TIA Wamshukuru Rais Samia kwa kuwaimarisha Kitaaluma

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia kiasi cha Sh bilioni 7.8 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la taaluma. Hayo yamesemwa jana mjini hapa kwenye maonesho ya kilimo yanayofanyika eneo la Nyamhongolo katika Manispaa ya Ilemela na Mkuu wa Taasisi ya TIA Kampasi ya Mwanza, Dk Honest Kimario alipokuwa akizungumzia juu ya mafanikio ya taasisi yake katika kutoa elimu kwa umma.

Alisema fedha hizo zilizotolewa katika mwaka wa fedha 2021 / 2022 kupitia Wizara ya Fedha, zimeiwezesha taasisi hiyo kujenga jengo lenye vyumba vya madarasa vyenye uwezo wa kuhudumia wanachuo 1,100 kwa wakati mmoja.

"Lakini pia tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu jengo hilo lina maktaba ya kisasa yenye uwezo wa kuhudu-mia wanachuo 250 na ndani yake kuna majarida ya aina imbalimbali ya uchumi," alifafanua.

Alisema jengo hilo pia lina maabara ya kisasa ya kompyuta yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 200 kwa wakati mmoja na kufafanua kuwa ni jengo litakaloiwezesha taasisi hiyo kuwa na uwezo wa kusajili wanachuo 1,550.

Dkt. Kimario alisema ujenzi wa jengo hilo umefanywa kwa niia za kisasa zaidi na utasaidia kuwapata wanachuo wengi kutoka nchi za nje kwenda kusoma katika taasisi hiyo.
 
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia kiasi cha Sh bilioni 7.8 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la taaluma...
Dkt. Kimario bana dah, jamaa kapambana sana,

Ashakuwa mkuu wa chuo!

Hongera zake
 
Back
Top Bottom