TIA: Nyoka mwenye vichwa viwili mwenye nguvu za ajabu

Salaam.
Nimekuwa nikipata habari za Nyoka aina ya TIA ambaye ana vichwa viwili, Nyoka huyu ana sifa ya kukaa katika misitu minene, yenye ubaridi mkubwa na unyevu nyevu.

Kwa mara ya kwanza, amesikika kuonekana kwenye Misitu ya Katavi sehemu ya mamba na amewahi kusikika kuwepo Mkoani Morogoro.

TIA nyoka wa ajabu anaelezwa kuwa na nguvu kubwa na wenyeji wa Mikoa ya Katavi na Rukwa wanamwita kuwa ni Fimbo ya Musa.

Inaelezwa na wenyeji wa Mikoa hii, Wafipa,wabende na wakonongo pamoja na wapimbwe kwamba wamekuwa wakipata wageni mbalimbali kutoka nchi mbalimbali wakiulizia viungo vya nyoka huyu kwa ajili ya matmizi yao.

''Juzi wamefika wachina wawili hapa wakitaka kiungo chochote japo kidogo kama punje ya mchele kwa gharama ya shilingi milioni 12 lakini hawajapata kwakuwa ni adimu'' alieleza mama Edita Kaniki Mkulima wa kijiji cha Mamba.

Nyoka huyu wa maajabu anatajwa kuwa na uwezo wa kutenganisha maji katika mito na bahari, wakandarasi wa miradi mikubwa humtumia.

Matumizi ya kiungo chochote cha nyoka huyu.

Inasadikikia kwamba, ukifunga kiungo chochote japo kidogo,damu au ngozi katika fimbo unaweza kuamuru mto kukatika bila kujali umefurika kiasi gani.

Unaweza kuamuru mvua kukatika, kuamuru kunyesha, kusimamisha wingu,jua kuwaka kwenye mvua nk.

Kwamba, ukiwa na kiungo cha nyoka huyu,unaweza kukata maji kwenye mto na ujenzi ukaendelea bila taabu.

Viungo vya TIA vinatumiwa pia na baadhi ya Watumishi wa Mungu katika ibada, akikugusa unaanguka na akiamuru upone unapona kweli.

Nyoka huyu wa ajabu, akiwa kwenye msitu huzungusha kamba kuzunguka eneo lake linalozidi ekari moja ,kamba ikikatika kuna nguvu kama umeme zinampa taarifa, hapo hapo husimamia mkia kuona adui aliyeko.

Taarifa kuhusu TIA nimezisikia hivi karibuni, zimenipa maswali mengi,nani anayejua zaidi kuhusu Nyoka TIA Maarufu ufipani
Kwa kifupi siamini habari hii.
Nyoka kama sumaku na anazuia mto?
Basi mito mingi ingekauka, na huyo si nyoka bali chuma chenye ncha chanya na hasi ya sumaku.
 
Hizi story kweli zipo tatizo huo uhakika wake sasa ndo shida,mwenye vithibitisho tafadhariii
 
Tiya hana vichwa viwili,ana kichwa kimoja chenye macho makubwa na ya kuvutia, ni mfupi mwenye rangi angavu ya kuvutia sana, hatembei kama nyoka wa kawaida, akiwa ktk matembezi ya kawaida hutembea kipande upande km katapila la minyororo linavyogeuka, sehemu yyte ambayo tiya hukaa mara nyingi pana mizoga ya wadudu na nyasi kavu hata km ni masika ya kijani kibichi,
Nyama ama mfupa wake ukiweka wembe una nasa km sumaku, ukiweka juu ya jani la mgomba linakauka,tiya dume ndo bongo, nyama yake ni nyekundu kupita wekundu wa kawaida, kuhusu kutega uzi ni sawa,lkn inasemekana japo ni mfupi akikuwa sana huota pembe dogo kichwani,
Kifupi ni nyoka wa maajabu, si nyoka wa kawaida
Jina lake kamili ni tiya nkwi
Yaani mkusanya kuni, jina hili limetokana na tabia ya yy kukusanya vjikuni kuzunguka makazi yake,
Nimependa nyongeza yako
 
Inasadikikia kwamba, ukifunga kiungo chochote japo kidogo,damu au ngozi katika fimbo unaweza kuamuru mto kukatika bila kujali umefurika kiasi gani.
Unaweza kuamuru mvua kukatika, kuamuru kunyesha, kusimamisha wingu,jua kuwaka kwenye mvua nk.
Kwamba, ukiwa na kiungo cha nyoka huyu,unaweza kukata maji kwenye mto na ujenzi ukaendelea bila taabu.

Imani ni kitu kibaya sana!!!
 
