TIA (Tanzania institute of Accountacy) Special thread:

TIA (Tanzania institute of Accountacy) Special thread:

Ngao ya Sponji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2018
Posts
341
Reaction score
545
Kwa wale waliochaguliwa Bachelor Chuo cha serikali TIA mwaka wa masomo 2018/2019 hii ni sehemu nzuri ya kukutana kujuzana Nini hasa kinahitajika ikiwemo ulipaji wa Ada na Malazi kwa wale wanaotoka Mikoani na mengine mengi. Karibuni
 
Now 2019/20
Remembering HALL III Room 25 wakati nikisoma NABOCE 1982/83; namkumbuka Mkuu wetu wa chuo Abdul Msina, nakumbuka na basi letu FIAT jeupe, Recreation Room tukicheza table tennis na darts. Wale tuliotoka kanda ya ziwa tuliitwa Magumagu; muda wetu wa kuoga ilikuwa usiku tu, au unavizia wenzako wakiwa class ili kukwepesha mikono ya sweta au filimbi zisionekane!! Vijana wa mjini walikuwa wakijua una mkono wa sweta au filimbi, taarifa zitafika mpaka HALL I (a.k.a Serengeti) bweni la wanawake!! Watu tulikatisha masomo kwenda makwetu kutoa mikono ya masweta na filimbi; tulivyorudi tukawa tunaoga kwa siku hata mara 8, mlango mwaaaa; ili waswahili waone; vitu bado pinkiiiii!! Mwisho wa mwezi tunapopata ile allowance ya shs. 120/= ilikuwa patashika kule Mtoni Kwa Azizi Ali; mishikaki, kuku, soda mpaka basii!! Jamani ilikuwa raha; kupanda Ikarus kwenda Posta kupitia Kilwa Road au Shimo la Udongo, nauli senti 50 ilikuwa burudani; acha tu!! Kweli siku hazigandi, dunia tunapita!! Kasomeni kwa bidii hapo chuo chetu pendwa, enzi zile DSA The Dar-es-salaam School of Accountancy.
 
Kwa wale waliochaguliwa Bachelor Chuo cha serikali TIA mwaka wa masomo 2018/2019 hii si sehemu nzuri ya kukutana kujuzana Nini hasa kinahitajika ikiwemo ulipaji wa Ada na Malazi kwa wale wanaotoka Mikoani na mengine mengi. Karibuni
Kwa nini unaandika accountacy badala ya accountancy wakati wewe ndiye ulitakiwa uwe unajua kuandika jina la fani yako kwa usahihi? Pia kwa nini unadai hii siyo sehemu nzuri ya kukutana na kujuzana vitu?
 
Nataka kufanya confirmation hawajanitumia code kila nikiwapigia hawapatikani kwenye simu inakuwaje nifanye
 
Sorry for the Inconvenience it may have caused you
Kwa nini unaandika accountacy badala ya accountancy wakati wewe ndiye ulitakiwa uwe unajua kuandika jina la fani yako kwa usahihi? Pia kwa nini unadai hii siyo sehemu nzuri ya kukutana na kujuzana vitu?
 
Back
Top Bottom