Tiba ya babu na utawala usiofuata sheria

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
Tiba ya Babu wa Loliondo ni uthibitisho tosha wa utawala usiofuata sheria.
Hoja yangu hapa sio kama anatibu au la. Lakini hakuna taifa litaloacha watu wake kunywa dawa inayotolewa bila uthibitisho wa kitaalamu.
Sasa huko Rombo (kulingana na Raia mwema) ameibuka mtu mwingine anatoza shs 1000 kwa vikombe viwili na raia wa Kenya wanamiminika kunywa dawa yeye katokewa na bikira Maria na kuonyeshwa dawa hiyo.
Kwa kuwa serikali indirectly imemuunga babu mkono hawawezi kuzuia mwingine yeyote hata kama atawanyesha watu sumu au vitu visivyofaa.
Ilipaswa serikali ikae pembeni na kusisitiza kuchukua vipimo vya kawaida vya maabara kwa kuwa inaitwa DAWA.
Kama ni imani basi iwaachie wenye dini waisimamie. Inasemekana ( Kulingana na Mtanzania jana) watu 15 wanakufa karibu kila siku.
 
Back
Top Bottom