ma2mbo
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 697
- 326
Hata ulimwengu uliumbwa kwa fikra ndugu. Na yawezekana hao wanaolalamikia muziki hawafikiri. Sasa, hao mapacha waliwabeba weusi kwa kipato kilichotokana na nini? Kama ni muziki mbona leo waanze kulia? Kama ni ishu zingine kwa nini leo walilie muziki? Sijui kama huwa unapata muda wa kujiuliza haya.
Kadhalika haimaanishi kuwa kila afanyaye kazi serikalini kipato chake kinamtosha. Hivyo haimaanishi kuwa kila afanyaye muziki basi aendeshe benzi, maana ndivyo unavyotaka tuamini.
Kingine ninachokiona hapa ni suala la kufuata mkumbo kwa hawa wasanii. Kisa tu fulani kaimba basi nami naweza. Ukiacha hilo kuna suala la kudhani muziki ni kimbilio baada ya kukosa kwingine, hasa kutokana na kukimbia umande. Bangi na malengo wapi na wapi?
nimekwambia Mapacha wamewapa fadhili Weusi,utake ustake ukweli ndio huo,na sio hao kuna wengine wengi...na nimekwambia jamaa ni Wajasiliamali,hawategemei muziki tena...
sasa ngoja nikupe faida ya wao kutoishi kutegemea muziki,kikubwa wao hawaishi kwa kutegemea muziki,ndio maana wapo huru kuzungumza ukweli bila kuwaogopa wadau...watu kama Weusi hawawezi kuzungumza malalamiko yao hadharani sababu wanaogopa kubaniwa nyimbo kupigwa,na airtime ndio inawapa maonyesho maana ata albam hawauzi siku izi...
Na siku zote usijidanganye kuwa kila anaeng'aa kwenye radio au tvs ni mkali...wengi wanatengenezwa tu...usifikiri unapomsikia sana Diamond,then Bele9 umskii ukadhani Bele hana kitu,au kazidiwa kipaji na Diamond..kuna mengi yanafanyika nyuma ya pazia na nyie walaji mnalishwa yalivyopikwa kama yalivyo...we unajua siri ya Diamond kushain?au umejikuta tu unamkubali bila kuelewa kwa nini...ivi siku izi unaskia nyimbo za dansi zinachezwa?unajua kwa nini azichezwi?
Natumai tunakwenda sawa...