rangi inayo wekwa kwenye ubuyu haina madhara?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
MziziMkavu binafsi mdogo wangu amepona allerg kwa Mafuta ya Ubuyu,tangu amezaliwa mpaka sasa ana miaka 12 alikuwa yeye ni kukohoa,mafua na kuwashwa macho,amekunywa dawa mpaka utamuonea huruma.

Dada mmoja akatuambia kuhusu Mafuta ya Ubuyu, yeye mwenyewe alikuwa anayauza,na kwa kuwa tunamfahamu akatuambia tusimpe fedha kwanza ila tuchukue tukampe
huyu mdogo wangu na asipopona basi tusimlipe.

Sasa ni wiki ya tatu anaendelea na dozi hakuna cha kukohoa,mafua wala kuwashwa macho.

Nikaamini kweli karibu kila kitu kinachotuzunguka chaweza kuwa Dawa kwa binadamu.

Kwa hiyo mpungara hiyo ni dawa kweli.
 
Asante bibie.@Soray kwa kutuletea hapa Feedback mimi huwa ninapenda watu kama nyinyi kwa kutuletea hapa majibu ya dawa zetu ubarikiwe mbinguni. Sasa bibie kisukari jaribu kutumia hayo mafuta ya Ubuyu kwa faida zake hapo juu utaona wewe mwenyewe matokeo yake.
 
Last edited by a moderator:
Wakina Mzizi Mkavu,kuna mwanamama aliwahi kutuhadithia kuwa alikuwa na moyo ulipanuka ila sasa amepona kabisa.Mtusaidie
 
Na hayo mafuta yanapatikana wap?na bei yake

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Na hayo mafuta yanapatikana wap?na bei yake

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Ukiyataka yale 'origina' yanapatikana Dodoma au Singida. Lita moja inaweza kuwa kama Sh10,000 hivi (Kwa bei niliyoiona miezi kadhaa iliyopita)
 
Ukiyataka yale 'origina' yanapatikana Dodoma au Singida. Lita moja inaweza kuwa kama Sh10,000 hivi (Kwa bei niliyoiona miezi kadhaa iliyopita)
Unaweza nisaidia connection ya wauza mafuta ya ubuyu huko mkoani dodoma na singida?samahani
 
ndugu zangu wana JF nimepita kona frani nikakuta jamaa wanajadiliana juu ya mafuta ya ubuyu kuwa yanatibu magonjwa mengi.sasa kwa wale wanaofahamu zaidi juu ya hili, naomba kujuzwa zaidi.
Unga wake ni mzuri sana kwa kusafisha figo
 
Back
Top Bottom