PAY-A-two-headed-snake-in-Kansas.jpg

ap-amazing-two-headed-animals-291211-02_042703.jpg

two-headed-snakes-02.jpg

maxresdefault.jpg

090805-two-headed-snake-picture_big.jpg

Two-Headed-Rhino-25898.jpg

part-003.jpeg

e1c781412e4857b510d20604a18baf58.jpg

photoshop-horse-10.jpg

Sasa kali ya yote, kuna demu mmoja anazo 2, moja bado chenza
 
Hakika haya mambo na nyoka hawa wapo hizi ni taarifa ya kweli kabisa.
Mfano mwakajuzi nilianika mpunga kijiji fulani kinaitwa mambo kipo mbarali Jirani na kijiji cha igurusi.
Jioni naenda kutoa/kuanua mpunga nilikutana na kitu cha ajabu ambacho sijawahi kukiona katika maisha yangu
Nilikutana na kitu kina miguu na ni kirefu kama nyoka pia kichwa chake kinaonekana kama jogoo, pia kilikuwa na manyoya

niliogopa sana sana
Baadae watu walikuja na kunambia huyo ni nyoka Hatari sana tena mno. Akikugusa tu na nyoya unakufa, bhasi watu wakamuua.

Baadae kidogo akaja mtu aliomba kumchukua yule nyoka akavaa Rambo mikononi akambeba yule nyoka na kuondoka nae kwa kudai babu yake alikuwa anamtafuta sana yuka yule nyoka kwa makumi ya miaka.

Ndugu zangu haya mambo yapo sana tena hapa mbeya kuna nyoka wa ajabu ajabu sana.

Lakini pia kijiji kimoja kinaitwa mbonile kipo mbeya vijijini kata ya ulenje, enzi hizo tunakua miaka ya tisini kulikuwa na nyoka wa ajabu sana , nyoka hao walikuwa wanaishi mtoni na ni wekundu kabisa ila ilikuwa nadra sana kuonekana.
Hawa nyoka wapo ndugu zangu mie nimewaona kwa macho yangu na wapo mazingira ambayo niko familiar nayo sana
 
Pamoja na yote hayo,ni rahisi sana kupata viungo vyake.ukimuwahi kumtemea mate anaganda.
 
Hizo picha ni za wanyama walemavu, yaani wana kasoro za maumbile "mutation", sio aina yao, sivyo walivyo kwa asili, ni kama mtu kuwa na vidole sita.
Nakubaliana na ww maana tumeshashuhudia watoto wanazaliwa na vichwa viwili au wengine wameungana
 
Hakika haya mambo na nyoka hawa wapo hizi ni taarifa ya kweli kabisa.
Mfano mwakajuzi nilianika mpunga kijiji fulani kinaitwa mambo kipo mbarali Jirani na kijiji cha igurusi.
Jioni naenda kutoa/kuanua mpunga nilikutana na kitu cha ajabu ambacho sijawahi kukiona katika maisha yangu
Nilikutana na kitu kina miguu na ni kirefu kama nyoka pia kichwa chake kinaonekana kama jogoo, pia kilikuwa na manyoya

niliogopa sana sana
Baadae watu walikuja na kunambia huyo ni nyoka Hatari sana tena mno. Akikugusa tu na nyoya unakufa, bhasi watu wakamuua.

Baadae kidogo akaja mtu aliomba kumchukua yule nyoka akavaa Rambo mikononi akambeba yule nyoka na kuondoka nae kwa kudai babu yake alikuwa anamtafuta sana yuka yule nyoka kwa makumi ya miaka.

Ndugu zangu haya mambo yapo sana tena hapa mbeya kuna nyoka wa ajabu ajabu sana.

Lakini pia kijiji kimoja kinaitwa mbonile kipo mbeya vijijini kata ya ulenje, enzi hizo tunakua miaka ya tisini kulikuwa na nyoka wa ajabu sana , nyoka hao walikuwa wanaishi mtoni na ni wekundu kabisa ila ilikuwa nadra sana kuonekana.
Hawa nyoka wapo ndugu zangu mie nimewaona kwa macho yangu na wapo mazingira ambayo niko familiar nayo sana
Mkuu siku nyengine tupigie picha
 
Hii si hadithi wakuu,ni habari ya kweli kabisa.Hawa nyoka walikuwepo wengi sana katika misitu minene ya mwambao wa ziwa Rukwa kati ya miaka 80 mpaka mwanzoni miaka ya 90.Lakini kutokana na uhitaji wake na wataalamu wa sayansi ya miti shamba waliwindwa wakaisha.Waambie hao wachina wanaotafuta waende huko wanaweza kubahatisha.
 
Back
Top Bottom