Leo Asubuhi
Member
- Apr 5, 2017
- 64
- 43
Salaam.
Nimekuwa nikipata habari za Nyoka aina ya TIA ambaye ana vichwa viwili, Nyoka huyu ana sifa ya kukaa katika misitu minene, yenye ubaridi mkubwa na unyevu nyevu.
Kwa mara ya kwanza, amesikika kuonekana kwenye Misitu ya Katavi sehemu ya mamba na amewahi kusikika kuwepo Mkoani Morogoro.
TIA nyoka wa ajabu anaelezwa kuwa na nguvu kubwa na wenyeji wa Mikoa ya Katavi na Rukwa wanamwita kuwa ni Fimbo ya Musa.
Inaelezwa na wenyeji wa Mikoa hii, Wafipa,wabende na wakonongo pamoja na wapimbwe kwamba wamekuwa wakipata wageni mbalimbali kutoka nchi mbalimbali wakiulizia viungo vya nyoka huyu kwa ajili ya matmizi yao.
''Juzi wamefika wachina wawili hapa wakitaka kiungo chochote japo kidogo kama punje ya mchele kwa gharama ya shilingi milioni 12 lakini hawajapata kwakuwa ni adimu'' alieleza mama Edita Kaniki Mkulima wa kijiji cha Mamba.
Nyoka huyu wa maajabu anatajwa kuwa na uwezo wa kutenganisha maji katika mito na bahari, wakandarasi wa miradi mikubwa humtumia.
Matumizi ya kiungo chochote cha nyoka huyu.
Inasadikikia kwamba, ukifunga kiungo chochote japo kidogo,damu au ngozi katika fimbo unaweza kuamuru mto kukatika bila kujali umefurika kiasi gani.
Unaweza kuamuru mvua kukatika, kuamuru kunyesha, kusimamisha wingu,jua kuwaka kwenye mvua nk.
Kwamba, ukiwa na kiungo cha nyoka huyu,unaweza kukata maji kwenye mto na ujenzi ukaendelea bila taabu.
Viungo vya TIA vinatumiwa pia na baadhi ya Watumishi wa Mungu katika ibada, akikugusa unaanguka na akiamuru upone unapona kweli.
Nyoka huyu wa ajabu, akiwa kwenye msitu huzungusha kamba kuzunguka eneo lake linalozidi ekari moja ,kamba ikikatika kuna nguvu kama umeme zinampa taarifa, hapo hapo husimamia mkia kuona adui aliyeko.
Taarifa kuhusu TIA nimezisikia hivi karibuni, zimenipa maswali mengi,nani anayejua zaidi kuhusu Nyoka TIA Maarufu ufipani